Kisutu: Mahakama yawahukumu miaka mitatu au faini wafanyakazi wa Quality Group

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,717
55,819
Mahakama ya Kisutu yawahukumu wafanyakazi 16 wa kampuni ya Quality Group miaka mitatu ama kulipa faini ya Shilingi milioni 22.

C5VthtPWcAA3mhF.jpg

Wafanyakazi wa Kampuni ya Quality Group Ltd walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kughushi viza za biashara, kuishi na kufanya kazi nchini bila vibali

Akiwasomea mashtaka mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha, Mwendesha Mashtaka wa Idara ya Uhamiaji, Method Kagoma alidai washtakiwa kwa pamoja Februari 13, katika Kampuni ya Quality Group Ltd iliyopo wilayani Ilala, wakiwa raia wa India walikamatwa wakiwa na viza za biashara zilizoghushiwa, wakiishi na kufanya kazi nchini kinyume na sheria.

----------
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu wafanyakazi16 wa Kampuni ya Quality Group, kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya jumla ya sh. Milioni 22.

Washtakiwa hao wametiwa hatiani baada ya wiki iliyopita kukiri mashtaka yao mahakamani hapo.Katika Hukumu hiyo, washtakiwa kila mmoja amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu katika kila kosa au kulipa faini ya sh. Milioni 1.5 kila mmoja katika kila kosa katika makosa matatu.

Washtakiwa hao walikuwa wanatuhumiwa kwa mashtaka matano likiwemo la kufanya kazi nchini kinyume na sheria na kuzuia maofisa Uhamiaji kutimiza majukumu yao.

Washitakiwa wote wametiwa hatiani leo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha.Hata hivyo, washitakiwa hao waliachiwa huru baada ya kulipa faini hiyo na kukwepa kifungo hicho.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Jose Kiran (40), Prakash Bhatt (35) ambao kwa pamoja walikuwa wakikabiliwa na mashitaka ya kuzuia maofisa wa Uhamiaji kufanya kazi yao.

Wengine ni Rajat Sarkar (35), Jagadish Mamidu (29), Niladri Maiti (41) Divakar Raja (37) ambao ni washauri wa kampuni hiyo, huku Mohammad Shaikh (44) mhasibu na Pintu Kumar (28) ambaye ni Meneja msaidizi wa kampuni.

Wengine ni, Bijenda Kumar (43), Prasson Mallik (46), Nipun Bhatt (32), Anuj Agarwal (46), Varun Boloor, Arun Kateel (46), Avinash Chandratiwari (33) na Vikram Sankhala (50) wote walikuwa wanakabiliwa na mashitaka matatu ya kukutwa na visa za kughusho na kufanya kazi nchini kinyume cha sheria

Hakimu Mkeha amesema, washitakiwa 14 kila mmoja atatakiwa kulipa faini ya Sh milioni 1.5 kwa makosa matatu huku washitakiwa wawili wote kwa pamoja faini ya Sh milioni moja kwa kosa moja.

Imedaiwa kuwa, Februari 20, mwaka huu washitakiwa Jose Kiran, na Prakash Bhatt waliwazuia maofisa uhamiaji kutimiza majukumu yao baada ya kukataa kuripoti kwa Ofisa Uhamiajiwa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa kujaribu kukimbia nje ya nchi kupitia mpaka wa Horohoro.

Ilidaiwa kuwa kwa washitakiwa 14 wanadaiwa kutenda kosa hilo Februari 13 mwaka huu maeneo ya Kampuni ya Quality Group wilayani Ilala mkoa wa Dar es Salaam.

Imedaiwa kuwa washitakiwa wote wakiwa ni raia wa nchini India, walikutwa na visa zilizoghushiwa kinyume na kifungu namba 31 (1) (e) na kifungu namba 2 cha sheria ya uhamiaji ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho na sheria namba 8 ya mwaka 2015.

Iliendelea kudaiwa kuwaalidai katika mashitaka ya pili kuwa washtakiwa hao walikutwa wakiishi nchini kinyume na sheria.Aidha katika shtaka la tatu, washtakiwa hao walikutwa wakifanya kazi nchini kinyume cha sheria.

Karama Kenyunko
 
Wafanyakazi 16 wa kampuni ya Quality Group wamehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela ama kulipa faini ya sh.milioni 22 katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu baada ya kutiwa hatiani katika kesi ya kuzuia maofisa wa uhamiaji kutimiza majukumu yao.

Chanzo: ITV
 
Tanzania ingeanzisha Sheria ndogo ndogo za kuwataka wageni kuwa wanaishi katika registered accomodation na sio magodown au sehemu zao za kazi.
Pili foreign companies ziwe pia zinakuwa na offices katika registered offices na sio kwenye makazi ya watu, hii itasaidia kuwa baini wageni haramu ambao hujificha ktk makazi ambayo hutumika kama offices na pia magodown ya uzalishaji ambayo pia hutumika kama makazi , na mtindo huu hutumika saaana na watu wa bara la asia hususana wachina, India, Pakistani, Bangladesh, Waturuki, Waarabu, nk
 
Tanzania ingeanzisha Sheria ndogo ndogo za kuwataka wageni kuwa wanaishi katika registered accomodation na sio magodown au sehemu zao za kazi.
Pili foreign companies ziwe pia zinakuwa na offices katika registered offices na sio kwenye makazi ya watu, hii itasaidia kuwa baini wageni haramu ambao hujificha ktk makazi ambayo hutumika kama offices na pia magodown ya uzalishaji ambayo pia hutumika kama makazi , na mtindo huu hutumika saaana na watu wa bara la asia hususana wachina, India, Pakistani, Bangladesh, Waturuki, Waarabu, nk
 
Hilo kosa la kugushi viza tu walitakiwa saa hizi wawe Mumbai,lakini tutaambiwa wamelipa viza na wamepewa vibali
Huwezi kugushi kibali India ukaachwa tu.
 
Uhamiaji kama wako kweli serious na hawa watu waishio na kufanya kazi kinyume na sheria za nchi basi waanze na wachina. Hawa watu ni balaa,wengi wao wanafanya kazi na biashara kwa vibari vya CTA wengi wapo ki magumashi.
 
Back
Top Bottom