son of king john2
Senior Member
- Jan 11, 2014
- 131
- 33
KAPTULA LA MARX
Hiki ni moja ya vitabu vilivyowahi kuandikwa kwa ustadi mkubwa na Prf. E kezilahabi juu ya mfumo wa uendeshaji maisha katika taifa hili ambalo pamoja na mifumo yake mingi limekuwa likijinasibu kuwa ni la kijamaa kujitegemea ingawa ujamaa huu unaonekana kama "kaptula kubwa la marx" kwa taifa hili ambalo bajeti yake asilimia 30 inategemea miasada ya wahisani.
Naliona kaptura la marx ambalo Kezilahabi aliliandika juu ya mfumo wa ujamaa miaka mingi iliyopita. katika kitabu chake "kaptula la marx" kezilabi anaonyesha ni jinsi gani taifa liliuchukua ujamaa bila kujiandaa na hatimaye mavazi yale(mfumo wa ujamaa) yakawa makubwa na yasiyowatosha watawala kwani si wananchi wala watawala wa ngazi za chini waliokuwa wamejiandaa na mfumo huo bali mtawala mkuu wa enzi hizo na viongozi wachache.
mfumo huu haukuwa mbaya, ubaya ulikuwa ni maandalizi;watu walilazimishwa kuamini kuwa kila "TAJIRI" ni munyonyaji, kila mwenye wafanyakazi lazima awe anawanyonya wafanyakazi hao,hakuna anayestahili kuishi kwa raha bila kujali amepataje alicho nacho.mali yote ilitakiwa kumilikiwa na jamii kwa ujumla na uzalishaji ulitakiwa kuwa wa ushirikiano.
lengo kuu la mfumo wa ujamaa ilikuwa ni kuleta usawa katika umliki mali na matumizi yake,kwa manufaa ya umma.uma unufaike kwa pamoja.lakini katika pitapita yangu juu ya fasihi iliyoandikwa katika kuushadadia mfumo huu nimekuwa nikiona kutokujiandaa vizuri kwa wananchi aidha kwa kutokushirikishwa vyema au kwa kulazimishwa kabla ya kuelewa maana halisi ya ujamaa na ndiyo maana haukufanikiwa kama ilivyotarajiwa.
Miongo kadhaa baada ya azimio la arusha taifa tanzania linarudi katika mfumo ambao unaonekana kama wa kijamaa "sura na umbo la kijamaa" ingawa sina uhakika kama hata "roho" yake ni ya kijamaa.
umbo la kijamaa linajitokeza katika mambo mengi, moja wapo ni swala la elimu bure,kupunguzwa kwa PAYE kwa wafanyakazi wa kipato cha chini na serikali kujaribu kutoa bei elekezi kwa bidhaa muhimu kama sukari (ingawa hali ni mbaya kuliko jana).lakini pia umbo hili linajidhihirisha kupitia kauli mbalimbali za Mh. Rais wa Tanzania ambaye amekuwa akilaani baadhi ya watanzani (wachache hasa viongozi wa umma na wafanyabiashara ) kuishi kama "malaika" huku watanzania wengi wakiishi kama mashetani katika nchi yao yenye kila raslimali.
sura ya kijamaa pia imekuwepo katika baadhi ya mambo hasa yale ambayo yanahusu maamuzi ya mtu mmoja badala ya wengi, na ni dhahiri kuwa katika mfumo wa kijamaa lazima kuna hali ya kimaamuzi kuwa mikononi mwa wachache hasa watawala ambao hujinmasibu kuwa uhuru huo wamepewa na wananchi wenyewe.watawala hupinga kukosolewa,hupinga mawazo mbadala na hata kuzuia ueneaji taarifa kwa njia na mbinu mbalimbali ili kuendelea kuaminiwa ana wnanchi.
umbo na sura ya ujamaa wa Tanzania ya leo halijakamilika vizuri ingawa "roho" yake imekwisha jiweka wazi. Ntaeleza kuhusu roho hii kupitia sekta nyeti ya ELIMU ambayo imevikwa gunia lenye sura ya ujamaa huku ikiwa na roho ya ubepari kuntu na uliotukuka.