Nilianza kujua maana ya kiti cha Spika kwenye bunge la tisa. Kiti hicho kilijengwa na kuheshimika. Aliyekikalia akasema nitaendesha bunge hili kwa kauli mbiu kasi na viwango, kwa kimombo 'speed' and 'standards'. Samweli Sita pamoja na udhaifu wake kama binadamu alijenga na kuuimarisha mhimili wa Bunge.
Bunge likawa ni mahali pa kujadili hoja zenye maslahi mapana ya Taifa. Bunge lenye meno. Bunge lilifanya kazi yake ya kikatiba ya kuisimamia na kuihoji serikali. Nakumbuka kwa mamlaka aliyopewa Spika na kanuni za kudumu za Bunge kwamba yeye anaweza kukataa majibu, ama hoja ambazo serikali haikuzijibu vyema; yeye kila mara alitoa tahadhari kwa mawaziri kujibu hoja za wabunge kwa makini. Spika Sitta hakutumia kanuni kama fimbo bali alizitumia kuliongoza bunge.
Nakumbuka mbunge kama amekosea namna ya kuwasilisha hoja yake kulingana na kanuni alimfundisha namna ya kuliweka kibunge ili lipate majibu ya serikali. Na hii ndio kazi ya Spika na sio kuibeba serikali. Nakumbuka akiwaambia wabunge " Naamini serikali haijatoa majibu ya kutosheleza, nakuona mbunge hujaridhika; kaitengeneze vizuri ilete kama hoja mahsusi" ndiko kina Richmond walikopatikana.
Leo kiti cha Spika kimekaliwa na Serikali. Kwa tasfiri nyengine Serikali ina nguvu bungeni kuliko Bunge lenyewe. Kiti cha Spika kinafanya kazi ya kuijibia Serikali badala ya kuhakikisha wawakilishi wa wananchi yaani wabunge wanapata majibu ya kero za wananchi wao. Kiti cha Spika kina itikadi ya vyama, kina ushabiki.
Leo kiti cha Spika kina upendeleo katika mijadala, kinaruhusu matusi ya nguoni kutolewa kwenye chombo hicho kitukufu bila hatua yeyote. Wanaohoji kuhusu utaratibu sawia wa kuliongoza bunge wanaambia wana fujo, na wanatolewa nje na Kiti chc Spika kwa jazba isiyozingatia kanuni. Kiti cha Spika kinatunga kanuni baada ya kutoa adhabu. ULIONA WAPI?.
Leo tunambiwa haya yote tunayoyaona ni kwa sababu kiti cha spika kinaongozwa kwa remote control. Tanzania nchi yangu, Nchi iko 'Auto-Pilot', Bunge remote. Dah!
Hiki ni kiti cha Spika Wetu.
Wanabodi nyie mwaonaje kiti cha Spika.