Kitchen party: Ina faida kweli?

Kitchen party: Ina faida kweli?

Kwetu-Mbagala

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
203
Reaction score
39
WanaJF, katika miaka ya hivi karibuni, ktk jamii na familia zetu, kumekua na mashamsham hasa wenzetu wanapofunga ndoa. Miongoni mwa shamrashamra hizo imekua ni kuwafanyia dada zetu 'sherehe ya jikoni' (kitchen party).Lengo kuu la sherehe hiyo ni kuwaandaa dada zetu ili waweze kutimiza vyema majukumu yao ya kifamilia ndani ya ndoa. Kwa sasa binafsi inashangaza kwa wanandoa wapya (pamoja na wadada kufanyia kparty) utakuta bw harusi kavaa shati limejikunja(halijanyooshwa), mabwana harusi wapya asubuhi tunakunywa nao chai magenge (inamaanisha asb wanatoka bila ya kuandaliwa chochote), wengine mpk jioni wanakula magengeni. Pia wengine ndani wiki moja wanaanza kuchepuka nje (inamaanisha kuwa ndani hawatosheki/waharidhishwi?).Hakika haya yananipa wasiwasi kuhusu kparty, je ni kweli zina faida au tunapoteza muda tu? Tafakari, chukua hatua.Karibuni Mbagala..
 
hao wanaume ndo wawekwe nao kitchen part coz ktk kitchen part ya dada hatufunzwi kumfunga mume kamba ili asile,asinye na kutoka nje 2wafundishwa......................
 
Kuna faida sana tu tena nyingi nikianza kuorodhesha hapa sitamaliza na ntachelewa kumhudumia hubby...
Na masaa machache ya siku ya kitchen party hayawez badilisha tabia ya mdada,namaanisha kama mdada hajui kupika na mchafu hyo cku ya kitchen party haiwez kumrekebisha,so pale wengine tupo kukusanya zawadi maana nasis tumetoa sana.
Ivo vitu vidogodogo vinavyoleta maana katika ndoa mwanamke unapaswa kuvijuaga cku nying kama kujua kupika vizuri na shughuli za usafi...
Kitchen party ziendelee kuwepo tu kwakweli
 
Faida yake ni kupata zawadi ImageUploadedByJamiiForums1381763754.597329.jpg
 
nikiskia kitchen party kitu kinachokuja kichwani faster ni zawadi tuu
 
yaani mtu mzima na akili zake atoke asubuhi shati limejikunja halafu umshangae mkewe badala ya kumshangaa mwanaume mwenzako?

Usmart ni hulka ya mtu

Kuna mijanaume mingine kuoga tu kwa mbinde sembuse kuvyaa shati lililonyooka

Halafu hao wake zenu wawafunge kamba ili msile magengeni?

Huyo mwanaume hajui wajibu wake kula nyumbani? Au ndo hao nyumbani hawaachi au wanaacha hela ya mchicha wao wanaenda kunywa supu au nyama choma bar

Ndoa zina mengi sana heri ushughulike na yako ya wenzio waachie wenyewe

Mkuu umemaliza kila kitu. Yaani mwanamke alaumiwe kisa mumewe kavaa shati lililojikunja hivi huyu mvaaji yeye hana macho na mikono ya kujinyooshea. Kwanini tusijiulize kwamba huyu mkaka alikua anaishije kabla ya kuoa. Unajua kuna wanaume wabinafsi halafu walalamishi yaani wanapenda kuwaaibisha wake zao utafikiri kuoa walilazimishwa. Kitccheni party kazi yake sio kumfunda mwali bali ilianzishwa kwa makusudi ya kukusanya vyombo manake huko nyuma kwenye hausi watu walikua wanajikuta wanapokea zawadi za aina moja kama vile chupa ya chai n.k . Ng'ombe hanenepi siku ya mnada kama alivyosema PLL
 
Last edited by a moderator:
Ahsante sana Ablessed yaani kuna baadhi ya wanaume wanajidekeza kupita kiasi!!!! Nimeshawahi kuona hapa mtu kaanzisha uzi mkewe hakumpelekea ndoo ya maji ya kuoga!!!! Utadhani yeye angeibeba ndoo hiyo mwenyewe mikono ingekatika!!!! Umevaa shati limejikunjakunja kama halijaguswa na pasi kwa miaka chungu nzima wa kulaumiwa ni Mke!!!! Dah!!!!!

