Kitengo, sera za usalama CHADEMA viimarishwe

hojja yako ni nzuri sana na mapendekezo yako yanaelewena na nakubaliana na wewe kabisa,kazi iliyopo ni uongozi wa CDM kuufanyia kazi ushauri wako.
 
Naunga mkono hoja yako, umekumbusha jambo moja la muhimu sana. Sera ya usalama CDM ipo, na kama
unavyosisitza wahimarishe kitengo kwa wakati huu, ambapo hofu imetawala ya kudhuliwa kwa viongozi wa upinzani.
Viongozi wa CDM ni wasikivu na wanatenda kazi kwa matakwa ya wananchi. Mawazo mapya na hoja za msingi za
maendeleo kwa nchi huwa wanazifanyia kazi mara moja, kwa hiyo swala lako limewafikia ni wasikivu.
 
Katika nchi hii Tz ambayo siasa zake zinafanyika ki adui sana(kwa chini chini) huku kukionekana dalili za kumalizana kisiasa kwa wale wanaoonyesha ujasiri wa kupinga maovu na kuipigania nchi, nadhani katika hatua za kujizatiti ni wakati muafaka kwa chama kama chadema ambacho kinaonesha mvuto na matumaini kwa jamii iliyochoka ya watanzania, kuanzisha idara maalum kwa ajili ya usalama...nikimaanisha.. a proper intelligence unit(si kikosi cha ulinzi kama sijui red/green/blue guard..no)....yaani wawe na proper intelligence unit ambao watafanya kazi underground..(kama wanavyofanya kazi TISS or mossad or CIA).....yaaani wawe properly trained nje ya nchi kama Israel or China or Russia(kuanzia sasa) ili waje waimarishe security haswa kama itakuja tokea chadema kuchukua dola(maana TISS wanawafanyia kazi ccm).Nasema hivi kwa kuwa naelewa chadema wamekuwa na mikakati kadha wa kadha ya kuchukua dola come 2015.....hivyo basi shime shime mikakati yao pia iliangalie hili suala(kama bado hawajalifikiria)na mipango ya kuanzisha hii intelligence unit ianze sasa fasta kwa vijana kupelekwa kusoma proper.Nasema hivi kwani kwa mambo ambayo tunayaona yakifanyika nchi hii haswa wakati wa chaguzi zetu kweli inauma saana...maana tumeona jinzi ambavyo TISS wameshiriki kuiingiza dola iliyopo madarakani,tunasikia hata sasa jinsi ambavyo maamuzi mengi yenye hujuma yanavyofanywa kwa kuwatumia hawa TISS na hata maandalizi ya ccm kuchukua dola tena 2015 huku wakiwatumia TISS.Hili jambo kama chadema watakaa tu bila kulifanyia kazi basi tusitegemee real change(itakuwa ngumu sana).....lazima kuwe na counter measures za kudili na counter intelligence issues ili kuwakabili hawa TISS kimbinu pale ambapo wameshaonekana kuingilia maamuzi mengi yaliyoonekana kuwapa faida chadema(haswa kwenye chaguzi zetu).....i just suggest....
 
Jamani mbona sijaona airbag zimefumuka? au ni mimi tu?

kweli kabisa umekumbusha jambo la maana sana, kwa staili ya wabunge usiku mchana wapo barabarani kati ya Dar na Dom ni muhimu ana magari yakawa na vifaa vyote vya kiusalama.
 
Kwa hiyo unataka CDM wafanyeje?
Wawakataze wabunge kuendesha? (Regia Case) wawakataze wabunge kuendeshwa? (Chacha Case) au wawasaidie wabunge (watu wazima) kuwaajiria madereva?

Mnataka CDM wafanyeje?...............Kawashaurini NCCR Mageuzi, hao ndio wanashaurika. Why bother??!!!

1.Gari zao zifungwe gavana, mwisho speed 60
2.wamdhibiti sugu asiendeshe gari wakati amestua ndumu.
 
