Kitengo, sera za usalama CHADEMA viimarishwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitengo, sera za usalama CHADEMA viimarishwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WATANABE, Jan 17, 2012.

 1. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  "Kikao cha mwisho cha chama ambacho nilishiriki na Regia nilihudhuria kwa muda mfupi sana. Wenzangu watakumbuka mengine katika kila kikao kile. Mimi ninakumbuka moja tu ambalo ni moja ya sifa pekee aliyokuwa nayo na wanayo wanasiasa wachache sana na hasa wanasiasa vijana (ambao hupenda zaidi siasa za kuridhisha kwa kusema watu wapendacho). Regia alikuwa na uwezo mkubwa wa kusema usichopenda kusikia. Alisema tu. Katika kikao kile wajumbe na Wabunge walikuwa katika ‘emotion' sana kuhusiana na muswada wa mchakato wa kuandika Katiba. Mjadala ulikuwa mkali sana. Mwenyekiti wetu akampa nafasi Regia aseme. 'mimi nashauri tuombe kuonana na Rais Kikwete' yalikuwa ni maneno yake makali kupenya kwenye ngome za masikio ya wengi na yalipokelewa kwa mguno mkubwa. Mwenyekiti akaamrisha wajumbe na Wabunge watulie kwani Regia ana haki ya kutoa maoni yake. Mimi niliondoka baada ya muda mfupi maana nilikuwa ndio nimetoka nchini India kwa matibabu na nilikuwa na masharti ya kupumzika muda mrefu. Ushauri wa Regia (pamoja na wajumbe na viongozi wengine wa chama walioshauri ama waziwazi au kwa chinichini) ndio uliofuatwa na sasa kumekuwa na mazungumzo ya mara kwa mara ya viongozi kuhusu sheria ile ya mchakato wa kuandika Katiba. Huyu ndio dada Regia. Maisha mafupi lakini mafunzo makubwa katuachia vijana wenzake kwenye medani ya siasa".By Zitto

  Kufuatia taifa kugubikwa na wasiwasi mkubwa sana baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kupitisha muswada wa marekebisho ya Katiba huku ukiwa unalamikiwa karibu katika kila pembe ya nchi yetu; leo baada ya kupokea ushuhuda wa Mhe Zitto ya nini kilichojiri hata kuiacha Tanzania ikiwa salama salmini hadi leo. Ni dhahiri kuwa kifo cha ndugu yetu Regia Mtema kitakuwa kimeacha pengo kubwa katika taifa hili kwani alikuwa miongoni mwa watu wanaoweza kutoa suluhisho la amani na utulivu hata katika hali tete kama ilivyokuwa wakati huo.

  Ni kwa kuzingatia hilo natoa raia kuwa kitengo na sera za usalamaza CDM viimarishwe ili viweze kutoa ushauri wa mambo ya kiulinzi na usalama ili kupunguza ama kuepusha kutokea tena kwa kadhia kama hii. Ikumbukwe kuwa hii ni mara ya pili kwa mbunge wa CDM kufariki kutokana na ajali za barabarani, wa kwanza alikuwa Marehemu Chacha Wangwe.

  Na mara zote makosa ya kibinadamu ndio yametajwa kusababisha ajali hizi. Mathalani katika ajali ya Marehemu Chacha Wangwe yafuatayo yalibainika:-

  a) Dereva hakuwa na leseni ya kuendesha gari na kupatikana na hatia ya kosa hilo na mahakama na kuhukumiwa.

  b) Licha ya kutokuwa na leseni ya kuendesha gari, dereva alikuwa kiendesha gari husika kwa mwendo wa kasi sana.

  c) Kutokana na gari husika kusemekana lilihitaji matengenezo kabla ya kuanza safari, inadhaniwa kuwa gari halikuwa katika hali nzuri kumudu sfari hiyo achlia mbali kutumiwa na Mhe Mbunge.

  Katika ajali iliyopoteza uhai wa Regia Mtema yafutayo yanatajwa kusababisha ajali hiyo:-

  a) Mwendo wa kasi wa dereva (Vyombo vya habari vinataja kuwa Marehemu Regia ndio alikuwa dereva wa gari hilo wakati wa ajali).

  b) Kwa mujibu wa mmoja wa askari aliyeshuhudia ajali hiyo, dereva (Vyombo vya habari vinataja kuwa Marehemu Regia ndio alikuwa dereva wa gari hilo wakati wa ajali) alifanya kosa kwa kuamua kulifuata gari lingine lilokuwa mbele yake upande wa kulia ili kulipita gari lililokuwa mbele yao; hivyo gari lililokuwa mbele ya gari la marehemu lilipomaliza kulipta gari hilo, ghafla lilirudi haraka upande wa kushoto na kuliacha gari la marehemu likitazamana uso kwa uso na gari liliokuwa likija toka upande wa wa pili (Ruvu), ndipo gari la marehemu likalazimika kuingia porini na kupindika mara tatu.

  c) Kwa uzoefu wangu binafsi wa kuhusika na ajali na majadiliano niliyoyafanya na baadhi ya madereva ambao wamewahi kuhusika katika ajali mbali mbali na kunusurika; ajali hii haikuwa kubwa kiasi cha kusababisha vifo kama hatua mbali mbali za kiusalama zingekuwa zimezingatiwa, inadhaniwa kuwa marehemu na pengine hata abiria katika gari hilo hakuwa amefunga mkanda wakati ajali inatokea.

  d) Kwa kuzingatia hali ya marehemu kimaumbile, haikuwa kitu cha hekima na busara kuendesha gari lenye nguvu kama Toyota Land Cruiser. Sijui kama gari hili lilikuwa ni maalum kwa walemavu. Kama gari hili lilikuwa ni gari la kawaida haiingii akilini marehemu kwa hali yake ya kimaumbile aliwezaje kuruhusiwa kuendesha gari hili; Chama chake na Kikosi cha Usalama barabarani wailikuwa wapi kutochukua hatua mapema hadi Mbunge anapoteza maisha?

  Kwa kuzingatia hayo machache wakati sote tukiwa na uchungu mkubwa, ni vyema viongozi wa CDM wakaondoa dhana ambayo bado wanaoonekana kuwa nayo kuwa CDM bado ni chama kidogo. Hivyo wachukue hatua mara moja ya kuwa kuimarisha kitengo cha uslama pamaoja na sera ya usalama wa viongozi wao ili kuepusha majanga kama haya kutumaliiza viongozi wetu.
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Umenena vema. Ila swali langu ni je CDM wanashaurika??
   
 3. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Gud idea!
   
 4. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Risk assessment/management ni janga la kitaifa. Naungana mtoa hoja. Kuna mambo mengi yanalitia hasara taifa kwa sababu watu hatuachukulii mambo serously mpaka baya litokee, na likisahaulika tunarudi kama kawaida.
   
 5. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu umenena maneno ya mbolea.
   
 6. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Wasishaurike wao nani bwana, kama hawashauriki wataendelea kupukutika hivi hivi kizembe.
   
 7. m

  mpendadezo Member

  #7
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono, kwa mtazamo wa kawaida kulikuwa na uzembe, cdm wanatakiwa kuhakikisha usalama wa viongozi wao hilo ni jukumu la chama ukizingatia ndio chama kikuu cha upinzani.
   
 8. L

  Logician Senior Member

  #8
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Well said!
   
 9. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Risk assessment/management ni janga la kitaifa. Naungana mtoa hoja. Kuna mambo mengi yanalitia hasara taifa kwa sababu watu hatuachukulii mambo serously mpaka baya litokee, na likisahaulika tunarudi kama kawaida.
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unataka CDM wafanyeje?
  Wawakataze wabunge kuendesha? (Regia Case) wawakataze wabunge kuendeshwa? (Chacha Case) au wawasaidie wabunge (watu wazima) kuwaajiria madereva?

  Mnataka CDM wafanyeje?...............Kawashaurini NCCR Mageuzi, hao ndio wanashaurika. Why bother??!!!
   
 11. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Good speculation and narrations mkuu, wanatakiwa kufanya hivo,watambue wabunge wa cdm c mali ya chama tu bali umma usalama wao kuanzia vyakula,namna wanavosafiri nk uangaliwe kwa umakini
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  1.Katika kuongea na waombolezaji wenzetu da Rejia hakuwa na leseni na aliwahi kukamatwa na traffic akawatukana na kuwatishia kuwa mimi ni mh.mbunge tena wa chadema,msiniletee habari zenu apa.
  2.Rejia alimfukuza dereva wake kwa sababu (dereva) alikataa kuokoka.
  3.da Rejia alikuwa katika mwendo mkali sana wakati wa ajali (ameshasema mwenzangu apo juu).
  4.kwa hiyo apa hatumlaumu marehemu lakini ni vyema sana viongozi wa cdm hasa wabunge kuheshimu sheria za nchi hata kama hawawaheshimu watu wanaosimamia sheria hizo kwa usalama wa maisha yao na wale wanaowaongoza.
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  wabunge wenye ulemavu wanaponunua vyombo vya usafiri ni vyema chama kiwasimamie na zaidi iwepo sheria inayowabana wasiendeshe vyombo hivyo labda kwa dharura sana
   