Mkuu umemaliza kila kitu. Yaani mwanamke alaumiwe kisa mumewe kavaa shati lililojikunja hivi huyu mvaaji yeye hana macho na mikono ya kujinyooshea. Kwanini tusijiulize kwamba huyu mkaka alikua anaishije kabla ya kuoa. Unajua kuna wanaume wabinafsi halafu walalamishi yaani wanapenda kuwaaibisha wake zao utafikiri kuoa walilazimishwa. Kitccheni party kazi yake sio kumfunda mwali bali ilianzishwa kwa makusudi ya kukusanya vyombo manake huko nyuma kwenye hausi watu walikua wanajikuta wanapokea zawadi za aina moja kama vile chupa ya chai n.k . Ng'ombe hanenepi siku ya mnada kama alivyosema PLL
 
Ahsante sana Ablessed yaani kuna baadhi ya wanaume wanajidekeza kupita kiasi!!!! Nimeshawahi kuona hapa mtu kaanzisha uzi mkewe hakumpelekea ndoo ya maji ya kuoga!!!! Utadhani yeye angeibeba ndoo hiyi mwenyewe mikono ingekatika!!!! Umevaa shati limejikunjakunja kama halijaguswa na pasi kwa miaka chungu nzima wa kulaumiwa ni Mke!!!! Dah!!!!!
Hahahahahahahaha unajua kuna wengine ni wachafu toka huko. Haingii akilini kijana anaejipenda akavaa shati limejikunja au socks zinazotoa harufu khaaaa. Nafikiri upo umuhimu wa kuanzisha mafundisho kwa wanaume kabla ya kuoa ili wasije kuaibisha nyumba zao. Tena kuna hii nyingine utakuta kijana anakula chakula kinabaki baki pembeni ya midomo mweee yaani hata table mana nayo anatakiwa afunzwe na mkewe hapo itakua kazi kweli kweli.
 
yaani mtu mzima na akili zake atoke asubuhi shati limejikunja halafu umshangae mkewe badala ya kumshangaa mwanaume mwenzako?

Usmart ni hulka ya mtu

Kuna mijanaume mingine kuoga tu kwa mbinde sembuse kuvyaa shati lililonyooka

Halafu hao wake zenu wawafunge kamba ili msile magengeni?

Huyo mwanaume hajui wajibu wake kula nyumbani? Au ndo hao nyumbani hawaachi au wanaacha hela ya mchicha wao wanaenda kunywa supu au nyama choma bar

Ndoa zina mengi sana heri ushughulike na yako ya wenzio waachie wenyewe

hahahahaha waambie waambie hao uchafu wake mwenyewe amsingizia mtoto wa watu ndo baaaas tena!!!!
 
Wanapewa zawadi na malimbwata ya kuwawekea mabwana zao..hamna lolote la zaidi
Bado niponipo mwana
 
Hahahahaha LOL!!!! Anatafuna utadhani anafukuzwa 🙂🙂....Ni kweli wengine uchafu ni jadi yao, hivyo wanauendeleza mpaka ndani ya ndoa ikatokea kama mke ni msafi wa kupindukia basi ugomvi ni kila leo. Mbona shati lako linashangaashangaa hapa, mbona soksi zako umezitupa pale mbona viatu vyako vimezagaa hovyo hovyo.

