Kitenge: Simba hata wangecheza siku 3 mfululizo wasingeweza kufunga wydad Casablanca

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
15,777
24,211
Wydad Umepigaje Hapo?

Kipindi Cha Pili

Sub ya kuingia Chama,Phiri,Miqqusone na Mzamiru ilikuwa na maana hii
1.Kuongeza Kasi kwenye eneo la mwisho labuwanja(zone C)
2.Kuongeza ubunifu (Chama)
3.Kupunguza hatari ya Kanoute ambaye alikuwa na Kadi ya njano

Sub hizi ilikuwa ni kamari kwasababu zilienda kupunguza pressing ya Simba kwenye mbele ya line ya kwanza Wydad kwa hiyo ule muundo wa 4+2 ukawa umekufa kwasababu Benchika alikuwa anataka ku attacks space zilizokuwa zinaachwa na Wydad wakati wamesogea juu kushambulia.

Simba hata wangecheza siku tatu wasingeweza kufunga goli mechi ya Jwaneng Galaxy,Asec Mimosa na Wydad huoni goli linatokea wapi.

Jean Baleke kadiri siku zinavyozidi kwenda Kuna kina kinapungua kwake.

NB
Unaruhusiwa kucheka kama timu yako ina alama zaidi mbili kwenye kundi.

Full-time

Wydad 1-0 Simba

@omarrkombo
1702182695089.jpg
 
Simba nae angekuwa kundi la Yanga; angekuwa na Point 5
Nayaona kabisa maumivu yako, jana umeumia sana mtani, tafuta kinywaji baridi sijui wanaita Kombucha tangawizi flani amazing (chungu lakini)!

5imba Guvu moyaaaa Pira objektiv inawatesa sana! Mbumbumbu wengi mtaishia mirembe hosp kwasasa maana mmejaa sumu na ghadhabu!

Ukimtania mwana thimba yuko mkiani ni makonde tu sasa hivi maana Ile jana nyani katema bungo ikawa utatoa utoi utatoa utoi utatoa utoi msako wa karne wa namtaka mke wangu, hatimae mbumbumbu wakakata pumzi na kutoa! aisee noma sana, thimba wakakandwa dkk za jiooooni kabisa!!

Kama unajali usalama wako wakati unaongea na mwanathimba fasta geuza msimamo wa kundi chini juu , juu chini hapo mtakaa pamoja kunywa supu! Na atacheeeeka maana ni mbumbumbu hawa watani zetu!

Wanathimbaaaaaa!
 
Kweli kabisa Phiri aliingia na kucheza kwa kasi na kujiamini, akiwapunguza sana Wydad japo hakupata mtu wa kampa kampa tena, mi ni uto ila nilimkubali jana japo alicheza kwa muda mfupi.
Kwa hiyo aliwala sana chenga wydad?🤣🤣🤣. Watanzania tunauliza magoli yapo wapi nyie mnatamba kuwapunguza waydad?!😡😡
 
Kweli kabisa Phiri aliingia na kucheza kwa kasi na kujiamini, akiwapunguza sana Wydad japo hakupata mtu wa kampa kampa tena, mi ni uto ila nilimkubali jana japo alicheza kwa muda mfupi.
Kabisa mkuu Mimi ni kolo ...ila tungekuwa na pacome.....tungeshinda mapema sana
 
Wydad Umepigaje Hapo?

Kipindi Cha Pili

Sub ya kuingia Chama,Phiri,Miqqusone na Mzamiru ilikuwa na maana hii
1.Kuongeza Kasi kwenye eneo la mwisho labuwanja(zone C)
2.Kuongeza ubunifu (Chama)
3.Kupunguza hatari ya Kanoute ambaye alikuwa na Kadi ya njano

Sub hizi ilikuwa ni kamari kwasababu zilienda kupunguza pressing ya Simba kwenye mbele ya line ya kwanza Wydad kwa hiyo ule muundo wa 4+2 ukawa umekufa kwasababu Benchika alikuwa anataka ku attacks space zilizokuwa zinaachwa na Wydad wakati wamesogea juu kushambulia.

Simba hata wangecheza siku tatu wasingeweza kufunga goli mechi ya Jwaneng Galaxy,Asec Mimosa na Wydad huoni goli linatokea wapi.

Jean Baleke kadiri siku zinavyozidi kwenda Kuna kina kinapungua kwake.

NB
Unaruhusiwa kucheka kama timu yako ina alama zaidi mbili kwenye kundi.

Full-time

Wydad 1-0 Simba

@omarrkomboView attachment 2838223
Chombo cha habari kisicho na habari.
 
Back
Top Bottom