‪Kesi namba 458 dhidi ya JamiiForums: Jamhuri yaomba Hati ya kukamatwa Shahidi, Mahakama yaridhia!‬

Roving Journalist

JF-Expert Member
Apr 18, 2017
532
1,000
E4B810D2-B79E-45E8-B0E3-11FA039D5232.png

6108394C-16B1-428C-9352-D931263F617A.jpeg


Kesi namba 458 ya mwaka 2016 (Jamhuri dhidi ya Mkurugenzi wa Jamii Forums na Mwanahisa wa Jamii Media) imetajwa tena leo 25 Juni 2020 mbele ya Hakimu Huruma Shaidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar.

Hata hivyo, kesi hiyo ambayo washtakiwa anashtakiwa kwa kuendesha mtandao usiosajiliwa Tanzania na kutotoa taarifa za Mteja anayedaiwa kuandika taarifa kuhusu Benki ya CRDB katika Mtandao wa JamiiForums, imeahirishwa hadi 30 Julai 2020.

Katika kesi hii inaendelea kwa Upande wa Jamhuri kuleta mashahidi wao, kwa mara ya Mwisho shahidi kusilikizwa Mahakamani hapo ilikuwa Novemba 12, 2018.

Hivyo hakimu ameridhia kutoa hati ya kukamatwa kwa Shahidi Tully Ester Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano kwa Umma CRDB.

Katika shtaka la pili la Shauri hili, Polisi ilimtaka Mshtakiwa ambaye ni Mkurugenzi wa Jamii Forums kutoa taarifa kuhusu Wanachama wawili wa Mtandao wa JamiiForums.com waliodaiwa kuandika kuhusu madai ya uhalifu uliokuwa ukiendelea katika Benki ya CRDB.

Taarifa zilizotakiwa ni za Wanachama walioanzisha mijadala inayosomeka "Charles Kimei (CRDB) jiuzulu, kashfa ya kontena, tiketi TFF, wanafunzi na ujambazi CRDB" mjadala unaodaiwa kuanzishwa tarehe 18 Januari 2016 pamoja na "Wizi wa Benki ya CRDB - Part II" unaodaiwa kuanzishwa Machi 11, 2015.

Taarifa za Wanachama ambazo zilitakiwa kutolewa ni IP-Address, barua pepe, Majina Halisi ya Wanachama hao. Pia ilitakiwa zitolewe post zote zinazohusu Uhalifu unaofanyika katika benki ya CRDB kitu ambacho Polisi wanasema Mkurugenzi huyo aligoma kuwapa.

Katika shauri hili leo, Wakili wa Jamhuri alikuwa Anna Chimpaye huku Mawakili wa Utetezi wakiwa Benedict Ishabakaki pamoja na Maria Mushi.

Kujua kesi hii ilipotokea tembelea >
Kesi namba 458 (Jamhuri v Maxence Melo): Ni ile kesi ya JamiiForums kudaiwa kutotumia Kikoa cha do-tz, imepigwa tena kalenda hadi Juni 25, 2020
 

Trillion

JF-Expert Member
Apr 24, 2018
838
1,000
Nchi ina muhitaji LISSU hii.
MaCCM kuweni wa kweli hata form kutoka moja tu imewashangaza sana..!

#LISSURAIS2020
 

mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
22,347
2,000
kuhusu majina kamili ya hao member.
Kwani humu jamii forum tunajiunga kwa majina yetu halisi?
 

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
1,268
2,000
Siri ilipofichuriwa na wale member wa jf, wahusika waliweweseka hadi leo bado wanajifariji kwa kushindana na the great thinkers lkn ukweli umeshajulikana hawawezi lolote.
 

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
4,794
2,000
Kwa upande wangu kesi kama hii naipenda sana. Pamoja na kwamba Mshitakiwa ni Jamiiforums, lakini nahisi ikiendelea, CRDB wenyewe watajiweka wazi walichokuwa wanafanya ktk mambo yao ya kibenki. Taarifa yenyewe sioni kama Serikali iliathirika na thrd, nahisi CRDB waliona kama wanaharibiwa na labda wakachochea kesi ili kunyamazisha watu. Tukumbuke ilikuwa ni ile enzi ya umaarufu mitaani.

Tusubiri kesi iendelee.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom