Kitambulisho cha mpiga kura na maajabu yake

Kitambulisho cha mpiga kura na maajabu yake

jogi

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Posts
25,556
Reaction score
25,371
Ikiwa haitapingwa, inaonekana kuwa jina kuwepo kwenye orodha ya daftari la kudumu la wapigakura linalomilikiwa na tume ya uchaguzi tanzani ndio tiketi ya kupigia kura.

Tunakubaliana wote kuwa haikuwezekana kupewa kitambulisho kile bila tume kwa kusaidiwa na mawakala wa vyama kuthibitisha kisha kuchukua taarifa za mwandikishwaji kwa kuzijaza kwenye form yao maalum, kisha unaruhusiwa kwa utaratibu maalum kupiga picha, kuchukuliwa alama za vidole, kuweka saini kisha unapewa kitambulisho kuthibitisha kuwa taarifa zako za sifa ya kuwa mpiga kura zimesailiwa na tume.

Kwa kuwa hiki kitambulisho hakuna mwenye mamlaka ya kukitengeneza zaidi ya tume, ukizingatia kuwa vifaa vya kuchapia vitqmbulisho hivyo ni ghali sana na serikali imevinunua mahsusi kwa ajili ya tume tu, hatuoni kuwa Ingetosha ukishapewa utambulisho wa mpiga kura pasiwe na kikwazo isipokuwa ukikosa sifa za ukazi kwa shauri la kura ya diwani na mbunge.

Kama jina kwenye daftari ndio mambo yote kwenye kupiga kura ccm haikuwa na sababu nzuri za kuliingizia hasara kubwa namna hii taifa kununua vifaa ghali kabisa kumbe tungeweza kujiorodhesha kwenye makaunta book kwa kutumia bic

Ushahidi wa jina langu kuandikwa kwenye daftari ni kitambulisho chenye saini yangu, picha na alama za vidole walichonipa tume ya uchaguzi.

Sizuiwi kizembe kupiga kura.
 
Nadhani Kila Mwenye Kitambulisho Wadau Wa Uchaguzi Wakubaliane Ikitokea Jina la Muhusika Halipo Kwenye Kumbukumbu

Basi Busara Itumike na Kura Apige.
 
Kuna kitu ambacho sijuhi maana yake wala tafsiri yake.... Ni kwa nini tupange mafoleni mengine kwenda kuhakiki majina yetu...???
Kuna mchezo gani nyuma ya pazia...??
Sasa leo unahakiki majina eneo hili na wapo waliojiandikisha eneo hilo lakini wapo nje ya eneo husika.. Hapa inakuwaje..??
Na je; nahakiki majina leo kama halipo mnafanyaje na kama lipo mtanya nini...??
..
 
Mtwara madftari mengi yamekomea ofisi za kata na vijiji vinavyozunguka kata viko mbalimbali hivyo imepelekea wananchi wengi kutokwenda kuhakiki majina yao kwasababu ya umbali..na wananchi wanalalamika na kusema hawatendewi haki ..kama BVR walikuja kuandikishwa mpaka vijijini kwanini madaftari yakomee ngazi ya Kata??
 
Busara itumike kwa tume ili wananchi wahakiki majina yao .

Usiialike busara wakati unatakiwa kutumia akili ya kuzaliwa, umeniandikisha na ushahidi wa kuniandikisha umenipa kitambulisho, kama hukunakili jina langu kwenye daftari lako mimi sihusiki, haki yangu ya kikatiba ya kupiga kura lazima niitumie.
 
Kuna kitu ambacho sijuhi maana yake wala tafsiri yake.... Ni kwa nini tupange mafoleni mengine kwenda kuhakiki majina yetu...???
Kuna mchezo gani nyuma ya pazia...??
Sasa leo unahakiki majina eneo hili na wapo waliojiandikisha eneo hilo lakini wapo nje ya eneo husika.. Hapa inakuwaje..??
Na je; nahakiki majina leo kama halipo mnafanyaje na kama lipo mtanya nini...??
..

Nilidhani kama jina hakuna wanaliandika kumbe wanakutangazia kukunyima haki ya kupiga kura bila kosa lolote.

Ikiachwa hivi ilivyo italeta vurugu mithili ya vita.
 
Kundi linaloogopwa ni Kati 25 na 18 kama uko age hiyo kuhakiki taarifa zako ktk daftari la wapiga kura ni muhimu.
 
Naona nazeeka sasa!

Maana sijaelewa ulitaka kusema nini!
 
Naona nazeeka sasa!

Maana sijaelewa ulitaka kusema nini!

Uzee dawa mkuu, hongera kwa kuufikia.
Nilikusudia kuuliza "kama jina kwenye daftari ndiyo mambo yote kadi ya mpiga kura ni ya nini?
Maana tungeorodheshwa kwenye daftari tu kisha tunapiga kura.

Mtu unapewa kadi halafu hao hao waliokupa kadi hawakuandiki kwenye daftari na hao hao wanakwambia eti umekosa sifa za kupiga kura huoni hapo kizungumkuti!!?
 
Litakuwa kosa kubwa sana hili swala likiachwa na kupita bila kulipeleka mahakanmani, hata kama mahakama hizo ni za wale wale.
Mleta mada amelieleza vizuri na kwa lugha nyepesi na hii inaonyesha wazi wanaoongoza taasisi zetu walivyo na mawazo mgando.
 
Litakuwa kosa kubwa sana hili swala likiachwa na kupita bila kulipeleka mahakanmani, hata kama mahakama hizo ni za wale wale.
Mleta mada amelieleza vizuri na kwa lugha nyepesi na hii inaonyesha wazi wanaoongoza taasisi zetu walivyo na mawazo mgando.

Nafakiri wanasheria wa vyama vinavyounda ukawa walishughulikie hili jambo.
 
Back
Top Bottom