Kitabu: New World Order - Uchambuzi

Kitabu: New World Order - Uchambuzi

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2011
Posts
1,234
Reaction score
1,815
Jina la Kitabu.The New World Order
Mwandishi.Ralph Epperson
Mchambuzi.Nanyaro EJ


Utangulizi

Mwandishi anajitambulisha kama mtu aliyependa kusoma maandishi mbalimbali,na kila alipomaliza kusoma kiu ya kutaka kujua zaidi ikawa inaongezeka,hii ilimfanya asome na kusoma na kusoma na kusoma...hadi akaja kugundua siri ambayo ataielezea kwenye kitabu hiki
Anaanza kwa kunukuu vyanzo mbalimbali vya habari na watu mbalimbali wenye ushawishi Duniani


"Gavana wa New York ndugu Nelson A. Rockefeller amesema akiwa Rais atapambana kuunda serikali Moja duniani
' .... Januari 30, 1976,
Maseneta 32 na wawakilishi 92 wameamini hati ya kuwa uhuru wa mwingiliano wa Kitaifa,wakati wakisaini wamesema kuwa karne mbili zilizopita Babu zetu waliunda Taifa moja la Marekani,na sasa ni jukumu letu kuungana ili kuunda Taifa Moja la Dunia


Dikteta Adolf Hitler, alinukuliwa mara kadhaa kabla ya kusababisha vita vya pili vya Dunia na wakati wa Vita,akisema kuwa serikali yake ya kijamaa itatumia mapinduzi kuhakikisha kuwa Dunia inakuwa na New World Order
Hitler alikuwa anajigamba mara kadhaa kuwa Serikali yake inapaswa kuongoza zaidi ya Ujerumani na kuwa yeye kaka *Barbarian* huwa hawafi!na itakuwa jukumu lake kuweka new World Order na kwamba mtu ambaye anakitazama chama cha NAZI kama chama cha siasa pekee ni mtu kipofu tu ambaye bado haoni lolote!
Mwandishi anasema kuwa ulimwengu wa zamani unapita na unakuja ulimwengu mpya,dalili zote zimetimia,ikiwa ni pamoja na mfumo mpya wa maisha,huu ulimwengu mpya ndio *New World Order*


Dalili za Ulimwengu mpya ni pamoja na maswala ya jinsia moja kuonekana ni jambo la kawaida,na hitaji la kijamiii,malezi ya watoto yasiyokuwa na maadili.Talaka zitakuwa jambo la kawaida na zitarahisishwa.Dini mbalimbali zitawekewa ukiritimba kwenye maswala yao ya dini,serikali zitachukua sehemu kubwa ya ibada (zitaratibu ibada mbalimbali)


Mwandishi anasema waratibu wa jambo hili wanaliratibu kwa umakini mkubwa,na wanafanya hatua baada ya hatua

Inaendelea
nanyaro EJ
 
Jina la Kitabu.The New World Order
Mwandishi.Ralph Epperson
Mchambuzi.Nanyaro EJ


Utangulizi

Mwandishi anajitambulisha kama mtu aliyependa kusoma maandishi mbalimbali,na kila alipomaliza kusoma kiu ya kutaka kujua zaidi ikawa inaongezeka,hii ilimfanya asome na kusoma na kusoma na kusoma...hadi akaja kugundua siri ambayo ataielezea kwenye kitabu hiki
Anaanza kwa kunukuu vyanzo mbalimbali vya habari na watu mbalimbali wenye ushawishi Duniani


"Gavana wa New York ndugu Nelson A. Rockefeller amesema akiwa Rais atapambana kuunda serikali Moja duniani
' .... Januari 30, 1976,
Maseneta 32 na wawakilishi 92 wameamini hati ya kuwa uhuru wa mwingiliano wa Kitaifa,wakati wakisaini wamesema kuwa karne mbili zilizopita Babu zetu waliunda Taifa moja la Marekani,na sasa ni jukumu letu kuungana ili kuunda Taifa Moja la Dunia


