'Kiti moto' ni salama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Kiti moto' ni salama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jan 18, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,008
  Trophy Points: 280
  SORCE: MWANANCHI

  WAZIRI wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk John Magufuli amesisitiza tamko la serikali kuwa nyama ya nguruwe, maarufu kama Kiti Moto, ni salama kwa kuwa hakuna taarifa za kuathirika kwa wanyama hao.

  Kuibuka kwa ugonjwa wa Mafua ya Nguruwe kulisababisha hofu kubwa nchini mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuua watu nchini Mexico, hata hivyo serikali iliwatoa hofu wananchi kwa kueleza kuwa nguruwe wa Tanzania hawajaathirika na kwamba ugonjwa huo unaambukiza kwa hewa na si kula nyama hiyo maarufu nchini.

  Mwishoni mwa wiki, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk John Magufuli alikuwa na kazi nyingine ya kuihakikishia Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Kilimo na Mifugo kuhusu wanyama hao.
  "Nguruwe wako salama," alisema Dk Magufuli kwenye kikao cha kamati hiyo jijini Dar es salaam.

  "Kama wangekuwa wana matatizo na kuathirika na homa hiyo hadi sasa tungekuwa tumepiga marufuku ulaji wake kwa wananchi.

  "Kwa hiyo wanaokula waendelee kula na wapo wanaendelea lakini wasiokula kama mimi tunaoita haramu, tusile."

  Alifafanua kwamba, wizara yake imekuwa katika mchakato wa kutekeleza Sera ya Taifa ya Mifugo ya mwaka 2006 na kuongeza kwamba rasimu ya mwisho ya mkakati huo imeandaliwa.

  Dk Magufuli aliongeza kwamba waraka wa Baraza la Mawaziri wa kupitisha mkakati huo umewasilishwa kwa katibu mkuu wa baraza hilo.

  Rasimu hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kuboresha mazao yote ya mifugo ili yaweze kuwa salama zaidi kwa mlaji. Mwishoni mwa mwaka jana, Tanzania ilikumbwa na tishio kubwa la homa ya mafua ya nguruwe na kufanya hata baadhi ya shule nchini hasa mkoani Mwanza kufungwa kwa muda.

  [​IMG]WAZIRI wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk John Magufuli ambaye amesisitiza kuwa nyama ya Nguruwe maarufu kwa jina la 'Kiti moto' iko salama, hivyo wananchi waitumie kama kawaida
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Jan 18, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kitimoto kwanini inapigwa sana vita, vijinenoneno haviishi, watu wanatuonea husuda na mnyama huyu basi tu, mara ooh ina mafua ya nguruwe, mara inalishwa ARV, mara sijui inanini sijui,
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  waambie maustadhi waendelee kusogelea.... KITIMOTO NI SALAMA...
   
Loading...