Kitambulisho cha taifa kuwa na expire date maanake nini?

Kitambulisho cha taifa kuwa na expire date maanake nini?

BRAND

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2013
Posts
296
Reaction score
260
Jana nilifanikiwa kupata kitambulisho cha taifa baada ya kuandikishwa hapa chuoni kwetu takribani miezi miwili iliyopita!

Kinaonyesha kuwa mwisho wake wa matumizi ni juni 2025,
Sijajua hasa mantiki ya kuweka muda wa mwisho wa matumizi yake!

Basi kuuliza si ujinga mwenye ufahamu na hili jambo naomba anifafanulie!
 
Ulichouliza kwenye title ya Tread yako majibu yake umejipa mwenye katika maelezo yako kwenye Thread.


Nashukuru.
 
Hii ni muhimu kwa sababu kuna kufa, inasaidia pia kujua idadi hasa ya watanzania ktk kupanga maendeleo yao
BRAND
 
Last edited by a moderator:
Hii ni muhimu kwa sababu kuna kufa, inasaidia pia kujua idadi hasa ya watanzania ktk kupanga maendeleo yao

Siyo kweli, ina maana ambao hawatakwenda kujiandikisha watakuwa wamekufa?
 
BRAND

Nilitaka nikujibu vibaya lakini baada ya kukuona sura kwenye face book na mitandao mingine ya kijamii nimegundua kwamba wewe ni kijana mdogo na unahitaji kufahamishwa.
Hebu iangalie picha yako kwenye hicho kitambulisho, Je ? miaka hamsini ijayo sura itakua hiyo hiyo ?
Jibu hilo kwanza ndio nikupe sababu tano za ku re new kitambulisho baada ya miaka kumi.
 
Last edited by a moderator:
Subiri itakuja pia, muda wa mwisho wa matumizi kwenye vyeti vya kuzaliwa na kufa. Mwisho wa muda wa matumizi yako ya cheti cha kuzaliwa ni... ukikosa kurenew... pigwa faini... au katafute nchi nyingine...
 
BRAND

Wala usihofu. Tanzania inataka kila mtu awe na vitambulisho vingi....ndio....unafikiri watu watapata wapi ten percent?

Kuna kitambulisho cha taifa, paspoti, kitambulisho cha mpiga kura, kitambulisho cha bank, kitambulisho cha mfuko wa jamii (nssf n.k), kitambulisho cha bima ya afya, leseni ya udereva, leseni ya mwandishi wa habari?, leseni ya mfamasia, leseni ya mhandisi, leseni ya daktari, kitambulisho cha makazi, kitambulisho cha kazi, ....unaweza kuongezea na vingine

Hivi vyote lazima ku-renew baada ya muda fulani.....isipokuwa cheti cha kuzaliwa ambacho kwa sasa wanaangalia kama kiwe re-newed baada ya muda gani. Wakipata mwafaka nacho kitaingia.....
 
Last edited by a moderator:
Nilitaka nikujibu vibaya lakini baada ya kukuona sura kwenye face book na mitandao mingine ya kijamii nimegundua kwamba wewe ni kijana mdogo na unahitaji kufahamishwa.
Hebu iangalie picha yako kwenye hicho kitambulisho, Je ? miaka hamsini ijayo sura itakua hiyo hiyo ?
Jibu hilo kwanza ndio nikupe sababu tano za ku re new kitambulisho baada ya miaka kumi.

Huwa si jibu watu wa aina yako!
 
BRAND

Ni muhimu sababu kina picha yako kina finger prints zako, wewe kama binaadamu utazeeka na sura uliyokuwa nayo sasa, hutokuwa nayo tena 2025 .
 
Last edited by a moderator:
Manake unatakiwa urenew baada ya muda! Ili wajue wangapi wamekufa
 
Kitambulisho kina picha inategemewa baada ya muda sura na muonekano vinabadilika pia ni suala la kupata taarifa zako mpya. Nadhani hizo mbili ni miongoni mwa sababu
 
Swali lako Ni la msingi Sana ila bahati mbaya wengi wamekimbilia kukujibu(hata Kama hawaelewi zaidi yako). Kwenye process ya kupata kitambulisho chako Kuna 'variable details' umesajilisha. Mfano sura, mfanyakazi/mwanafunzi, makaazi, marital status, nk. Kwa hiyo baada ya muda husika maisha yako yanabadilika kwa mambo mengi mfano;mwanafunzi>kuajiriwa, sura inabasilika, unaweza hamishia makaazi mahali tofauti Na eneo ulilopatia kitambulisho nk. Hivyo ku-renew kitambulisho maana yake kusajilisha current variable details zako. Usipokuwepo huo utaratibu sisi wenyewe siku moja likijatokea tazizo la serikali kutumia invalid details tutajaa humu kutukana kama vile hatuna malezi mema. Nawasiliaha.
 
Ila nimekumbana na kadhia ya kutokukubaliwa kwa hicho kitambulisho na baadhi ya taasisi za fedha tena za umma nchini.
 
Ama kweli hapa ni TZ, birth certificate inakuwa na expired date!
 
Ama kweli hapa ni TZ, birth certificate inakuwa na expired date!

Mkuu Na wewe kirahisi unaamini Na kutoa comment yako katika Hilo, Kama hauna uhakika Si uangalie ya kwako halafu uone akili zinazojaza page za jf.
 
Back
Top Bottom