Kitengo kipya cha kupokea malalamiko ya kodi

Nancyjoa13

Senior Member
Joined
May 18, 2018
Posts
167
Reaction score
97
"Serikali imeanzisha kitengo kipya cha kupokea malalamiko ya kodi na kitaratibiwa na Wizara ya Fedha na Mipango,
kitahusisha kupokea malalamiko kutoka kwa walipa kodi yakiwamo ya kuombwa rushwa na Watumishi wa Mamlaka ya Kodi TRA."

SERIKALI imependekeza kuchukua hatua za kisera na utawala kwa lengo la kuimarisha na kurahisisha ukusanyaji mapato ikiwemo kuanzisha kitengo huru cha kupokea malalamiko na taarifa za kodi kitakachoratibiwa na Wizara ya Fedha na Mipango. Kitengo hicho kitakuwa na jukumu la kupokea na kupitia malalamiko ya taarifa za kodi zitakazotolewa na walipakodi au watu wenye nia njema.

Aidha serikali inapendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwenye usimamizi wa viwango unaojumuisha ubora na usalama wa chakula na vipondozi ili Shirika la Viwango Tanzania (TBS) liendelee kusimamia eneo la chakula na vipodozi kwa ujumla kama ilivyo kuwa tangu mwaka 1975.

Serikali pia imependekeza kuimarisha na kurahisisha ukusanyaji mapato na kubuni mfumo wa kudhibiti michezo ya kubahatisha. Hayo yalisemwa bungeni jana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alipokuwa akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka ujao wa fedha.

Akizungumzia kuanzishwa kwa kitengo cha kodil; Waziri Mpango alisema;“Baadhi ya majukumu ya kitengo hiki ni kupokea malalamiko ya rushwa dhidi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Pia kupokea malalamiko ya ukadiriaji wa kodi na uthamanishaji wa bidhaa usio wa haki wala uhalisia dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania; Kupokea malalamiko ya matumizi ya nguvu katika ukusanyaji kodi dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania; Kupokea malalamiko ya ufungaji wa biashara bila kufuata sheria na taratibu dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.” Kuhusu TFDA na TBS, Waziri Mpango alisema katika bajeti hiyo serikali inapendekeza kurekebisha sheria ya TFDA.
 
Ikiwa malalamiko yatapokewa,yatafuatiliwa na kupatiwa ufumbuzi kwa muda muafaka basi itakuwa ni jambo jema.

Kinyume chake,kama ni kama yule jamaa aliyeagiza mzigo Zambia kalipa kodi,na kudaiwa rushwa kubwa ya kufa mtu,mwishowe ufumbuzi unapatikana baada ya miaka mitatu,tena mpaka rais mwenyewe ndiye aamue..basi tuna wakati mgumu.

Tunadhani huenda mambo hayatakuwa yaleyale.
IMG-20190605-WA0008.jpeg
 
Ikiwa malalamiko yatapokewa,yatafuatiliwa na kupatiwa ufumbuzi kwa muda muafaka basi itakuwa ni jambo jema.

Kinyume chake,kama ni kama yule jamaa aliyeagiza mzigo Zambia kalipa kodi,na kudaiwa rushwa kubwa ya kufa mtu,mwishowe ufumbuzi unapatikana baada ya miaka mitatu,tena mpaka rais mwenyewe ndiye aamue..basi tuna wakati mgumu.

Tunadhani huenda mambo hayatakuwa yaleyale.View attachment 1126667
Well said👍🏽👏🏽
 
Kiufupi, Kitengo hicho ni cha kuidhibiti TRA. Kama kitakuwa na watu waadilifu, migogoro ya kodi itapungua Sana na mapato ya Serikali yataongezeka. Kikiwa ni cha watu wasio waadilifu, ni bomu lingine linaundwa kwa kuzingatia majukumu yao nyeti.
 
"Serikali imeanzisha kitengo kipya cha kupokea malalamiko ya kodi na kitaratibiwa na Wizara ya Fedha na Mipango,
kitahusisha kupokea malalamiko kutoka kwa walipa kodi yakiwamo ya kuombwa rushwa na Watumishi wa Mamlaka ya Kodi TRA."
-Philip Mpango
#BajetiKuuTZ2019
This is what was missing. Kule TRA ni syndicate tupu. Hata ukamuone nani, hakuna la maana utakalopata.
Yule mbaba sijui kashafika njombe? Akapulizwe kwanza na baridi yenye kuleta ngiri apate akili
 
Sasa hivi TRA awapumui.Vijana wadogo wamenona mpaka unashindwa kujua huyu ni mzee au kijana.
 
