Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,915
- 30,259
KITABU CHA KHAMIS ABDULLA AMEIR KIPO TAYARI
Rafiki yangu mmoja katika uongozi wa juu Zanzibar na aliyeshuhudia yote yaliyotokea kabla na baada ya mapinduzi alipata kuniambia kuwa ili kuielewa historia ya Zanzibar inataka mtu apinde mgongo kuisoma.
Akaendelea kusema na ubongo wako ufungue uwe wazi kujifunza bila kutanguliza mbele hisia zako.
"Historia ya Zanzibar ni tofauti sana na historia ya kwenu Tanganyika.
Hivi mnavyotuona sisi Wanzanzibari sote sie ni ndugu.
Sote sisi Waislam.
Mkiyajua haya na kuyakubali hamtopata shida na sisi."
Sijayasahau maneno haya.
Kila kitabu cha historia ya Zanzibar kilichoandikwa na Wanzanzibar wenyewe nje ya waandishi walioko au walikuwa ndani ya "Mapinduzi Daima," ukifungua tu ukurasa wa kwanza utahisi kama vile vidole vyako vimeshika bakuli la bati la uji wa moto uliotoka jikoni huku unatokota.
Msomaji wangu kwanza ningependa utambue kuwa hiki niandikacho si pitio la kitabu.
Hapana la hasha.
Si pitio la kitabu.
Sijakimaliza kukisoma kitabu.
Lakini ninachoweza kueleza ni kuwa hiki si kitabu cha kawaida kama alivyo mwandishi wa kitabu hiki kuwa si mtu wa kawaida pia.
Si ajabu pia kwahiyo kuwa historia ya maisha ya Khamis Abdulla Ameir yasingeweza kuwa ya kawaida.
Yeyote awae yule atakaekuwa na ujasiri wa kukipitia kitabu hiki na kukichambua kitamuacha taabani na si yeye mptiaji bali na wasomaji wake sawia.
"The Eagle Has Landed."
Hii ilikuwa Apollo 11 ilipotua mwezini mwaka wa 1969.
Hapa kwetu nyumbani ni tai katua juu ya mti.
Kitabu hiki ni tai aliyetua juu ya mti tena mti wenyewe mjengaua ulioko uani kwetu.