Kitendawili cha nani awanie Jimbo la Kiteto chatenguliwa

Kitendawili cha nani awanie Jimbo la Kiteto chatenguliwa

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Jimbo la Kiteto limewekwa sawa baada ya mvutano mkali kujitokeza kati ya Mbunge aliyemaliza muda wake Ben Nangoro na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Emmanuel Papian kutangazwa rasmi kuwa mshindi wa kura za maoni

Awali Emmanuel Papian alishinda kwa zaidi ya kura elfu tisa dhini ya mbunge wa zamani Ben Nangoro aliyekata rufaa na kuibua mvitano mkali uliosababisha madhara makubwa

Baadhi ya madhara hayo ni kuvunjwa vioo gari la Ole Sendeka aliyetuhumiwa kuja kumfanyia kampeni Nangoro akiwa na kamati ya Siasa ya Mkoa

Pia katika kuweka mambo sawa Jeshi la Polisi wilayani Kiteto lililazimika kutumia mabomu ya machozi kumwokoa Ole Sendeka na wajumbe wa kamati ya Siasa ya mkoa na Ole Nangoro waliokuwa Ofisi ya CCM kuhakiki matokeo

Nderemo na vifijo vilisikika majira ya saa 12 za jioni hii leo baada ya taarifa kutolewa na chanel five kipindi cha hot mix kuwa EmmanueL Papian ameteuliwa rasmi kugombea Jimbo hilo kupitia CCM
 
Kuvunjwa kioo gari ndio madhara makubwa??!!

Kama wewe ni sehemu ya timu ya huyu jamaa wa "Internet" baai jimbo litakuwa tupu sana
 
Back
Top Bottom