KISUTU: Mwandishi Kabendera asema kufanyiwa vipimo na kukutwa na matatizo ya mgongo. Kesi yaahirishwa mpaka Oktoba 01

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
746
3,058
Erick Kabendera mwandishi wa Kujitegemea wa Habari za uchunguzi anapandishwa kizimbani mda huu, huku bado afya yake ikionekana Kutetereka.

------
Kabendera aliyefika Mahakamani hapo akiwa bado anatembea kwa kuchechemea amesema kuwa jana alipelekwa hospitali kupimwa afya hospitali ya amana ikiwa ni kufanyiwa vipimo vya x-ray na majibu ya awali yameonesha ana matatizo ya mgongo."

Aidha, ameongeza kuwa amefanyiwa vipimo vingine vinavyoweza kuwa tayari ifikapo mwisho wa wiki hii huku akibaisha kuwa bado anapata maumivu makali ya mgongo

Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 01, 2019 baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa upelelezi haujakamilika lakini upo katika hatua nzuri.

 
Mwandishi wa habari za Kiuchunguzi, Erick Kabendera amepandishwa tena kizimbani asubuhi ya leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar

Kabendera aliyefika Mahakamani hapo akiwa bado anatembea kwa kuchechemea amesema kuwa jana alipelekwa hospitali kupimwa afya

Amesema, "Jana nilipelekwa hospitali ya Amana na kufanyiwa vipimo vya x-ray na majibu ya awali yameonesha nina matatizo ya mgongo."

Aidha, ameongeza kuwa amefanyiwa vipimo vingine vinavyoweza kuwa tayari ifikapo mwisho wa wiki hii huku akibaisha kuwa bado anapata maumivu makali ya mgongo

Hata hivyo, kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi imeahirishwa hadi Oktoba 01, 2019 baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa upelelezi haujakamilika lakini upo katika hatua nzuri

Kabendera alifikishwa katika mahakama hiyo kwa mara ya kwanza, Agosti 5, 2019 akikabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kuongoza genge la uhalifu, kukwepa kodi na kutakatisha fedha zaidi ya Sh173.2 milioni.
 
Jela ni jumba la marekebisho kwa wenzetu huko mbele (with exception of Quantanamo bay, and some few others out there), ila huku kwetu mara nyingi wamelenga kukomoa sio kuirekebisha jamii. Kuwa jela hakumuondelei mtu haki zake za msingi za kibinadamu, na sio uchochoro wa kupiga na kutesa tu watakavyo watawala.

Leo tunawapa wao kesi, kesho watatupa sisi kesi. Maisha ni mzunguko, kama ilivyo: utukufu wa mwisho utakuwa utukufu mkubwa zaidi, vivyo hivyo anguko la mwisho litakuwa anguko kubwa zaidi.
 
Serikali inataka afe tu ndowatafurahi.
Kamamtu anaumwa si aruhusiwe akapatiwe matibabu stahiki, then akipona aendelee na mashtaka?
 
‘...Ukiisaliti Rwanda hutakuwa salama na ninakujulisha hupaswi kuwa Salama . ... kwangu binafsi na kwa Wananchi wenzangu wa Rwanda .. dhambi ya kuisaliti Rwanda ni kubwa kuliko ya kuhujumu Msaliti wa Nchi.....’

Paul Kagame
 
Back
Top Bottom