Jimbo la Kiteto: Taarifa kwa Wananchi wa Kiteto

Jimbo la Kiteto: Taarifa kwa Wananchi wa Kiteto

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430
TUMEPOKEA FEDHA KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO KIASI CHA SHS 949,200,000

Ndugu wananchi wenzangu wa Jimbo la Kiteto, nachukua fursa kuwafahamisha kuwa tumepokea fedha 949,200,000 Shs kwa ajili ya miradi ya maendeleo kama ifuatavyo:

Nimezungumza na Mhe. Waziri wa Tamisemi, Mhe. Mohamed Mchengerwa na amethibitisha kuwa pesa zimetumwa na Mkurugenzi wetu CPA Hawa Hassan Abdul amenithibitishia kupokelewa kwa fedha hizo na kuwa fedha hizo zitatumwa katika maeneo husika bila kuchelewa. Mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:

1. Ujenzi wa Shule ya Msingi Mpya ya Olmugi, Kata Namelock - Shs 350,500,000

2. Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Matundu 6 ya Vyoo Shule za Msingi Orgira, Kata ya Sunya - Shs 63,600,000

3. Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Matundu 6 ya Vyoo Shule za Msingi Malimogo, Kata ya Lengatei - Shs 63,600,000

4. Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Matundu 6 ya Vyoo Shule za Msingi Enguserosidan, Kata ya Laiseri - Shs 63,600,000

5. Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Matundu 6 ya Vyoo Shule za Msingi Nalangitomon, Kata ya Partimbo - Shs 63,600,000

6. Ujenzi wa Vyumba 3 vya Madarasa, Matundu 6 ya Vyoo na Madarasa na Vyoo ya Mfano ya Awali Shule za Msingi Kurash, Kata ya Lengatei - Shs 157,700,000

7. Ujenzi wa Nyumba ya Waalimu Shule ya Sekondari ya Ndirigish Kata ya Ndirigish - Shs 98,000,000

8. Ujenzi wa Vyumba 3 vya Madarasa na Matundu 6 ya Vyoo Shule za Msingi Orkitikiti (Engangongare), Kata ya Lengatei - Shs 88,600,000

Kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo la Kiteto, tunamshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote Serikalini kwa kuendelea kuboresha maisha yetu Wana Kiteto kwa kuendelea kutuletea miradi mikubwa ya maendeleo na kushughulikia changamoto za wananchi katika wilaya yetu. Ahadi za CCM zinaendelea kutekelezwa.

Ndugu wananchi wenzangu wa Kiteto, tunayo kila sababu ya kutoa shukrani kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupa fedha nyingi kwa ajili ya kutatua miradi ya maendeleo. Tumwombe Mhe. Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan Mwenyezi Mungu ampe afya njema na kumlinda vyema ili aendelee na maono yake mazuri katika kujenga taifa letu.

Mhe. Rais wetu mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kusikia kilio chetu kupitia sauti yenu Bungeni.

Ndugu wananchi wenzangu, kwa dhati kabisa nawahakikishia kuwa nitaendelea kuwa sauti yenu Bungeni na kuwawakilisha ipasavyo kwa unyenyekevu na uaminifu mkubwa.

*MUHIMU:*Natoa wito kwa watumishi wote kuhakikisha kuwa miradi hii inasimamiwa vizuri na kwa ufanisi mkubwa ili wananchi wapate huduma hizi kwa wakati.

Kiteto yetu inaendelea kung'ara!

Mungu Ibariki Kiteto!

Mungu Ibariki Tanzania!

Mungu ambariki Mhe. Rais wetu mpendwa Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge

Edward Ole Lekaita Kisau
(Mbunge wa Jimbo la Kiteto)

Leo tarehe 21.6.2024

Kazi Iendelee
 
Baba katoka kulewa na kugawa pesa kwa malaya karudi na vijisamaki kidogo kuwadanganyia familia yake.
 
Back
Top Bottom