GE2025 Kitila azisaka kura, bila kujali mvua ilikuwa ikinyesha leo Dar

GE2025 Kitila azisaka kura, bila kujali mvua ilikuwa ikinyesha leo Dar

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
505
Reaction score
887
Muda huu hata wakiambiwa na wananchi walale chini kwenye tope ili wapate kura watalala tu!
==============
Leo Oktoba 7, 2025 Mgombea Ubunge wa jimbo la Ubungo Professa Kitila Mkumbo ameendelea na kampeni zake za nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa katika mtaa wa Kimara Baruti uliopo kata ya Kimara, Ubungo Dar es Salaam.

Pamoja na uwepo wa hali ya mvua Kitila aliendelea kuwatembelea waajiri wake(wananchi) kueleza aliyotekeleza pamoja na kuomba kura ili kupewa nafasi ya kuongoza kwa miaka mingine mitano.

Kitila aliambatana na mgombea Udiwani wa Kata ya Kimara Mhandisi Ismail Mvungi.
 
Haya majitu yametuharibia nchi vibaya sana, huu si uchaguzi ni uhuni tuu na kupotezeana muda and taxpayers money
 
Back
Top Bottom