Dikteta Adolf Hitler, alinukuliwa mara kadhaa kabla ya kusababisha vita vya pili vya Dunia na wakati wa Vita,akisema kuwa serikali yake ya kijamaa itatumia mapinduzi kuhakikisha kuwa Dunia inakuwa na New World Order
Hitler alikuwa anajigamba mara kadhaa kuwa Serikali yake inapaswa kuongoza zaidi ya Ujerumani na kuwa yeye kaka *Barbarian* huwa hawafi!na itakuwa jukumu lake kuweka new World Order na kwamba mtu ambaye anakitazama chama cha NAZI kama chama cha siasa pekee ni mtu kipofu tu ambaye bado haoni lolote!
Mwandishi anasema kuwa ulimwengu wa zamani unapita na unakuja ulimwengu mpya,dalili zote zimetimia,ikiwa ni pamoja na mfumo mpya wa maisha,huu ulimwengu mpya ndio *New World Order*


Dalili za Ulimwengu mpya ni pamoja na maswala ya jinsia moja kuonekana ni jambo la kawaida,na hitaji la kijamiii,malezi ya watoto yasiyokuwa na maadili.Talaka zitakuwa jambo la kawaida na zitarahisishwa.Dini mbalimbali zitawekewa ukiritimba kwenye maswala yao ya dini,serikali zitachukua sehemu kubwa ya ibada (zitaratibu ibada mbalimbali)


Mwandishi anasema waratibu wa jambo hili wanaliratibu kwa umakini mkubwa,na wanafanya hatua baada ya hatua

Inaendelea
nanyaro EJ
Sio wote wanayo macho kuona na kutambua hili, hata hii covid-19 ni moja ya mkakati kudhoofisha imani, lockdown ni mfano mzuri.
Yaani serikali zinalipangia kanisa/msikiti......

End times.......
 
Kitabu.New World Order
Mwandishi.Ralph Epperson
Mchambuzi.Nanyaro EJ

CHAPTER 1 TOMORROW'S RULERS

Mwandishi anasema kuwa swala la NWO halijaanza leo,ni mpango ulikuwepo kwa miaka kadhaa na taasisi nyingi kubwa zimekuwa zikikubaliana kwenye swala hili,Illuminant iliyoasisiwa na Adam Weishaupt mwalimu wa Canon Law mwaka 1176 huko Bavaria alinukuliwa akisisitiza kuwa ni lazima kuwa na utawala wa mmoja Duniani,Lazima kuwa na Serikali Moja Duniani(Hii ni mwaka 1776)
Baadae taasisi ya Freemason nao wanakubaliana na mawazo haya ya NOW,mmoja wa Freemason wakubwa na mwenye heshima kubwa Bwana Paul Fisher katika kitabu chake BEHIND THE LODGE DOOR,anasema kuwa Masonia watakuja kutawala Dunia na wataifanya Dunia iwe na Utawala mmoja yaani NWO

Albert Pike,katika kitabu chake MORALS AND DOGMA huyu ni mmoja wa waandishi nguli Duniani na ambaye maandishi yake yamekuwa sehemu ya kufungua Ulimwengu kuelewa hizi jamii za siri sana.Na vitabu vyake humika na freemason kuwapa wale wanaotaka kujiunga ili kupata uelewa mpana wa aina ya jamii ilivo…kwenye kitabu chake anasema kuwa Dunia na Walimwengu wataomba wenyewe kutawaliwa na mkuu wa Freemason….anaitwa Pontiffs nae atakubali kwa kuwa ni jamii iliyostaarabika na yenye mipango imara .
Anasema kiwango chochote cha upinzani kutoka kwenye jamii au taasisi yoyote ile ndio ishara na dalili kuwa wao masonia wanasogea mbele!kama wangekuwa hawasogei mbele hakuna ambaye angewapinga..hivo wanaamini wanakaribia kule wanakopaswa kuwa na kuiweka dunia kwenye mikono yao
Ili kufikia malengo haya imeundwa New Age Movement ambayo ni kama taasisi ya dini,yenye mafundisho yake,Imani yake na utaratibu wake wa ibada,ndio wale wanaoamini kuwa binadamu akifa,atatokea tena akiwa kitu kingine,mfano ulikuwa mwanaume mwafrika,ukifa unaweza kuzaliwa tena kama mwanamke mzungu,au mchina au hata ukazaliwa kama Simba,Nyati au kiumbe chochote..Katika kufanikisha haya wanasema kuwa haya sio mambo mapya ni mambo ambayo yamekuwepo kwa vizazi vingi,na kwamba binadamu alipoteza asili yake ya zamani,ndio maana anapata majanga mbalimbali,hivo wao wanakusudia kumrejesha binadamu kule anakostahili kuwepo kwa kutafuta ukweli wote wanajiita jina linguine (Truth seekers)
 
Kitabu.New World Order

Mwandishi.Ralph Epperson

Mchambuzi.Nanyaro EJ



CHAPTER 2 THE NEW AGE MOVEMENT


Mwandishi anasema New Age Movement ni vuguvugu linalofanya kazi kuelekea kwenye NWO, na wanachofanya kwa sasa ni kuanza kubadili fikra za watu,kuanzia kwenye utaratibu wa ibada za Kimungu,na kuleta utaratibu Mpya

Ili kufikia malengo yao wanatengeneza mipango mbalimbali yenye lengo la kufupisha uhai wa binadamu ili wakazi wa dunia wapungue na iwe rahisi kuwatala.Wamekuwa wakitengeneza program mbalimbali pamoja na madawa na majanga ya Dunia.Mipango kama vyakula ambavyo sio vya asili au dawa za kuzuia uzazi ambazo baadae husababisha saratani mbalimbali ni moja ya ajenda za hawa watu kwa lengo la kupunguza watu Duniani.Ugaidi wa kutengenezwa pia ni silaha yao kwa lengo la kutisha watu ili baadae iwe rahisi kulazimisha watu wawekewe chip(microchip) ambazo zitakuwa na taarifa zote,na hakutakuwepo na privacy tena,maana kila ufanyacho watakuwa na uwezo wa kukiona.Jambo lingine ni kuwa wameshikilia mifumo ya kuuza na kununua ambayo utalazimika kufuata masharti yao ili upate huduma!kwa sasa Dunia inaondoka kwa kasi kubwa katika mfumo wa kushika hela za makaratasi,malipo mengi yatakuwa yanafanywa online

Mwandish anasema kuwa hawa jamaa wana maneno mazuri sana,wanasema chini ya serikali moja hakuna binadamu ataruhusiwa kuwa na njaa,au kukosa mavazi,au malazi.Itakuwa ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kulala bila kula,au kukosa mavazi au makazi,hivo itakuwa jukumu la serikali kuhakikisha inatoa huduma hizo hata kama mtu hataki atalazimishwa kukubali.Itakuwa ni lazima kwa mtu yeyote chini ya serikali moja maisha mazuri whilst you were permitted to live, you would have to live well."

Kwa upande mwingine binadamu anayetakiwa kuishi vizuri ni yule tu ambaye amepata bahati ya kuruhusiwa kuishi.Ili aruhusiwe kuishi anapaswa kukubaliana na NWO na masharti yao ya kila aina ikiwepo kuwa Liberal.Kwenye sehemu ya kwanza tuliona kuna Illuminant na Freemason,hawa wote wanakubaliana kuwa na NWO,ila kundi moja lina msimamo mkali kuhusu maisha hili ni Illuminant"No man is fit for our Order who is not ... ready to go to every length ....huu ndio msimamo wao,kwa Illuminant kuua sio dhambi wala sio kosa,kwa yeyote ambaye hataki kufuata sheria zao,adhabu yake ni kifo,wakati kwa freemason wanaamini kidogo kuhusu Mungu na kuwa kutoa uhai ni dhambi na kosa kubwa

Mwandishi anasema katika kufikia malemgo yao chini ya taasisi zao za siri ambazo zipo nyingi tu,wanajipenyeza kwenye serikali mbalimbali Duniani.Wanahakikisha watu wao ndio wanakuwa katika vyombo vya kufanya maamuzi mbalimbali mwandishi anasema hiki ni mojawapo ya maswali ambayo unapaswa kukiri ili uwe mwanachama

"Are you prepared to give your life? Are you prepared to commit murder? Are you prepared to commit acts of sabotage which may cause the death of hundreds of innocent people? Are you prepared to betray your country to foreign powers? Are you prepared to cheat, to forge, to blackmail, to corrupt the minds of children, to distribute habit- forming drugs, to encourage prostitution, to dissem- inate venereal diseases — to do anything which is likely to cause demoralization and weaken the power of the [people?] Are you prepared to commit suicide, if and when we order you to do so?"
 
Kitabu.New World Order

Mwandishi.Ralph Epperson

Mchambuzi.Nanyaro EJ



Chapter 3 Lord Maitreya

Mwandishi anasema kuwa hawa NEW AGERS wana mungu/kiongozi wao ambaye atakuwa ndie kiongozi mkuu wa Dunia,wanamwita LORD MAITREYA,huyu bado hajaonekana hadharani ila inaaminika atashuka kutoka milima ya Himalaya katika mipaka ya India na Tibet.Wao wanaamini kuwa huyu ni yule ambaye dini nyingine zinamwita majina mengine kama Kristo kwa Wakristo,au Mesiya kwa Wayahudi,au Budha wa tano kwa Wabudha,Krishna kwa Wahindu,au Imam Mahdi kwa Waislam

Mwandishi anasema kuwa kwa mujibu wa New AGERS huyu alionekana 1977 huko London na ndie ambaye Dini nyingine zinamsubiri na hazijui yupo wapi.Kwao wanangojea muda mwafaka wamtoe.New Agers wanaamini kuwa Dini nyingine huwa zinakosea na kwamba wao ndio wako sahihi mitazamo ya dini nyingine inapaswa kuwa kama sehemu tu katika Imani yao.Wanasema kuwa huyu Master ni binadamu aliyechangia katika mabadiliko na mafanikio ya kiteknolojia ya leo kuanzia karne nyingi nyuma na huyu ndio kiongozi wao anayepaswa kuitawala dunia chini ya NOW

Mwandishi anasema kuwa kutokana na ubinafsi wa wafuasi wa NWO inaonekana kutatokea vita kati ya wafuasi wa Bwana Maitreya na wale wasiokubaliana nae.Bahati mbaya hawa NWO wamefanya na wanaendelea na maandalizi wakati watu wengine hawana habari,hii ni kwa kuwa maandilizi yake yanafanywa kwa siri kubwa kupitia jumuiya mbalimbali ambazo tumeshaona huko nyuma na tutaziona mbeleni
 
Kitabu.New World Order

Mwandishi.Ralph Epperson

Mchambuzi.Nanyaro EJ



Chapter 4 The Ancient Mysteries

Mwandishi anasema kuwa New Agers wana msemo kuwa "The One Who Knows The Secret Does Not Speak. The One Who Speaks Does Not Know The Secret." Mwandishi anasema kuwa kwa mujibu kitabu INTRODUCTION TO FREEMA- SONRY, imeandikwa kuwa wanafanya ibada za siri sana,kwenye baadhi ya maeneo nyumba/eneo la ibada hujulikana lakini uendeshaji wa ibada kwa ujumla huwa siri mno,baadhi ya wanaofika hawajui hizo taratibu hadi wafikie ngazi Fulani ya juu

Mwandishi anasema kuwa pamoja na New Agers kujiona ni watu wakweli na waadilifu(jambo ambalo sio kweli) bado wanafanya haya mambo kwa usiri kwa kisingizio kuwa ukweli wote unapaswa kujulikana kwa wale tu walio tayari kuujua na ambao wana kifua cha kuhimili ukweli huo,anatoa mfano kuwa hata kama unampenda mtoto wako ndogo kwa kiasi gani lakini huwezi kumlisha chakula cha watu wazima,kila hatua na chakula chake.mambo mengi yanafanywa kwa ishara na nyakati na alama maalum.Kila alama unayoiona duniani ina maana yake na itafunuliwa kwa wakati wake na mazingira yake