Laiti kama dada yetu asingepoteza maisha na wakapoteza maisha watu wengine katika hiyo ajali, unafikiri reputation ya CDM ingekuwa vipi ikizingatiwa wabunge ndio watunga sheria hivyo wanatakiwa kuwa kwanza kuonyesha njia ya kufuata sheria zilizotungwa na bunge. Ndio maana viongozi wakifika level fulani inakuwa ni lazima kuwa na dereva ili kuepukana na kadhia hizi na kuongeza usalama wa kiongozi husika.

wawakataze wabunge kuendeshwa? (Chacha Case) Hii hata kama ni kuwaruhusu wabunge waendeshwe ndio waendeshwe na madereva wasiokuwa na leseni? Kama kitengo cha usalama kingekuwa na nguvu kingeweza kuratibu upatikanaji wa hawa madereva hivyo kukagua leseni zao n.k. Sio lazima kuwaiga CCM kila kitu,


wao kwa kuwa ni chama dola wanaweza kuwaachia wabunge wao kumanage kila kitu lakini CDM inaweza kuja utaratibu mabadala ambao utaokoa heshima ya chama.

Hapa siajkuelewa kwa kuwa umeanza kuingiza lugha za mitaani katika jambo sensitive.

Yaani uko juu mkuu,. Kamata tano. Unamaliza kabisa mwenye macho na aone na mwenye masikio asikie. Maneno na ushauri wako unapaswa kuzingatiwa lakini kuna watu wanabisha kila kitu.
 
"Kikao cha mwisho cha chama ambacho nilishiriki na Regia nilihudhuria kwa muda mfupi sana. Wenzangu watakumbuka mengine katika kila kikao kile. Mimi ninakumbuka moja tu ambalo ni moja ya sifa pekee aliyokuwa nayo na wanayo wanasiasa wachache sana na hasa wanasiasa vijana (ambao hupenda zaidi siasa za kuridhisha kwa kusema watu wapendacho). Regia alikuwa na uwezo mkubwa wa kusema usichopenda kusikia. Alisema tu. Katika kikao kile wajumbe na Wabunge walikuwa katika ‘emotion’ sana kuhusiana na muswada wa mchakato wa kuandika Katiba. Mjadala ulikuwa mkali sana. Mwenyekiti wetu akampa nafasi Regia aseme. ‘mimi nashauri tuombe kuonana na Rais Kikwete’ yalikuwa ni maneno yake makali kupenya kwenye ngome za masikio ya wengi na yalipokelewa kwa mguno mkubwa. Mwenyekiti akaamrisha wajumbe na Wabunge watulie kwani Regia ana haki ya kutoa maoni yake. Mimi niliondoka baada ya muda mfupi maana nilikuwa ndio nimetoka nchini India kwa matibabu na nilikuwa na masharti ya kupumzika muda mrefu. Ushauri wa Regia (pamoja na wajumbe na viongozi wengine wa chama walioshauri ama waziwazi au kwa chinichini) ndio uliofuatwa na sasa kumekuwa na mazungumzo ya mara kwa mara ya viongozi kuhusu sheria ile ya mchakato wa kuandika Katiba. Huyu ndio dada Regia. Maisha mafupi lakini mafunzo makubwa katuachia vijana wenzake kwenye medani ya siasa".By Zitto

Kufuatia taifa kugubikwa na wasiwasi mkubwa sana baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kupitisha muswada wa marekebisho ya Katiba huku ukiwa unalamikiwa karibu katika kila pembe ya nchi yetu; leo baada ya kupokea ushuhuda wa Mhe Zitto ya nini kilichojiri hata kuiacha Tanzania ikiwa salama salmini hadi leo. Ni dhahiri kuwa kifo cha ndugu yetu Regia Mtema kitakuwa kimeacha pengo kubwa katika taifa hili kwani alikuwa miongoni mwa watu wanaoweza kutoa suluhisho la amani na utulivu hata katika hali tete kama ilivyokuwa wakati huo.

Ni kwa kuzingatia hilo natoa raia kuwa kitengo na sera za usalamaza CDM viimarishwe ili viweze kutoa ushauri wa mambo ya kiulinzi na usalama ili kupunguza ama kuepusha kutokea tena kwa kadhia kama hii. Ikumbukwe kuwa hii ni mara ya pili kwa mbunge wa CDM kufariki kutokana na ajali za barabarani, wa kwanza alikuwa Marehemu Chacha Wangwe.

