Kissa cha nabii Nuhu kwenye Qur-an tukufu

Kissa cha nabii Nuhu kwenye Qur-an tukufu

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,450
Reaction score
32,292
SURAT NUH IMETEREMKA MAKKA INA AYA 28 NI SURA YA 71 JUZUU TABARAKA.

Baada Ya Audhu Billahi Minashaitwan Rajim Biamillahi Rahman Rahim.

Hakika sisi tulimtuma Nuhu kwa watu wake, ya kwamba aonye watu wako kabla ya kuwajia adhabu iumizayo.

Akasema: Enyi watu wangu ! Kwa hakika mimi ni mwonyaji niliye dhahiri kwenu.

Ya kuwa mwabuduni Mwemyezi Mungu na mcheni na mnitii.

Atakusameheni madhambi yenu na Atakuahirisheni (bila ya balaa) mpaka muda uliowekwa. Hakika ijapo ajali itokayo kwa Mwenyezi Mungu haizuiliki. Laiti mngejua !

Akasema: Ee mola wangu hakika nimewalingania watu wangu usiku na mchana.

Lakini mwito wangu haikuwazidishia ila kukimbia;

Na kila ulipo waita uwasamehe, waliziba masikio yao kwa vidole vyao, na walijifunika nguo zao (gubigubi), na walizidi kuendelea na (kufuru) na wakafanya kiburi kingi.

Tena niliwaita kwa jahari.

Kisha nikawatangazia kwa kelele, tena nikasema nao kwa siri.

Nikawaambia: Ombeni msamaha kwa Mola wenu. Hakika yeye ni Mwingi wa msamaha.

Atakuleteeni mawingu yanyeshayo mvua nyingi.

Na Atakupeni mali na watoto, Na atakupeni mabustani, na atakufanyieni mito.

Mumekuwaje hamuweki heshima ya Mwenyezi Mungu.

Na hali Yeye amekuumbeni namna baada ya namna ?

Je hamuoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyoziumba mbingu saba (tabaka moja juu ya moja).

Na Akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru na akalifanya jua kuwa taa ?

Na Mwenyezi Mungu amekuotesheni katika ardhi, (kama) mimea.

Kisha atakurudisheni humo na Atakutoeni tena.

Na Mwenyezi Mungu amekufanyieni ardhi kuwa (kitu kizuri) mlicho tandikiwa.

Ili mtembee katika njia zilizo pana.

(Nabii) Nuhu akasema: "Mola wangu ! Hakika hao wameniasi na wamewafuata ambao mali yao na watoto wao haukuwazidishia ila hasara"

Na wakafanya hila kubwa kubwa za (kubatilisha Dini).

Na waliwaambia (wafuasi wao): "Msiache miungu yenu, wala msiwaache Waddi wala Suwa'a wa Yaghutha wala Ya'uka wala Nasra." (Majina ya waungu wao wa kisanamu).

Nao wamekwishapoteza (watu) wengi; wala usiwazidishie madhalimu hawa ila kupotelea mbali !

Basi kwa ajili ya makosa yao waliagharakishwa wakaingizwa motoni, wala hawakupata wa kuwanusuru mbele ya Mwenyezi Mungu.

Na Nuhu (akizidi) kusema: Mola wangu ! Usimuache juu ya ardhi mkazi wake yeyote katika makafiri.

Hakika ukiwaacha watapoteza watu Wako (waliotengenea) wala hawatazaa ila (watoto) waovu wenye kufuru (kama wao).

Mola wangu ! Nighufurie mimi na wazee wangu , na kila aliyeingia nyumbani mwangu hali ya kuwa Muislamu, na Waislamu wamaume na Waislamu wanawake; wala usiwazidishie madhalimu ila maangamizo.

Swadaka llhahu llhadhimu.

Maelezo.

Kinatajwa kisa cha Nabii Nuhu kwa urefu na kazi ngumu kabisa aliyo ifanya kwa muda wa miaka 950 mfululizo

Basi tusichoke katika kufundisha mema hata hatuoni upesi na tija yake. itakuja tu na sisi wenyewe tuendelee kuutenda huo wema kwani hili ni jukumu la kila Muislamu na tukatazane maovu yasije yakatukuta kama kaumu zilizotutangulia kama kaumu Nuhu.
FB_IMG_1521001971496.jpg
 
nilisoma sehemu kuwa kuna utata ni nafsi ngapi ziliokoka gharika. je ni nafsi ngapi kwa mujibu wa Quran?
 
Back
Top Bottom