Kiteto wahofia mabadiliko ya tabianchi

Kiteto wahofia mabadiliko ya tabianchi

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara ni moja ya eneo lililokubwa na mabadiliko ya tabia nchi mwaka jana na kusababisha madhara ya vifo vya Mifugo kwa wingi.

Madhara hayo yalitokana na mvua chache, pamoja na kuibuka magonjwa ya mifugo yaliyosababisha vifo kwa wingi

Hali hii imefanya wadau wa mamlaka ya hali ya hewa wakiwemo shirika la msalaba mwekundu, TMA, Ofisi ya Waziri Mkuu na mengine kuungana kunusuru hali hii kwa nyanja mbalimbali.

Akizungumza kwenye mafunzo ya umuhimu wa Taarifa za hali ya hewa, Tamimu Kambona, mkurugenzi wa halmashauri ya Kiteto amesema, mabadiliko ya tabianchi yakijitokeza tena Halmashauri yake inayotegemea asilimia 90 kwa mapato ya ndani itayumba.

Mafunzo hayo yaliandaliwa na shirika la msalaba mwekundu kwa kushirikiana na TMA kutoa elimu namna ya kukabiliana na majanga.

Mratibu wa mradi toka shirika la msalaba mwekundu, Bw. Allen alisema leo ni kuifanya jamii kuwa na uelewa wa kutosha juu ya hali ya hewa na namna ya kukabiliana na majanga.

Kwa upande wa TMA pamoja na mwakilishi toka ofisi ya Waziri Mkuu waliitaka jamii kutumia ipasavyo Taarifa za hali ya hewa pamoja na kuchukua hatua wanaposhauriwa kitaalamu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • IMG_0164.JPG
    IMG_0164.JPG
    33 KB · Views: 26
  • IMG_0266.JPG
    IMG_0266.JPG
    38.2 KB · Views: 26
Back
Top Bottom