Kesi namba 458 ya Jamhuri vs JamiiForums yazidi kupigwa Kalenda

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,789
11,931
Kesi namba 458 ya Jamhuri dhidi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo na mwenzake Mike William inayohusu kuendesha mtandao (JamiiForums.com) bila kutumia Kikoa cha do.TZ iliendelea 27/02/2020 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Katika Kesi hiyo ambapo Watuhumiwa hao wanashtakiwa pia kwa kuzuia upelelezi wa Polisi kwa kutokutoa taarifa za Mteja aliyeandika taarifa kuhusu Benki ya CRDB ikihusishwa na makato katika miamala zaidi ya inavyotakiwa imeendelea mbele ya Hakimu Huruma Shaidi.

Upande wa Jamhuri umewakilishwa na Wakili Simon Wankyo huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Omary Msemo.

Wakili wa Jamhuri amesema bado hawajapata shahidi wa kuendelea naye katika shauri hili.

Kwa mara ya Mwisho kesi hii kuwa na shahidi mahakamani ilikuwa mwaka 2018. Na kesi imekuwa ikiahirishwa kwa sababu mbalimbali. Tarehe ya mwisho shahidi kusikilizwa ilikuwa ni Novemba 12, 2018 ambapo Mpelelezi Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Mtandaoni kutoka Makao Makuu ya Polisi (HQ), Inspekta Beatrice Majule ndiye alikuwa shahidi.

Kesi iliahirishwa hadi 23 Machi 2020.

Kujua kinachoendelea, soma: Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums
 
Back
Top Bottom