Ninampango wa kuanzisha kilimo cha umwagiliaji kwenye eneo la ekari kumi kuanzia 2013. Sehemu nitakayochimba kisima haina umeme nategemea kutumia solar kuvuta maji chini ya ardhi. Mazao ya mbogamboga na matunda ya muda mfupi ndio nategemea kuzalisha. Kama kuna mtu ana uzoefu wa kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia visima virefu naomba atupe ufanisi na vikwazo katika hiki kilimo.