Kiteto waja na mkakati mpya ukusanyaji wa mapato...

Kiteto waja na mkakati mpya ukusanyaji wa mapato...

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Serikali imesema halmashauri itakayoshindwa kukusanya mapato ya ndani na kushindwa kufika asilimia 80% itafutwa.

Lengo ni kutaka halmashauri ziwe na makusanyo makubwa ziweze kujiendesha kwa kutumia mapato yake ya ndani

Ili kufikia kipimo hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, TAMIMU KAMBONA amekuja na mpango mpya wa kuongeza minada na magulio wilayani humor.

Kwa sasa amefikia hatua ya kutangaza kupitia vyombo vya habari na hata vyombo vya mziki tarehe za kufanyika minada na magulio ili wananchi waweze kufika na kuuza bidhaa zao

Kufunguliwa kwa minada na magulio hayo wilayani humo kumelenga kutaka kutekeleza agizo la Serikali halmashauri kujiendesha kwa kutumia mapato yao.

Kila mwisho wa mwezi, kutakuwa na mnada wa Chapakazi, tar 1 utakuwa Dosidosi, 2 Kibaya, 14 Dosidosi 15 Kibaya 18, na 20 Kijungu na Sunya..

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Kambona anasema, usimamizi wa minada hiyo unaongeza mapato ya halmashauri, kwani awali mnada wa Dosidosi walipata 83,000 baada ya kuwa makini mapato hayo sasa yameongezeka mara dufu.

NI VYEMA WAKURUGENZI WAKAWA WABUNIFU LENGO LIKIWA NI KUIHUDUMIA JAMII..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ludisheni na kodi ya baiskeli, mikokoteni na punda....maana mapato yote ya Halmashauri sasa yamerudi serikali kuu!
 
Back
Top Bottom