Hahahahahahahaha unajua kuna wengine ni wachafu toka huko. Haingii akilini kijana anaejipenda akavaa shati limejikunja au socks zinazotoa harufu khaaaa. Nafikiri upo umuhimu wa kuanzisha mafundisho kwa wanaume kabla ya kuoa ili wasije kuaibisha nyumba zao. Tena kuna hii nyingine utakuta kijana anakula chakula kinabaki baki pembeni ya midomo mweee yaani hata table mana nayo anatakiwa afunzwe na mkewe hapo itakua kazi kweli kweli.
 
Hahahahaha LOL!!!! Anatafuna utadhani anafukuzwa 🙂🙂....Ni kweli wengine uchafu ni jadi yao, hivyo wanauendeleza mpaka ndani ya ndoa ikatokea kama mke ni msafi wa kupindukia basi ugomvi ni kila leo. Mbona shati lako linashangaashangaa hapa, mbona soksi zako umezitupa pale mbona viatu vyako vimezagaa hovyo hovyo.
Hahahahahahaha kimsingi wanandoa yapasa wasaidiane mmoja anapokua juu basi anyooshe mkono wake ili mwenzake aweze nae kuufikia. Na anaejiona yuko chini nae awe tayari kuupokea mkono wa mwenzake. Tunakutana 2 tusioperfect tunasaidiana kuufikia ukamilifu na mwisho ndoa inaonekana ni mahali pazuri na mti mkubwa wenye kivuli ili waliochoka wapate pumziko.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ablessed nimemuona pacha wako akichungulia huu uzi 🙂🙂
 
Last edited by a moderator:
Kparty za siku hizi hata hazinogi, zinanoga unapoona mazawadi mengi ambayo chache zina quality haswa. Nyingi ni zakuharibika zikitumiwa kwa majukumu yake kila siku.

Zamani ilikuwa hadi raha unasikia mengi na ushauri mzuri toka kwa wamama, wadada etc. Sasa siku hizi hata wanaume utaona wanaingia baadae khaaaaa zinaboa.

Kwa zawadi ok zinasaidia mabinti wengi ambao hata hawajui kutumia vyombo hivyo na wanaojua wanakuwa wamefika heaven. Wengi wanasubiri mama/dada zao kuja kufundisha housegirls na labda ndio maana unaona wanaume wanakunywa gengeni.

Ila hao wanaokunywa gengeni inamaanisha wengi wao hawana kazi au unasemaje? Maana kama mama na baba wote wanakazi basi ni shida kwa mama kumuhudumia mume chai na vitafunio afurahie asubuhi ukiangalia foleni na watu kuondoka hm giza kuwahi makazini hii kitu inachangia sana kwenye ndoa kuharibu utamu wa kila siku asubuhi na ndio maana na hg nae anakuwa anaingia kutengeneza chochote na wengi wanakuwa hawana muda wa kula ukikaa ukafikiria safari bora ule ukiwa upande wa pili karibu na kazini au kijiweni wanapopenda wanaume kusubiri dili.

Umesahau kibao kata duh hicho ndio ungeuliza kama kinasaidia nini pia?

Maisha ndio yanasababisha sidhani kuwa wanaume hawapendi wake zao hau wanapenda kula nje asubuhi kwa wengi wao.

Hao wanaotoka nje ni wajinga wiki moja tu? Mmmhh wanakuwa hawajui kulea wake zao na kuwazoea wakiibiwa ndio watajua na kujuta.
 
Nimeupenda sana huu mchango wako. Hivyo ndivyo inatakiwa iwe na mkiweza kufanikisha hili basi mtaishi raha mustarehe. Vitu vidogo vidogo kama kupelekewa ndoo ya maji ya kuoga ni vya kudharau tu.

Hahahahahahaha kimsingi wanandoa yapasa wasaidiane mmoja anapokua juu basi anyooshe mkono wake ili mwenzake aweze nae kuufikia. Na anaejiona yuko chini nae awe tayari kuupokea mkono wa mwenzake. Tunakutana 2 tusioperfect tunasaidiana kuufikia ukamilifu na mwisho ndoa inaonekana ni mahali pazuri na mti mkubwa wenye kivuli ili waliochoka wapate pumziko.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom