Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,916
- 30,259
- Thread starter
- #261
Mazindu...Mkuu, nimecheka sana, imebidi niende kwenye uzi wake nione hiyo picha ya avator yake, kweli kaweka picha ya Coca Cola. Haa ha haha, halafu anashindwa kutuwekea hayo majarida yalionukuu HOJA zke huko kwenye vyuo "bora". Anyway, back to the topic; kujua kama Nyerere ndiye aliyewadidimiza Waislamu au la ni hivi, kwanini majarida yake huyu mzee anayapeleka kwenye vyuo vya nchi ambazo waislamu wengi wanadai ni za Kikristo badala ya kupeleka kwenye vyuo vya nchi za Kiislamu? Jibu lake ni rahisi tu, huko Uislamuni hawaheshimu elimu na ndicho walicho kiambukiza hadi huku kwa wamatumbi, na wenyewe hawapendi elimu halafu wanakuja kuilamu serikali kwa uzembe wao wenyewe. Gadafi pamoja na kutoa elimu bure kwa Walibya, je ni Walibywa wangapi walioamua kwa moyo mmoja kuwapeleka watoto wao shule? Juzi kati hapa nimeona kwenye taarifa ya habari ITV kwamba wanafunzi 17000 kule Lindi (Lindi ni miongoni mwa mikoa yenye waislamu wengi) wamegoma kuripoti shule/sekondari. Hapa na penyewe tuilamu serikali? Huwezi kuusambaza uislamu bila kueneza CHUKI, huwezi. Uislamu na chuki pamoja na fitina ni mapacha.
Kwa kuleta suala la picha za chupa za Coca Cola sidhani kama ndiyo tunachojadili hapa.
Wala sijashindwa kuweka ''reviews,'' za vitabu vyangu.
''Reviews'' zote ninazo wala si kazi kubwa kuziweka hapa.
Nilichomweleza Ndjabu ni kuwa wala asijiitabishe kuwa nimeandika kitabu kwa kuwa hili linamsumbua kwa miaka mingi hapa Barzani.
Nimemwambia kuwa na achukulie kuwa mimi sijaandika chochote na kama sijaandika chochote ''review'' itatoka wapi?
Kinachonichekesha mimi kama wewe unavyocheka kuona picha za Coca Cola ni mtu kushughulishwa na ''review'' ya kitabu asishughulishwe na kitabu chenyewe.
Mimi nikikusoma na hizi kejeli za ''huyu mzee'' basi nakuwa nimeshakufahamu na wala sipati tabu na wewe kwani wewe si wa kwanza wala hutakuwa wa mwisho kunikejeli hadi ukweli utakapokudhihirikia.
Wengi wanaponifahamu taratibu heshima hurejea.
Wewe hunijui na inawezekana ndiyo mara yako ya kwanza kunisoma au kunisikia.
Nimeandika vitabu saba na kipo kingine In Shaa Allah kitabu cha nane kinakuja.
Ninazo pia ''paper'' kadhaa wala sijui hesabu yake nilizoandika kuwasilisha katika vyuo mbalimbali hapa nyumbani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Lakini mimi furaha yangu huzidi pale unapotokea mtu kama wewe ukanikejeli.
Wala mimi sitakuuliza wewe umeandika nini kwani nakujua kutokana na unavyoandika na kujenga hoja hapa Barzani na kutiatia maneno ya Kiiingereza kuwa lipo tatizo.
Wewe kama nilivyomfahamisha mwenzio nakuomba jiaminishe kuwa mimi si lolote wala sijaandika chochote cha kutambulikana katika dunia ya usomi.
Hayo mengine wala sijaona haja ya kuyasemea.
Kitabu changu cha mwisho kimeingia Tanzania mwanzo wa mwaka huu hicho hapo chini pamoja na baadhi ya vingine.
Kitabu cha watoto nimekusudia kuwafunza Kiingereza na historia ya Zanzibar.
Sidhani kama bado unacheka.