Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia?

Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia?

sayoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
5,281
Reaction score
7,953
Baada ya kusahau nywila(password) ya kadi yangu ya kiotomotela(ATM) nikaamua kukaa mgahawani (restaurant) jirani na kilipo kiotomotela na kuagiza vibanzi (chips) vikavu na sharubati (juice) baridi sana! Nikiwa nasubiri kuletewa nikafungua tarakilishi mpakato (laptop) na kujaribu kufungua diski mweku (local disk) iliyogoma kufunguka kwa wakati huo. Nikafungua diski tepetevu (floppy disk) na kukuta imevamiwa na mtaliga(virus). Nguvu ikaniishia, nikashindwa hata kushika wala kupalaza kisharazio(cursor) cha tarakilishi yangu. Siku yangu ikaishia hapo na nikaishia kusahau hata vibanzi na sharubati nilivyoagiza.

Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia??
A. Ndio
B. Hapana
 
B..hapana bora english tu aisee. ... Tutauana kama ndio hivyo
 
Kiswahili kitumike kwingine siyo kwenye mambo ya technology weeee
 
Kwani lazima tutumie hayo maneno tunayoyaona magumu kwa sababu ya kuyazoea hayo ya kiingereza?
 
Baada ya kusahau nywila(password) ya kadi yangu ya kiotomotela(ATM) nikaamua kukaa mgahawani (restaurant) jirani na kilipo kiotomotela na kuagiza vibanzi (chips) vikavu na sharubati (juice) baridi sana! Nikiwa nasubiri kuletewa nikafungua tarakilishi mpakato (laptop) na kujaribu kufungua diski mweku (local disk) iliyogoma kufunguka kwa wakati huo. Nikafungua diski tepetevu (floppy disk) na kukuta imevamiwa na mtaliga(virus). Nguvu ikaniishia, nikashindwa hata kushika wala kupalaza kisharazio(cursor) cha tarakilishi yangu. Siku yangu ikaishia hapo na nikaishia kusahau hata vibanzi na sharubati nilivyoagiza.

Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia??
A. Ndio
B. Hapana
B
Lakin si kwa hoja dhaifu km hiyo.
 
Swali lako ni pana sana.Kujibu A au B ni kuifanya iwe hafifu sana.
 
Kiswahili lugha nzuri sana kutongozea mwanamke ila kwenye kufundishia tusameheani jamani.
 
Back
Top Bottom