ITV zingatieni maadili ya uandishi wa habari mmewatisha watoto leo kwa kuonesha mbuzi akichinjwa mubashara na wazee wa kimila wa Kiteto kumaliza mapigano ndani ya wilaya hiyo taarifa ya habari ya leo saa mbili za usiku. Kwa nini hamkutoa tahadhari kabla?
======
Wazee wa makabila manne makuu ya wilayani Kiteto wakubaliana kumaliza migogoro ya ardhi.
Wazee wa makabila manne makuu ya wilayani Kiteto mkoani Manyara yamemhakikishia waziri mkuu Mhe.Kassimu Majaliwa kwamba hakutakuwa na mapigano yatakayotokana na migogoro kati ya wakulima na wafugaji mara baada ya kuridhiana kwa kuchinja kondoo na kuku ili kukubaliana kutafuta amani ya kudumu,huku waziri mkuu akiwataka viongozi wa serikali kutatua mgogoro wa mpaka kati ya wilaya za Kiteto na Chemba.
Kauli hiyo ya wazee imefuatia baada ya kufanya maridhiano hayo kwenye msitu wa hifadhi ya kijiji cha Partimbo yakiwahusisha makabila ya Wamaasai,Wanguu,Wagogo na Wakamba kama sehemu ya kutafuta damu ya kupoza ardhi hiyo iliyosababisha zaidi ya watu 30 kuuwawa kikatili na mamia kujeruhiwa kwa nyakati tofauti.
Akipokea taarifa hiyo ya amani kufuatia kuwepo kwa maridhiano mbele ya wananchi wa mji wa Kibaya waziri mkuu Majaliwa amesema kutokana na migogoro hiyo serikali ya awamu ya tano haitavumilia viongozi kuwa sehemu ya vyanzo vya migogoro.
Hata hivyo katika ziara yake hiyo alitembelea hospitali ya wilaya na kuzindua ujenzi wa jengo la halmashauri ya wilaya hiyo iliyokuwa haina jengo kwa miaka 44 amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa pacha kujenga kwa kiwango,huku pia mbele ya watumishi akikemea dawa za kulevya kuanzia ngazi za kijiji na kuwataka wananchi kuwafichua.
Chanzo: ITV