Kiswahili nacho....!

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
Wadau, ningependa mnifahamishe usahihi wa maneno ONYESHA n ONESHA...

Kwa mfano sentensi ipi ni sahihi kati ya hizi?

> CHADEMA YAONYESHA DEMOKRASIA

> CHADEMA YAONESHA DEMOKRASIA.


Aksanteni sana.
 
Sahihi ni sentensi ya pili. Chadema yaonesha demokrasia.
 
ila utata upo sana coz mpaka leo magazeti yetu yanaandika hayo makosa.
 
Wadau, ningependa mnifahamishe usahihi wa maneno ONYESHA n ONESHA...

Kwa mfano sentensi ipi ni sahihi kati ya hizi?

> CHADEMA YAONYESHA DEMOKRASIA

> CHADEMA YAONESHA DEMOKRASIA.


Aksanteni sana.

Yote yapo sahihi na yanatumika, ingawa kimantiki onesha ni sahihi zaidi (linatokana na mzizi -ona).

Lakini kinachosisitizwa ni kwamba, kama mwandishi ametumia 'onyesha' basi iwe hivyo hivyo bila kuchanganya-changanya na 'onesha'.
 
Yote yapo sahihi na yanatumika, ingawa kimantiki onesha ni sahihi zaidi (linatokana na mzizi -ona).

Lakini kinachosisitizwa ni kwamba, kama mwandishi ametumia 'onyesha' basi iwe hivyo hivyo bila kuchanganya-changanya na 'onesha'.

Yote ni sahihi na kutegemea orientation na audience, muandishi anaweza kuchanganya. Haya maneno yanatokana na lahaja tofauti za Kiswahili, ndiyo maana wengine husema hapo na wengine husema papo, na wengine huchanganya na kusema papo hapo (Kiswahili cha biblia kime influence sana hii style ya kuchanganya lahaja kwa sababu audience yake ilikuwa wanaoongea Kiswahili wote na lahaja zote kubwa).

Wengine watasema anaoga, wengine watasema anakoga, wengine watasema anaenda, wengine watasema anakwenda, yote maneno ya Kiswahili sawia, tofauti lahaja tu.
 
ONESHA ni sahihi zaidi, kwa sababu chanzo cha neno ONESHA ni ona na chanzo cha neno ONYESHA ni onya!
 
Hebu kwanza tuanze kunyumbua maneno ndipo tutaona neno gani ni sahihi.
Mzizi wa neno ONYESHA ni ONY-A ambapo ukiunganisha unapata kiini cha neno ambacho ni ONYA

Vivyo hivyo ONESHA ni ON-A =ONA

Turudi kwenye mfano wa sentensi hizo mbili
Sentensi sahihi ni CHADEMA YAONESHA DEMOKRASIA.
ina maana demokrasia inaonekana sio inaonyesha. ONYESHA inatokana na neno ONYA ambalo kwa tafsiri yake ni kama mtu ukikosea jambo fulani pale UNAONYWA.

Wataalamu wa Kiswahili hebu changieni mawazo yenu hapa.
 
Ni kweli kaka! inabidi watusaidie coz kila mtu anatoa jibu lake
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom