‪KISUTU, DAR: Mahakama yawapa dhamana Viongozi 6 wa CHADEMA bila kuwepo mahakamani. Kutoka gerezani Aprili 3, 2018...

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,810
11,980
Leo Mwenyekiti wa Chadema Mhe Freeman Mbowe pamoja na viongozi waandamizi wa Chadema wanatarajia kufikishwa Mahakama ya Kisutu Kwa ajili kusikiliza shauri la dhamana leo

======
UPDATES:
======

04:00pm > Hakimu Mashauri baada ya kusikiliza hoja zilizowasilishwa na upande wa Jamhuri na utetezi amesema Aprili 3, 2018 washtakiwa waletwe mahakamani wasaini bondi wakishakuwa huru ndiyo zoezi zima la taarifa ya kukata rufaa kama Jamhuri ilivyoonyesha nia litafanyika.

03:20pm > Upande wa Jamhuri (mashtaka) wamesema hawajaridhishwa na uamuzi wa kutoa dhamana na watakata rufaa. Hii ni kwa mujibu wa wakili wa Jamhuri, Faraja Nchimbi. Wanasema kuwa usalama wa umma unaweza kuwa shakani kwa washtakiwa kuwa huru mtaani.

Hakimu amekubaliana na Wakili Kibatala kuwa mawakili wa Jamhuri hawakuwa na hoja za msingi wa kisheria kupinga dhamana kwa washtakiwa.

03:00pm > Hatimaye Hakimu ametoa dhamana kwa washtakiwa! Kila mshtakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini bondi ya Sh. Milioni 20 na wawe na barua toka kwa viongozi wao wa vijiji ama S/Mtaa na wawe na nakala za vitambulisho vyao.

Watatakiwa kuripoti Polisi kila Alhamisi (Central Police)

02:25pm > Wakili wa Jamhuri anamuomba mkuu wa Logistics za kuleta wafungwa Kisutu, aliyemtaja kwa jina moja la Shaban aeleze sababu za watuhumiwa kutofika mahakamani. Shaban anasema asubuhi aliwasiliana na mkuu wa gereza la Segerea ambaye alisema gari limeharibika.

2:08pm > Hakimu na Mawakili wa pande zote wanaelekea kwenye Ukumbi wa Mahakama. Ukumbi umeshajaa watu tayari. Ni wazi kuna uamuzi flani utatolewa hapa...

2:00pm > Hakimu amewaita mawakili. Waendesha mashitaka hawapo, aijulikani wameenda kula au vipi...

1:50pm > Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa amerejea mahakamani akiwa na Ndg. Mgeja. Amefika na kunong’onezana kitu na Wakili Kibatala

FF87A7C3-C832-43FC-B0F7-D9FF055A641A.jpeg

ECDEF45A-013B-4E51-B884-CBFE8E3A6539.jpeg


1:20pm > Vurugu nje ya mahakama ya Kisutu now, mtu mmoja amezongwa na kulazimishwa kuondoka kwenye makusanyiko wa wanachama wa CHADEMA.

"Huyooooo huyoooo, ondoka hapa, wewe kibaraka, hatukutaki, ondoka," kelele zimesikika wakimtimua mtu huyo.

Inadaiwa na wanachama hao wa CHADEMA kuwa mtu huyo ni "kibaraka" wa CCM na wengine wakimtuhumu kuwa mwanausalama.

Mtu huyo kaondoka kwa kukimbia akielekea katikati ya jiji.

12:26pm > Wakili Kihwelo ameiambia JamiiForums kuwa Hakimu Mashauri ameamua kusoma uamuzi mdogo, wawepo watuhumiwa ama wasiwepo, kuhusu dhamana ya Mbowe na wenzake. Hatua hii inakuja baada ya Mawakili wa Mbowe na wenzake kwenda kwa Hakimu Mkuu Mkazi, Wilbard Mashauri.

12:01pm > Hadi muda ni kuwa watuhumiwa wote wakiongozwa na Mh. Freeman Mbowe ambao wapo gerezani Segerea waliokuwa waletwe Kisutu, hawajatokea. Inadaiwa gari hakuna na lililopo ni bovu!

11:50am > Askari wenye silaha za kivita wameanza kuitana, wanajikusanya. Hatujui walikuwa wanapanga nini. Baadae wamesambaa; baadhi wameelekea getini huku wengine wakijipanga tena kuzunguka viunga vya mahakama.

11:45am > Mawakili wa Jamhuri - Patrick Mwita, Mutalemwa Kishenyi na Mawakili wa washitakiwa Peter Kibatala na Hekima Mwasipu wameingia ofisini kwa Hakimu Mkuu Mkazi, Wilbard Mashauri.

11:34am > Baadhi ya Viongozi wa juu wa CHADEMA waliokuwa wamefika mahakamani wameondoka mahakamani Kisutu. Wanaenda kushiriki msiba wa marehemu Kimesela ambaye anazikwa makaburi ya Kinondoni jijini Dar.

11:30am > Wananchi na makada wa CHADEMA wameanza kukosa uvumilivu baada ya kuzuiliwa nje ya lango kuu la mahakama na Polisi. Wameanza kuimba nyimbo za kudai haki, Wakili Kibatala amewasihi waondoke lakini dalili hazionyeshi kama wataondoka eneo hili.

11:20am > Mpaka muda huu, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watano, hawajafikishwa katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar. Tetesi zinadai kuna mikakati ya kuhakikisha wanakula Pasaka wakiwa gerezani. Kisingizio kinachodaiwa kutumika ni kuwa “Magereza hawana gari la kuwaleta mahakamani”

======
Katika Picha:

> Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa afika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi inayowakabili viongozi wakuu wa chama hicho, akiwamo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.

IMG-20180329-WA0002.jpg

==========
> Waandishi wa habari na wananchi wengi wamefika mahakamani ambapo ulinzi leo umeimarishwa sana. Kulikuwa na kesi ya Ugaidi hivyo inapelekea watu kuzuiliwa.

> Jeshi la Polisi limeimarisha zaidi ulinzi katika Mahakama ya Kisutu, baadhi ya wafuasi wa CHADEMA na wananchi wamezuiwa kuingia, wamekusanyika nje ya mahakama.

7C50B06D-BE68-4D8B-98D4-B91C604A6ED3.jpeg


> Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye pia amewasili mahakamani hapa kushuhudia kitakachotokea.

4557AF29-DC59-4724-BE18-545388188778.jpeg


> Baadhi ya wanachama wa CHADEMA, viongozi na wananchi wakiwa ndani ya chumba cha mahakama kusubiri shauri la Mbowe na wenzake

18EEF9BF-C964-4CCB-B3E6-5FA02945ECEC.jpeg


Habari zaidi, som=>Mbowe na viongozi 6 wa CHADEMA wafikishwa Mahakamani Kisutu, wasomewa mashitaka 8, wanyimwa dhamana hadi Machi 29
 
Jeshi la kipolisi.wanazuia wanachama na viongozi wetu kuingia mahakamani Kisutu kusikiliza kesi ya viongozi wao!!!! Makaburu weupe Afrika kusini waliruhusu wananchi weusi kusikiliza kesi maarufu ya Rivonia trial ya kina Nelson Mandela, hata kuvaa nguo ya Chadema ni kosa!!!
 
index.jpg


Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na viongozi wenzake watano wa chama hicho wamerejeshwa tena mahakamani leo Machi 29, kuendelea na kesi inayowakabili.

Updates kukujia kupitia uzi huu.....
 
Kama ni kufunga mtu, Magufuli alipaswa kuwafunga wale waliokuwa wanatuibia madini kupitia makinikia na sio kutesa watanzania wengine kwa makosa ya kipuuzipuuzi. I hope akimaliza muda wake, Rais ajaye nae aanze kufukua "makaburi" ya kivuko feki, meli ya samaki na mikataba ya bombardier
 
Back
Top Bottom