Kiswahili cha Magufuli kinahitaji msasa

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
22,323
Reaction score
56,062
Kuna watu wamekuwa wakijadili umahiri wa Lugha ya Malkia kwa MTUKUFU MHESHIMIWA RAIS DOKTA Magufuli.
Lakini kiukweli tatizo halipo katika Lugha ya malkia bali Lugha kwa ujumla
Ukimsikiliza kiswahili chake sio standard anatafuna maneno na mengine hawezi kuyatamka ana misamihati michache sana ya kiswahili
wataalamu wa linguistic pale BAKITA na TUKI fanyeni kazi yenu
Mungu amegawa vipaji tofauti,kujua lugha ni kipaji ila hata wasio na kipaji wakipigwa msasa wanakuwa na angalau.
 
mi napita tu ........
 
Tumechagua Rais atakaesukuma gurudumu la maendeleo yetu,hatukuchagua msoma taarifa ya habari,kama unataka matamshi nenda BBC,hapa kazi tu
 
Akiongea Kiingereza kuna malalamiko, Kiswahili kinaleta shida Mr Mdukuzi unataka rais aongee Kisukuma?
 
Ni misamiati bro, sio MISAMIHATI
 
Lakini c unamuelewa?!au shida yako kubwa nini?!mbona mzungu akiongea kiswahili vibaya hamcheki hata km amezaliwa tanzania!
 
Nchi inahitaji Rais jasiri, mtendaji na mfuatiliaji wa shughuli za kuwaletea maendeleo wananchi sio mwalimu wa kiswahili wala kiingereza, kwani umahiri wa kiswahili na uswahili wa JK umeisaidia nini nchi kama sio kuitosa kwenye majanga, wizi mtupu wakati mswahili akiendekeza vijembe, mipasho na kejeli!?
 
Tatizo mkuu anaongea kapanik kwa kila kitu, hii inasababisha kutoyatendea hak matamshi
 
Akiongea Kiingereza kuna malalamiko, Kiswahili kinaleta shida Mr Mdukuzi unataka rais aongee Kisukuma?
Lugha ya taifa ndio lugha pekee ya kujidai nadhani ameathiriwa na mother tongue
 
Kwa position aliyonayo haihitaji kubobea kwenye lugha, ni kiasi kidogo tu cha ufahamu wa lugha kinahitajika kwa ajili ya kutolea maelekezo ya kufanya kazi ili zifanyike. Like "lifanyike zoezi la kuhakiki vyeti vya taaluma kwa watumishi wa umma" simpo!
 
"...ukiemba dukani dai risti..."
 
Mtu ana miaka karibu 60 sasa unataka afundishwe matamshi yatakayo kuridhisha wewe ya kiswahili? Hiyo ndio priority ya wananchi wa Tz kwa sasa. Wazo lako ni mfu.
 
Kwa mtanzania ambaye kiswahili either ni first language au second language aliyezaliwa kukulia na kusomea tanzania mpaka chuo kikuu kushindwa kutamka baadhi ya maneno ya kawaida
 
Lugha ya taifa ndio lugha pekee ya kujidai nadhani ameathiriwa na mother tongue
Sikiliza yaliyomo kwenye ujumbe usisikilize utamu wa lugha, kuna wenye lugha muafaka na pumba wanazotoa unaona aibu wewe msikilizaji. mdukuzi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…