 14. m

  masewa Member

  #14
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ushauri wako makini sana mkuu asiyetaka anamatatizo. CDM ni taasisi kubwa ni lazima ijari mstakabali wa washikadau wake wakubwa kama kinataka kusonga zaidi ya hapa
   
 15. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Laiti kama dada yetu asingepoteza maisha na wakapoteza maisha watu wengine katika hiyo ajali, unafikiri reputation ya CDM ingekuwa vipi ikizingatiwa wabunge ndio watunga sheria hivyo wanatakiwa kuwa kwanza kuonyesha njia ya kufuata sheria zilizotungwa na bunge. Ndio maana viongozi wakifika level fulani inakuwa ni lazima kuwa na dereva ili kuepukana na kadhia hizi na kuongeza usalama wa kiongozi husika.

  wawakataze wabunge kuendeshwa? (Chacha Case) Hii hata kama ni kuwaruhusu wabunge waendeshwe ndio waendeshwe na madereva wasiokuwa na leseni? Kama kitengo cha usalama kingekuwa na nguvu kingeweza kuratibu upatikanaji wa hawa madereva hivyo kukagua leseni zao n.k. Sio lazima kuwaiga CCM kila kitu,


  wao kwa kuwa ni chama dola wanaweza kuwaachia wabunge wao kumanage kila kitu lakini CDM inaweza kuja utaratibu mabadala ambao utaokoa heshima ya chama.

  Hapa siajkuelewa kwa kuwa umeanza kuingiza lugha za mitaani katika jambo sensitive.
   
 16. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Sio kwa wabunge wenye ulemavu tu: tukumbuke CCM ni chama dola hivyo all systems are in their favour. Hivyo wapinzani wanatakiwa kuwa more sensitive katika usalama wa wabunge wao in almost every aspect.
   
 17. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  H
  Wanashaurika warishauliwa kuonana na jk wakakubali towa ushauli wako
   
 18. F

  FUSO JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,867
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  ni kweli wakuu, ingawa si vizuri sana ku-discuss jambo hili wakati msiba ukiwa bado mbichi kiasi hiki, linaweza kuongeza machungu zaidi - nafikiri cha muhimu ni kama ulivyosema, lakini je nani anajua kwamba CDM hawana Guidelines za usalama wa viongozi wao wakiwemo wabunge? Nafikiri muda ukifikia tutawaomba CDM watueleze kama kitu hiki kipo basi watuambie au kama hakipo basi wakipangie mpango mkakati. Sisi wananchi ndiyo wadau wakuu wa chama hiki na ni kweli CDM sasa ni chama kikubwa.

  Ni kweli na wote kumbukeni kwamba barabara baada ya Ruvu Darajani mpaka Chalinze ina mawimbi sana, mara mbili mi nilishawahi kuyumba yumba na kigari changu SUZUKI, bila kushikiria usukani sawasawa sasa hivi nisingekuwa naandika hivi. kwa hiyo Guidelines kama hizo huwa zipo popote Kwa mfano kwa wale wapenda Kandanda kuna mchezaji mtukutu wa Man -City Mario Balotelli majira ya joto likizo alinunua pikipiki kule US, alipofika nayo Uingeleza Kocha wake alimkataza asiendeshe kabisa. nafikiri ni mambo haya haya ya usalama. Na kama angekiuka na akaendesha basi huwa ni faini hata karipio kali pamoja na kukatwa mshahara. Kwenye vyama pia nafikiri vitu hivi vinaweza kuwa implemented.
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  Jan 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu mtoa mada amenena vyema nawe pia umenena vema tu. Aliyosema mtoa mada ni kweli kabisa na kama ulivyosema timing yake kidogo haijakaa sawa, tungesubiri kidogo tu tumhifadhi mwenzetu kisha sasa ndio tuongelee mambo haya.

  Mkuu eneo kuanzia Mlandizi hadi Chalinze ni black spot kwa maana kwamba ni eneo ambalo ajali inaweza kutokea wakati wowote. Barabara hiyo imechoka na imejaa mawimbi hivyo riding quality yake iko chini ya kiwango. Inatakiwa madereva wawe makini sana eneo hilo. Ni muhimu pia serikali ikakarabati hako kakipande kwa kuwa kanachukua maisha ya watu wengi sana.
   
 20. N

  Nyalutubwi JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 572
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Duh! hiyo Logo yako imeniogofya sana.It was Sold for how much?.
   
Loading...