Mwandishi wa habari za Kiuchunguzi, Erick Kabendera amepandishwa tena kizimbani asubuhi ya leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar
Kabendera aliyefika Mahakamani hapo akiwa bado anatembea kwa kuchechemea amesema kuwa jana alipelekwa hospitali kupimwa afya
Amesema, "Jana nilipelekwa hospitali ya Amana na kufanyiwa vipimo vya x-ray na majibu ya awali yameonesha nina matatizo ya mgongo."
Aidha, ameongeza kuwa amefanyiwa vipimo vingine vinavyoweza kuwa tayari ifikapo mwisho wa wiki hii huku akibaisha kuwa bado anapata maumivu makali ya mgongo
Hata hivyo, kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi imeahirishwa hadi Oktoba 01, 2019 baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa upelelezi haujakamilika lakini upo katika hatua nzuri
Kabendera alifikishwa katika mahakama hiyo kwa mara ya kwanza, Agosti 5, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kuongoza genge la uhalifu, kukwepa kodi na kutakatisha fedha zaidi ya Sh173.2 milioni.