Wizara ya Ardhi
Member
- May 14, 2024
- 79
- 62
Ikungi – Singida
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amewataka wananchi wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida kufanya mapatano ya amani kwenye migogoro ya ardhi inayowakabili katika maeneo yao.
Naibu Waziri Pinda amesema hayo Novemba 07, 2024 kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ambao wametoa salamu za pole kwa Mbunge wa Ikungi Mhe. Elibariki Kingu kufuatia kifo cha kaka yake Ibrahimu Immanuel Kingu ambaye amezikwa mkoani humo.
”Ikungi matatizo ya ardhi si mengi sana ingawa yapo, ardhi haingozeki isipokuwa idadi ya watu huongezeka. Kwa hiyo pataneni vizuri kwenye migogoro ya ardhi inayowakabili kwenye maeneo yenu”, Naibu Waziri Pinda.
Soma Pia: Naibu Waziri Pinda: Hekima itumike kutatua migogoro ya familia inayohusu ardhi
Naibu Waziri Pinda amesema kuwa Watanzania wanaungana na familia ya Kingu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na kuwasihi wanafamili, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kuwa wavumilivu kufuatia kifo cha ndugu yao.
Naibu Waziri Pinda amewasihi waombolezaji kuwa kila mwanadamu ni zawadi ya mwanadamu mwenzake na hata Mungu alipokuwa anawaleta duniani aliwaamuru kupendana na kuishi kwa upendo na kutumikiana kwa sababu watakuwa wanatimiza amri iliyo kuu ya upendo.