Na mara zote makosa ya kibinadamu ndio yametajwa kusababisha ajali hizi. Mathalani katika ajali ya Marehemu Chacha Wangwe yafuatayo yalibainika:-

a) Dereva hakuwa na leseni ya kuendesha gari na kupatikana na hatia ya kosa hilo na mahakama na kuhukumiwa.

b) Licha ya kutokuwa na leseni ya kuendesha gari, dereva alikuwa kiendesha gari husika kwa mwendo wa kasi sana.

c) Kutokana na gari husika kusemekana lilihitaji matengenezo kabla ya kuanza safari, inadhaniwa kuwa gari halikuwa katika hali nzuri kumudu sfari hiyo achlia mbali kutumiwa na Mhe Mbunge.

Katika ajali iliyopoteza uhai wa Regia Mtema yafutayo yanatajwa kusababisha ajali hiyo:-

a) Mwendo wa kasi wa dereva (Vyombo vya habari vinataja kuwa Marehemu Regia ndio alikuwa dereva wa gari hilo wakati wa ajali).

b) Kwa mujibu wa mmoja wa askari aliyeshuhudia ajali hiyo, dereva (Vyombo vya habari vinataja kuwa Marehemu Regia ndio alikuwa dereva wa gari hilo wakati wa ajali) alifanya kosa kwa kuamua kulifuata gari lingine lilokuwa mbele yake upande wa kulia ili kulipita gari lililokuwa mbele yao; hivyo gari lililokuwa mbele ya gari la marehemu lilipomaliza kulipta gari hilo, ghafla lilirudi haraka upande wa kushoto na kuliacha gari la marehemu likitazamana uso kwa uso na gari liliokuwa likija toka upande wa wa pili (Ruvu), ndipo gari la marehemu likalazimika kuingia porini na kupindika mara tatu.

c) Kwa uzoefu wangu binafsi wa kuhusika na ajali na majadiliano niliyoyafanya na baadhi ya madereva ambao wamewahi kuhusika katika ajali mbali mbali na kunusurika; ajali hii haikuwa kubwa kiasi cha kusababisha vifo kama hatua mbali mbali za kiusalama zingekuwa zimezingatiwa, inadhaniwa kuwa marehemu na pengine hata abiria katika gari hilo hakuwa amefunga mkanda wakati ajali inatokea.

d) Kwa kuzingatia hali ya marehemu kimaumbile, haikuwa kitu cha hekima na busara kuendesha gari lenye nguvu kama Toyota Land Cruiser. Sijui kama gari hili lilikuwa ni maalum kwa walemavu. Kama gari hili lilikuwa ni gari la kawaida haiingii akilini marehemu kwa hali yake ya kimaumbile aliwezaje kuruhusiwa kuendesha gari hili; Chama chake na Kikosi cha Usalama barabarani wailikuwa wapi kutochukua hatua mapema hadi Mbunge anapoteza maisha?

Kwa kuzingatia hayo machache wakati sote tukiwa na uchungu mkubwa, ni vyema viongozi wa CDM wakaondoa dhana ambayo bado wanaoonekana kuwa nayo kuwa CDM bado ni chama kidogo. Hivyo wachukue hatua mara moja ya kuwa kuimarisha kitengo cha uslama pamaoja na sera ya usalama wa viongozi wao ili kuepusha majanga kama haya kutumaliiza viongozi wetu.


sawa una idea nzuri, lakini kuhusu kuendesha gari hakuna tatizo kwani hata leseni za watu wenye ulemavu kama yeye zinatolewa pale TRA. Haruhusiwi kuendesha gari ambazo ni manual ila automatic anaendesha bila tatizo. hope kibaya hapo ni kama hawakuvaa mkanda. ila kibaya zaidi ni barabara zetu kuwa mbaya sana, kwa wale madereva wenzangu watakubaliana nami kuwa kutoka kibaha mlandizi mpaka chalinze, kutoka Gairo mpaka dodoma barabara inateleza sana na ina mawimbi makubwa, then ni finyu mno. Hivi ndo vyanzo vya ajali maeneo hayo na si kingine

 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom