Kitakachotokea kesho bungeni


Hapana mkuu asubuhi hakukua na habari ya Mahakama, miongozo yote ililenga juu ya halihalisi ya pale Dodoma wbunge kupenyezewa makabrasha ya report na kuhusu mtu aliyeshikwa na polisi lakini ndio makinda alikataa wabunge kujadili hilo. Lakini kuhusu kujadili report ya kamati alisema ipo pale pale na aliagiza kurudufiwa kwa copy za ile report ili kesho iwezwe kusomwa nadhan ccm kweli walikuwa na jitihada za kila namna kuzuia lakini ukweli ni kwamba walichelewa kidogo kuzuia na siku zikawa zimefika sasa wamekuwa hawana jinsi mana ile mianya yooote waliyotaka kupita kuzuia ilikuwa inagundulika kabla bungeni wanaisema sasa wamekuwa hawana mpenyo. me nadhan kesho watatafuta namna kuifanya hiyo report isiwe na uhalali katika kujadili alradi kuwe na mazonge mazonge kuwe msitosito fulani ivi.
 

mkuu kwa mawazo uliyowasilisha hapa ni thahiri kabisa yote yanaweza kutokea.je ninataka kujua je kunauwezekano wa kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na kiti cha spika hiyo kesho?
 

Mkuu, hapo umenena sana. Kesho Sugu, Lema, Filikunjoombe, Nassari, Lissu, Machali, Kafulila na wengine wengi waliopo mjengoni....wawape kibano hao maccm na mafisadi wa escrow mpk wasome hiyo report.

Hapo wataheshimiana..
 
Bunge halina ujanja zaidi ya kutii mahakama kwa swala hili. Kuna sababu kuu moja naiona mimi ambayo inafanya hoja ya bunge kutokuwa na jinsi zaidi ya kuitii mahakama. Sababu kubwa ni tofauti ya strategies kati ya bunge na mahakama katika suala hili. Mahakama naona katika hili imetumia sheria wakati bunge linaonekana kutumia siasakatika kudai power yake. Ntafafanua, Bunge lilijua kuwa kuna uwezekano wa mahakama kuweka zuio lakini bunge halikujiandaa kwa hoja za kisheria katika jambo hili.

Tatizo la bunge letu ni kuwekeza sana kwenye kusema kwa ukali bila kujali sana matokeo. Ningetemea wanasheria wa bunge tangu walipopata tetes za zuio wange andaa legal team na hoja na mipango ya kuwaongoza kupita hapa walikokwama. Lakini wao walipambana na miongozo. Sasa mahakama ikatae kupokea malalamiko ya mtu? si ndio kazi yake? Ishu hapa si mahakama kulibana bunge ila ni mahakama kufanya kazi ilizoletewa na mlalamikaji.Sasa ina maana mahakama ilitakiwa ispokee kesi? IS IT REAL?? Can any law maker argue for this?

Nadhani haki inatafutwa mahakamani sio bungeni. Kama mahakama imepokea kesi tatizo liko wapi? Na KAMA MAHAKAMA HAINA UWEZO HUO KISHERIA SI WANASHERIA WA BUNGE WAENDE MAHAKAMANI WAONYESHE HIYO OVERSIGHT YA MAHAKAMA? Bora huko mahakamani maana maamuzi yake yanaweza kutekelezwa kuliko maneno makali ya wa bunge yanayo burudisha nafsi lakini matokeo ni kuunga mkono hoja.
 
Hivi tunataka kuona nini hiyo kesho au masaa machache yaliyobaki?
Wahusika tunaotarajia kuwasikia wengine majina yao yanajulikana na hawajachukia hatua zozote mpaka mda huu. Kwa mtuhumiwa ambaye dhamira yake iko hai, angeshafanya maamuzi siku nyingi. Hata yule mama Tibaijuka ambaye amejitaja mwenyewe asingetakiwa kusubiri mpaka mda huu.
Tutegemee lugha za kukashifiana na kutukanana humo alafu wawili au watatu wanakuwa kondoo wa sadaka na game inaisha. Msitarajie mambo makubwa yatakayokuwa na tija kwa taifa maana dhamira za hawa wenzetu zimesha kuwa SUGU
 
Mkuu, hapo umenena sana. Kesho Sugu, Lema, Filikunjoombe, Nassari, Lissu, Machali, Kafulila na wengine wengi waliopo mjengoni....wawape kibano hao maccm na mafisadi wa escrow mpk wasome hiyo report.

Hapo wataheshimiana..

uliona wapi ngedere anampinga nyani .
 
Mkuu, ulichoongea ni kweli ingawa inasikitisha.

Kamati ya Uongozi pamoja na wanasheria wa bunge watamshauri spika asitishe mjadala huo.

Najua bunge litalipuka lakini mwenye maamuzi ni spika hivyo ataliahirisha bunge huku kukiwa na zogo kubwa la spika kuzomewa.
 
Kabisa mkuu, watu wanapenda saana nafuu ya muda mfupi kupitia maneno matamu ya hasira za wabunge lakini si kila tatizo linamalizwa kwa mijadala tu. Ishu hii bunge lingejipanga kupambana kisheria haswa na huko ndo lingeenda kufumua ishu nzima. Lingekubali kwenda mahakamani na kuonyesha udhaifu wote wa kisheria katika ishu hii na hapo ndo bunge lingewashughulikia wezi na mawakala wao. Uzuri wa mahakamani adhabu inaendana na kushindwa ila ushindi wa mijadala ya bunge inampandisha mtu hadhi ya kisiasa lakini suluhisho ni dogo au hakuna.
 
Umeusemea Moyo wangu!
 
Katibu ajapokea amegoma..

Kikao cha kamati ya uongozi kimeitishwa asubuhi hii kama nilivyosema.

Kama spika anajiamini,hicho kikao ni cha nini kama sio kupitia hiyo hukumu na kisha waje na maamuzi tofauti?

Subiri tu yatimie niliyoyasema.
 
Kwa Kumuona Huyo Zungu Hapo ... Kwa hakika Ni Ishara rasmi Taifa linaingia kwenye Kiza Kizito ... huko aliko Makinda na Kama Ya Uongozi HAKITAKUA CHEMA MBELE YA MTANZANIA
 
Kikao cha kamati ya uongozi kimeitishwa asubuhi hii kama nilivyosema.

Kama spika anajiamini,hicho kikao ni cha nini kama sio kupitia hiyo hukumu na kisha waje na maamuzi tofauti?

Subiri tu yatimie niliyoyasema.

Huu ni mtizamo mmoja ... alternative. ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…