Kitengo cha Itikadi na Uenezi CCM: Tunaomba Ufafanuzi


dudus

dudus

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Messages
9,723
Likes
10,149
Points
280
dudus

dudus

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2011
9,723 10,149 280
Mkuu salaam. Naamini yote yanayoendelea katika nchi yetu hususan mambo mazito yaliyoibuliwa au kutokea hivi karibuni na mijadala mbali mbali kuibuka Bungeni na mitaani yamefika Ofisini kwako. Mkuu wangu, kwa faida ya wale ambao pengine hawako "aware" naomba tukumbushane tena matukio machache:-

(i) UFISADI: Sasa imedhihirika rasmi kwamba kumbe MAGAMBA pekee sio wale wachache uliowahi kututajia hapo kabla. Imedhihirika tatizo la UFISADI serikalini na chamani ni kubwa kuliko ambavyo tungeweza kudhania likihusisha watendaji wakuu kabisa wa Wizara hadi watendaji wadogo huko halmashauri. Kwa ufupi ni tatizo la kimfumo - mfumo wa chama chenu. Tunaomba ufafanuzi wako ni vipi Chama chako kimejipanga kupambana na tatizo hili au ni lini mtatoa tena tamko la kuwataka wahusika wote wajivue gamba na mtawachukulia hatua zipi za kinidhamu na kisheria.

(ii) WANACHAMA KUIKIMBIA CCM: Ni kweli kila mtanzania ana haki ya kujiunga na hata kuachana na chama chochote cha siasa kadiri anavyoona inafaa. Hili wimbi la wanachama na hata viongozi wa ngazi mbali mbali kuikimbia CCM unalichukuliaje? Uliwahi kutuaminisha kwamba wote wanaoondoka CCM ni magamba; hivi kweli umati wote huu unaohama ni magamba? Unadhani ni nini hasa wanachokikosa huko CCM hadi kuwafanya wahame kaka?

(iii) KEBEHI KWA UPINZANI: Imekuwa ni desturi kwa viongozi wa CCM kuvidharau vyama vya upinzani na kudai havina ajenda na hasa Chadema wakidaiwa hawana ajenda nyingine zaidi ya UFISADI. Kwa haya yanayodhihirika si sahihi kwamba wapinzani wako sahihi kwamba adui namba moja wa taifa letu ni UFISADI unaolelewa na CCM na hivyo basi kwa maana nyingine adui namba moja ni CCM? Tafadhali toa kauli yako Mkuu.

(iv) KUKOSEKANA UWAJIBIKAJI: Imekuwa ni desturi pale viongozi wanapobainika kufanya madudu kutowajibika na kwa bahati mbaya sana kuna kila dalili kwamba wanalindwa na "mamlaka iliyo kuu". Ndio kusema kwamba siku hizi chama chako kimeweka pembeni miiko yake ya uongozi - kutosema uongo, kutopokea rushwa (ufisadi), cheo ni dhamana, n.k?

(v) CCM KUINGILIA MIHIMILI YA DOLA: Ni jambo lililo wazi kwamba chama chako kinaingilia maamuzi au uhuru wa vyombo vya kikatiba vya wananchi hususan Bunge. Ni lini desturi hii itakoma? Au bado ile dhana ya "CCM ITATAWALA MILELE" bado ingalipo?

(vi) URAIS WA KIFALME: Kwa kutokuwa na maono wabunge wa Chama chako kwa kshirikiana na wale wa CUF waliwahi kumshambulia vilivyo Mh. Tundu Lisu (Mb) pale alipojenga hoja ya urais wa kifalme akilenga hasa kupunguzwa kwa madara ya Rais ili kulisaidia taifa na sio kumshushia hadhi Rais wetu bali kumpunguzia mzigo mzito alio nao. Kwa bahati mbaya kipindi kile Mh. Lissu hakueleweka vizuri lakini yanayotokea leo nadhani tumemwelewa alikuwa anamaanisha nini. Sijui wewe una maoni gani katika hili.

Kazi njema katika kukitumika chama chenu.

Wasalaam, dudus.
 

Forum statistics

Threads 1,275,100
Members 490,908
Posts 30,532,670