KISUTU: Kesi namba 457(Jamhuri v JamiiForums), Hakimu apata dharura. Yapigwa kalenda mpaka Juni 01, 2018

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Kesi namba 457 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) inayohusu kampuni za CUSNA Investment na Ocean Link kudaiwa kukwepa kodi Bandarini Dar na kunyanyasa wafanyakazi wa kitanzania imeendelea leo Mei 28, 2018 katika Mahakama ya Mkazi, Kisutu.

Hata hivyo kesi hii inayosikilizwa mbele ya Hakimu Godfrey Mwambapa imeahirishwa leo mpaka Juni 01 na Hakimu Mkazi Martha Mpanze baada ya Hakimu Mwambapa kupata dharura.

Mara ya Mwisho shauri hili liliposikilizwa na Hakimu Mwambapa mnamo Mei 22, 2018 alisema leo Mei 28, 2018 angetoa uamuzi wa kujua kama Washitakiwa wana Kesi ya kujibu ama la.

Katika Shauri la leo upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Mwendesha Mashitaka wa Umma, Nassoro Katunga huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Benedict Alex.

Mwendesha Mashitaka wa upande wa Jamhuri, Nassoro Katunga alimueleza Hakimu Mpanze kesi ilipoishia mara ya mwisho kuwa unasubiriwa uamuzi wa Hakimu kujua kama Washtakiwa wana kesi ya kujibu au hawana.

Hivyo, Hakimu Mpanze ameahirisha shauri mpaka Juni 01, 2018 ambapo uamuzi utatolewa.

Kujua ilipotokea kesi hii soma; KISUTU: Hatma ya kesi namba 457(Jamhuri v JamiiForums) kutolewa Mei 28, 2018
 
Sasa mkiifunga jamii forums tutapumzikia wapi kama bunge live hamtaki sisi wavijijini tunaitegemea jf kupata habari zilizo bora zaidi
 
Back
Top Bottom