Kabisa lakini kwamwendo huu wamzee jinsi unavyokwenda nakasi hii inatakiwa watumishi wa uma wabadilike tu vinginevyo watapukutika wengi sana kwakutumbuliwa.maana huyu mzee hataki masihara kabisaaa
Kiufupi, Kitengo hicho ni cha kuidhibiti TRA. Kama kitakuwa na watu waadilifu, migogoro ya kodi itapungua Sana na mapato ya Serikali yataongezeka. Kikiwa ni cha watu wasio waadilifu, ni bomu lingine linaundwa kwa kuzingatia majukumu yao nyeti.
 
Na takukuru wafanye kazi gani hebu acheni kuchezea pesa za walipa Kofi nyie washamba na malimbukeni wa karne .
 
Kiufupi, Kitengo hicho ni cha kuidhibiti TRA. Kama kitakuwa na watu waadilifu, migogoro ya kodi itapungua Sana na mapato ya Serikali yataongezeka. Kikiwa ni cha watu wasio waadilifu, ni bomu lingine linaundwa kwa kuzingatia majukumu yao nyeti.
Naungana na wewe mimi naamini watawaweka watu waadilifu sana na wasio na makandokando ya rushwa tangu utoto wao.
 
Niliwahi kusikia wao wanalipwa mishahara mizuri ili wasipokee rushwa.
Halafu nikasikia kuwa wao wapo wachache na mwisho nikaambiwa wao ndio wabeba kikapu kama yuda eskarioti aliebeba fedha na kumuuza Mkuu wake kwa fedha hiyo hiyo
Walimu tulipoomba kuongezewa mshahara tulipewa kinyume cha sababu hizo hizo ambazo kumbe hata wao serikali wameshaona haziwasaidii.

Standardization ya mishahara huo utakuwa muarobaini. Wenye Elimu sawa walipwe sawa hasa kwenye sekta za umma kwani kila MTU ana umuhimu wake
 
SERIKALI imependekeza kuchukua hatua za kisera na utawala kwa lengo la kuimarisha na kurahisisha ukusanyaji mapato ikiwemo kuanzisha kitengo huru cha kupokea malalamiko na taarifa za kodi kitakachoratibiwa na Wizara ya Fedha na Mipango. Kitengo hicho kitakuwa na jukumu la kupokea na kupitia malalamiko ya taarifa za kodi zitakazotolewa na walipakodi au watu wenye nia njema.

Aidha serikali inapendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwenye usimamizi wa viwango unaojumuisha ubora na usalama wa chakula na vipondozi ili Shirika la Viwango Tanzania (TBS) liendelee kusimamia eneo la chakula na vipodozi kwa ujumla kama ilivyo kuwa tangu mwaka 1975.

Serikali pia imependekeza kuimarisha na kurahisisha ukusanyaji mapato na kubuni mfumo wa kudhibiti michezo ya kubahatisha. Hayo yalisemwa bungeni jana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alipokuwa akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka ujao wa fedha.

Akizungumzia kuanzishwa kwa kitengo cha kodil; Waziri Mpango alisema;“Baadhi ya majukumu ya kitengo hiki ni kupokea malalamiko ya rushwa dhidi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Pia kupokea malalamiko ya ukadiriaji wa kodi na uthamanishaji wa bidhaa usio wa haki wala uhalisia dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania; Kupokea malalamiko ya matumizi ya nguvu katika ukusanyaji kodi dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania; Kupokea malalamiko ya ufungaji wa biashara bila kufuata sheria na taratibu dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.” Kuhusu TFDA na TBS, Waziri Mpango alisema katika bajeti hiyo serikali inapendekeza kurekebisha sheria ya TFDA.
 
Haya andika vizuri sasa kichwa cha habari umekuwa wa kwanza
 
Hii ni kuongeza ukiritimba tu; TRA iko chini ya Wizara ya fedha, halafu tena kitengo hicho nacho kiwe Wizara ya fedha.

Ni uppuzi tu. Tatizo kubwa liko kwenye muundo wa kodi zenyewe na mfumo wetu wa fedha.

Kodi nyingi ni za kukadiriwa na afisa wa TRA tu, hivyo lazima rushwa iwepo; ilitakiwa kodi ziwe za wazi kabisa.

Halafu mfumo wetu wa fedha bado haujaimarika kabisa kiasi kuwa watu wanafanya transacations za kibishara kwa fedha taslimu.

Kwa hiyo cash flow ya mfanya biashara inakuwa haijulikani sawasawa, na hivyo anaweza kudanganya katika kutoa kodi.

Matatizo kama haya yanaweza kutatuliwa kwa kuwa na flat rate tu katika kodi; na kusiwe na vikdoi vidogovidogo tena; yaani kodi iwe ni moja tu.

Kama ni import tax basi inaishia hapo, halafu sales tax nayo inaishia hapo.
 
Nakubaliana na mchangia hoja hapo aliposema kodi isiwe inakadiriwa na afisa wa kodi bali iwe kodi tambulishi kwa kila mlipa kodi
 
Back
Top Bottom