kiswahili kigumu

kiswahili kigumu

Son of Alaska

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2008
Posts
2,812
Reaction score
1,070
jamani kiswahili kigumu sana,mimi sielewi,hivyo JUMAMOSI na JUMAPILI ni weekend au mwanzo wa week
 
jamani kiswahili kigumu sana,mimi sielewi,hivyo JUMAMOSI na JUMAPILI ni weekend au mwanzo wa week

we ulifikiria chepesi?kigumu ndio kwa kuwa inategemeana na mtumiajia wa maneno hayo.

Pili maneno yote ya kiswahili ni ya kibantu labda tuwaulize waanzalishi wa maneno hayo Je,ni biblia au nini?

Nawasilisha.
 
Aisee hata mimi nashindwa kuelewa maana hata humu jamvini lugha inayotumika sana ni KISWANGLISH, yaani mtu kutoa hoja bila ya kuweka neno kiingereza sijui ndio usomi au inakuwaje?
 
Lakini neno week end siyo la kiswahili wakulu, ni la Kiinglish... Na lina maana hiyo hiyo, kwa hiyo hata kiinglish nacho kigumu pia!
 
Ijumaa ni wikendi kwa waarabu, Jumamosi wikendi kwa wayahudi na Jumapili ni wikendi kwa wakristo na nchi za magharibi. Juma linaanza Jumatatu kwa utaratibu kwa nchi za magharibi. Kumbe juma linakwisha Jumapili (wikendi)

Sisi waswahili tumezipa siku majina kwa kufuata utaratibu wa Kiarabu ambao juma huisha Ijumaa. Kumbe Jumamosi ni siku ya kwanza ya juma. Ndiyo maana inaitwa na waswahili Juma-mosi, yaani siku ya kwanza ya juma.

Kumbe kwa majina ya siku tumefuata utaratibu wa Kiarabu, lakini kwa kupanga juma tumefuata utaratibu wa Kimagharibi ambapo juma huanza Jumatatu na kuisha Jumapili.
 
Back
Top Bottom