Anaendelea kuandika kuwa kuna kundi lenye maarifa lalkini halina siri na kundi lenye siri ili kufikia kuwa na siri zamani kidogo ilikuwa unawekwa kwenye jeneza kwa muda kisha unatolewa alafu unakula kiapo hapo unafikia ngazi ya Master Mason ambayo unaweza kupewa siri,siku hizi unaenda kusujudu kwenye madhabahu yao kwa utaratibu utakaokubaliwa,unalishwa viapo ambavo ukikiuka adhabu yake ni mauti
 
Kitabu.New World Order
Mwandishi .Ralph Epperson
Mchambuzi.Nanyaro EJ

Chapter 5 Secret Societies

Mwandishi anasema kuwa kuna mkono wenye nguvu kubwa isiyoonekana lakini ndio inaongoza Dunia na Walimwengu"An invisible hand is guiding the populace."
Kwamba nguvu hii ndio imekuwa ikiamua na kuratibu matukio mbalimbali katika historia ya Dunia(ukiona vinaelea vimeundwa).Hakuna tukio kubwa ambalo halijaratibiwa na hizi jamii za siri isipokuwa yale matukio ya asili tu kama vimbunga na Tsunami etc.
Rais Woodrow Wilson wa USA aliwahi kunukuliwa akisema kuwa "... there is a power so organized, so subtle, so complete, so pervasive, that they had better not speak above their breath when they speak in condemnation of it." Hizi jamii za siri zilimwingiza upepo Rais hadi akafikia kuwaonya watu wanaozinyoshea vidole,unaweza sasa kujua nguvu za ushawishi za hizi jamii za siri.Msingi wa siri au kutenda kwa siri ni kupunguza msuguano wa kijamii wakati huu.Wana falsafa yao kuwa
"The great strength of our Order lies in its conceal- ment; let it never appear in its own name, but always covered by another name, and another occupation."
Mwandishi anasema jambo lingine ni Imani yao kuwa binadamu wengi wamefungwa kwenye vifungo vya DINI ambazo sio za kweli(Wao wanapinga Dini zote) hivo wao watakuja kuwafungua binadamu kwa kutengeneza NWO.Wanachama wengi wa hizi jamii za siri wanaamini kuwa jamii yao ndio bora na matendo yao ni matakatifu…yaani wamekuwa brainwashed kujiona wao na malengo yao ndio ya masingi kuliko wengine,wapo tayari kufanya chochote kufikia malengo yao
 
Kitabu.New World Order
Mwandishi.Ralph Epperson
Mchambuzi.Nanyaro EJ


Chapter 6 Concealed Mysteries




Mwandishi anasema kuwa NWO na taasisi zake za siri wanaamini katika usiri wa hali ya juu,mmoja wa masonia alinukuliwa kwenye kitabu akisema kuwa Ukweli wa Mambo ya Dunia upo kwenye mfumo wa alama ili wachache wanaostahili ndio waelewe!.Pia anasema lazima uwe na uwezo wa kutambua nani umueleze ukweli,na nani asijue jambo fulani,kuna mambo ya kusema na watoto,mengine na wafanyabiashara,mengine na marafiki,hata kama ni jambo hilo hilo lakini uwasilishaji wake uwe kwa kadri ya kila kundi


Mwandishi anasema kwa asilimia kubwa sana mawasiliano ya hizi jamii za siri yanafanywa kwa lugha na code pamoja na alama ambazo ni wao tu wanazijua.Hii inafanya mwandishi ahitimishe kuwa lazima wana mambo mabaya ndio maana hawataki jamii itambue,wala hawataki yawe wazi.Inasemakana kuwa kuna siri ambayo iko ndani ya siri na ambayo iko ndani ya siri,kwa hiyo ni kitendawili kama cha Yai na Kuku...
*"Cut through the outer shell and find a meaning; cut through that meaning and find another; under it if you dig deep enough you may find a third, a fourth!*
 
