Kiswahili na maneno | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiswahili na maneno

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Che Kalizozele, Jan 6, 2009.

 1. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuna wakati uwa nahisi labda kiswahili kina upungufu wa maneno,ingawa kuna nyakati zingine uwa nagundua ni uchovu wangu tu katika kuifahamu lugha hii adhimu ndo unanisumbua ila kiswahili kuna uwezekano kikawa kimekamilika.
  Kwa sasa nina tatizo la kiswahili kutumia vitu katika kueleza aina za rangi.Hii inanipa shida kwa kuhisi inawezekana kiswahili hakina maneno ya kuelezea rangi hizi.Mfano rangi ya zambarau,rangi ya damu ya mzee,rangi ya kijivu.Kama kuna mtu anajua maneno yanayotambulisha rangi hizi,tafadhari naomba unielimishe.
   
 2. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Mkuu hiyo ni kawaida tu kwenye lugha kwani hata kiingereza kinafanya vivyohivyo, mfano chocolate color. Na siyo kwenye rangi tu, kama ambavyo maisha ya viumbe hai yanategemeana (equal system) ndivyo hivyo na lugha, angalia hapa; kwenye ujio wa teknolojia ya habari na mawasiliano wataalamu waliamua kutumia neno web site-neno web- walililinganisha na nyumba ya buibui. Kwa hiyo usione tabu Shekh wangu, ndo lugha zinavyoishi na kukua.
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280

  Hii list inaweza kukusaidia? English (Swahili):

  White (Nyeupe)
  Grey (Kijivujivu, Majivu)
  Black (Nyeusi)
  Yellow (Manjano)
  Gold (Dhahabu)
  Orange (Rangi ya machungwa)
  Deep orange (Rangi ya balungi)
  Red (Nyekundu)
  Pink (Pinki)
  Purple/violet (Samawi (samawati?), Zambarau)
  Red violet (Zambarau mbivu)
  Blue (Bluu, Buluu)
  Light blue (Buluu nyepesi)
  Navy blue (Bluu nzito)
  Green (Kijani, Majani)
  Light green (Kijani nyepesi)
  Emerald green (Kijani kibichi)
  Sea green/blue (Kijani/bluu bahari)
  Yellow green (Jani la mgomba)
  Brown (Kahawia, Hadharani)
  Cream (Mtindi)
  Silver (Fedha)
   
 4. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Asanteni sana wakuu,kwa kunitoa tongotongo,mana kama ningeenda na kuanza kubishana mbele za watu ndo nilikuwa naumbuka mtu mzima.Mbarikiwe sana
   
 5. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2009
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mkuu, siku zote uhitaji kubishana kwa kitu ambacho huna uhakika nacho. Pia sidhani kama ubishani ni sehemu ya kujua vitu. Uliza tu jibu linapatikana kirahisi sana. Ikishindikana nenda google. Tena hapo mnaweza kujadili na si kubishana
   
 6. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #6
  Jan 6, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nafikiri ni ushauri mzuri,nitajaribu kuufuata.Binafsi uwa nina tatizo moja,uwa sikubali kirahisi hasa kama yale unayoyasema hayana mashiko,ingawa si kila kinachoonekana kukosa mashiko ni cha uongo.Na kutokujua haimaanishi ndo ukubali kila kitu.
   
 7. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Tafadhali rekebisha hayo maneno niliyoyatia rangi ya hudhurungi, yamenitatiza kidogo katika kuyasoma.
  uwa linamaana ya kuoa uhai, huwa linamaana ya jambo litokealo mara kwa mara.
  ndo ni chombo maalum cha kuchote/kubebea/kuhifadhia Maji. ndio inamaana ya kukubali/kuitikia jambo sahihi.
   
 8. M

  Mahmoud Qaasim JF-Expert Member

  #8
  Jan 6, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Mwanjelwa tujitahidini kukienzi kiswahili kwa kukitumia kwa usahihi wake.
  neno UHITAJI linamaana ya kuwa katika hali ya kuhitajia jambo. matakwa mahitajio.

  wewe ulitakiwa kutumia neno HUHITAJI ukimaanisha hali ya kukanusha mahitajio/matakwa. huhitaji = hutakiwi/hutaki yaani huna hitajio.
  kuacha herufi H katika kanushi hupoteza maana ya kanushi na pengine maana ya neno lenyewe kubadilika.
   
Loading...