Sehemu ya nne
Enoko akauliza hawa ni akina nani?
Akajibiwa kwamba ni baadhi ya wale malaika waliotaka kupambana na Mungu, wamechukuliwa na kuning’inizwa hapo wakisubiri hukumu siku ya mwisho.
Hawa malaika wataonekana tena mbingu ya tano, na wengine watatu walishushwa duniani.
Swali ninalojiuliza ni moja.
Kwa nini Mungu aliamua wengine kuwaacha mbinguni wakiteseka na wengine kuwashusha duniani? Ngoja tuendelee kwanza.
Wengine walikuwa wakimwambia Enoko: “Mtu wa Mungu, tuombee kwa Mungu atusamehe!”
Enoko akawa anawajibu: “Mimi ni nani mpaka niwaombee? Ni binadamu, nisiyekuwa na lolote lile. Kama nikiwaombea ninyi, nani ataniombea mimi?”
Baada ya hapo malaika hao wakamchukua na kumpeleka mbingu ya tatu.
Huko akakutana na sehemu iliyotawaliwa na miti mingi mizuri iliyokuwa inamea matunda mazuri, ni kama bustani kubwa sana. Ilipendeza machoni mwake, ilikuwa ni sehemu ambayo ilimvutia kila alipokuwa akiiangalia.
Katikati ya bustani hiyo kulikuwa na mti mkubwa wa uhai, ni kama ule ambao uliwekwa kwenye bustani ya Eden ambapo kama Adam na Hawa wangekula hakika wasingekufa.
Mti huo ulikuwa na muonekano wa tofauti na miti yetu ya duniani. Ulikuwa kama umetengenezwa kwa mafuta yanayoteleza lakini pia ulionekana kuwa na muonekano wa dhahabu.
Mti huo ulikuwa na uwezo wa kuotesha kila aina ya tunda unalolijua wewe na usilolijua katika maisha yako. Pia katika bustani hiyo kulikuwa na mito, si ya maji, bali ilikuwa ni ya asali na maziwa.
Na pia kulikuwa na mingine ambayo ilikuwa inatiririsha mafuta na mvinyo (wine). Ukiachana na hiyo, pia kulikuwa na malaika mia tatu ambao walikuwa wanaitunza bustani hiyo kubwa huku wakiimba kila wakati.
Kwa namna walivyokuwa wakiimba, Enoko anasema hakuwahi kuona ama kusikia mtu duniani akiimba kama hivyo.
Hiyo ndiyo sehemu ambayo watakatifu watakwenda na kuishi. Yaani kama wewe unatenda mema duniani, utakwenda kuishi kwenye bustani hiyo milele na milele.
Baada ya hapo, malaika wale wakamchukua na kumpeleka upande wa Kaskazini mwa mbingu ile ya tatu. Sasa huko ndipo wale wasiokuwa watakatifu walipokuwa wanahifadhiwa, ndipo jehan
amu ilipo.
.