Kitabu.New World Order
Mwandishi.Ralph Epperson
Mchambuzi Nanyaro EJ


Chapter 7 Serpents, Stars and Suns


Mwandishi anasema moja ya alama ambayo ni muhimu kutambua maana yake ni alama ya nyoka au dragoni.Nyoka alichukuliwa kama ishara/alama ya Hekima tangu binadamu wa kale,kwenye simulizi za mwanzo kabisa za binadamu wa kale Nyoka alimaanisha hekima na busara na matumizi yake ni ya kitambo sana
Sasa yule kiongozi/mungu wao ajae Lord Maitreya anatajwa kuwa kiongozi mwenye hekima na busara..tena anatajwa kuwa ndie chanzo cha hekima,wengine wanapata hekima kutoka kwake.Watu wa kale wanasema hivi kuhusu nyoka *for it tempts man to the knowledge of himself.*
Kwa kuwa nyoka alimjaribu binadamu wa kwanza katika bustani ya Edeni na akaweza kumshawishi avunje amri ya Mwenyenzi Mungu ndio kusema kuwa nyoka alikuwa na maarifa kuliko Adam na Eva!
*as the sun was the great enlightener of the physical world, so the serpent was held to have been the great enlightener of the spiritual, by giving man- kind the 'knowledge of good and evil.*
Jua ni ishara ya uhai..wanafalsafa wa zamani za Uyunani waliamini kuwa jua ndio chanzo cha maisha(hii ni mjadala usioisha na kuna makubaliano ya kisayansi kuhusu hili isipokuwa imani tu,kila mtu ana toleo lake,kimsingi linahitaji makala inayojitegemea)..sasa kwa hawa jamii za siri wanaamini kuwa jua ndio msingi na chanzo mhimu na Jua linatawala mchana hivo nao watakuwa watawala,Nyota kwa kuwa zinatawala usiku na ni nyingi ndio kusema kuwa wao ndio watawala wa mchana na usiku.
* "The sun is the ancient symbol of the life-giving and generative power of the Deity. The Sun was His manifestation and visible image." "The Sun is the hieroglyphical sign of Truth, be- cause it is the source of Light." *


Kwa hiyo wakati wengine wakitazama jua kwa mazoea,kwa masonia ni sehemu ya ibada na utawala wao,kwa hiyo sio ajabu kukuta alama ya jua kwenye majengo yao.Mwandishi anasema alama hizi zimetumika kama cover katika kueneza Umasonia,maana ni rahisi kufafanua maana zimetumika miaka na miaka,ila kuna zaidi nyuma ya pazia.
Mwandishi anasema ibada za masonia zinaanzia Mashariki na kuishia Magharibi,majengo yake ambayo huitwa Lodge...lazima yaelekezewe Mashariki kama vile Jua linaavyoanzia Mashariki hii humaanisha kuwa wanaanza kupata mwanga ambao ni chanzo cha nguvu ya ubongo na hekima.Kaskazini ni Upande wa laana kwao




the healing of the nations begins with the healing of ourselves. We must draw forth from the Great Cen- tral Sun — that eternal Light with which we were anointed from the beginning."
Mwandishi anasema kuwa fashisti Adolf Hitler, alikuwa mmoja wa viongozi wakuu aliyekuwa anaabudu Jua,Hitler alikuwa mwanajumuia wa jumuia ya siri iliyoitwa THULE SOCIERTY.Hitler na cha chake cha Nazi kilisababisha vita ya pili ya Dunia ambayo iliua zaidi ya watu 30mil,mauaji ya haya watu na tamaa ya Hitler ya kutawala Dunia ni ishara ya tamaa za masomo,bila shaka alikuwa mmoja wa masonia
 
Back
Top Bottom