Kisima kingine cha gesi chavumbuliwa Tanzania

Kisima kingine cha gesi chavumbuliwa Tanzania

Vyamavingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2014
Posts
6,044
Reaction score
5,920
Kampuni ya Statoil ya Norway kwa ushirika na Exxon Mobil ya Marekani, imetangaza kugundulika kwa gesi asilia ktk enei jipya la Giligiliani-1 ktk ukanda wa Bahari ya Hindi. Kisima hicho kina futi za ujazo wa 1.2tr ktk Kitalu namba 2.

Gas discovery is no longer an excitment in Tanzania, maana hiyo habari haikupewa kipaumbele kwenye vyombo vya habari.

Au yawezekana Watanzania hatutegemei makubwa kwa utajiri huo.

=====================================

Kiasi kingine kikubwa cha gesi chagunduliwa nchini


gas.gif

Ugunduzi huo mpya katika Kisima Piri-1 umefanyika katika eneo lenye kiwango kidogo cha mawe ya mchanga kama ilivyokuwa wakati ilipogunduliwa gesi katika Kisima cha Zafarani-1 mwaka 2012

Dar es Salaam. Kampuni ya Statoil ya Norway na mshirika wake ExxonMobil wamegundua kiasi kingine kikubwa cha gesi katika Bahari ya Hindi nchini Tanzania.

Kiwango hicho kinakadiriwa kufikia futi za ujazo trilioni mbili mpaka tatu (sawa na lita trilioni 56.6 hadi trilioni 84.9).

Ugunduzi huu unafanya jumla ya ujazo wa gesi iliyogunduliwa na washirika hao kufikia takriban futi za ujazo trilioni 20 (lita trilioni 566.25) kwenye Kitalu Namba 2, ambako washirika hao wanafanya shughuli za utafiti na uchimbaji.

''Tangu mwaka 2012 tumekuwa tukipata mafanikio ya asilimia 100 nchini Tanzania na eneo hilo limekuwa kitovu cha utafiti ndani ya muda mfupi. Ni kwa haraka tulitoka kwenye kuchimba kisima kimoja hadi kuwa na mkakati wa kuchimba visima vingi,'' alisema Makamu wa Rais wa Shughuli za Utafiti za Statoil Ukanda wa Magharibi, Nick Maden.

Ugunduzi huo mpya katika Kisima Piri-1 umefanyika katika eneo lenye kiwango kidogo cha mawe ya mchanga kama ilivyokuwa wakati ilipogunduliwa gesi katika Kisima cha Zafarani-1 mwaka 2012.

Ugunduzi katika kisima hicho unakuwa wa sita katika Kitalu Namba 2.

Uchimbaji wa gesi katika kisima hicho ulifanywa na meli ya Discoverer Americas, usawa wa mita 2,360 za kina cha maji. Meli hiyo sasa inachimba kisima kingine cha Binzari katika Kitalu namba 2.

"Eneo lingine la utafiti limeshaandaliwa na litajaribiwa ndani ya mwaka 2014 na 2015. Tunatarajia kuchimba visima zaidi na tunatumaini kuwa matokeo ya visima hivi yataongeza kiasi cha ujazo wa gesi kwa ajili ya miundombinu ya mradi mkubwa wa gesi hapo baadaye,'' alisema Maden.

Statoil ambayo imekuwapo nchini tangu 2007, inatafiti na kuchimba gesi katika kitalu namba mbili kwa niaba ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ikiwa na hisa ya asilimia 65 katika kitalu hicho wakati ExxonMobil Exploration and Production Tanzania Limited ina asilimia 35.

Chanzo:Mwananchi,Oktoba 16,2014.

 
kwenye gasi na mafuta yanakuwepo, sasa hayo mafuta yanakwenda wapi au yanaliwa na wanaojiita wajanja
 
hadi sasaivi zimevumbuliwa kiasi gani kwa ujumla? yaani leo tarehe 16 october 2014
 
Baba wa Taifa Mwal JKN Nchi uliyoipigania inatafunwa na wazungu kwa kivuli cha wawekezaji.
 
shida hapo ni uwaz wa mikataba juu ya ugunduzi huo wa gesi asilia ,mtanzania wa kawaida atafaidika vip .,itakuwa kama migodi ya dhahabu ,almasi ,tanzanite na madin mengine ambapo tunashuhudia hadi udongo unapakiwa kwenye ndege unapelekwa ulaya na america na gesi itakuwa hivyohivyo itakuwa inaenda nje watanzania tunabakia na jina tuu kwamba tunazalisha gesi
 
Mi nasikia wanachimba tu ila mpaka leo sijawah sikia hela Iliyokana na gesi imepelekwa wapi kwa utajili tulionao sidhan hata kama tunahitaj misaada ya nje na kuwa na madeni kiasi icho. Sio siri nchi inaliwa inatafunwa tukiwa tunaangalia yani kuna vitu vinakera mpaka havifikiliki sababu inauma
 
Nimeshinda bila umeme leo, na vyanzo ndio hivyoooo..kwni hawawezi kuanzisha power plants tuuziane wabongo tu?
 
Utajiri wa maliasili je itawanufaisha wananchi maskini waliokata tamaa ? There is unfair in the provision of national cake.
 
Nashukuru kwamba gesi hii inagunduliwa baharini ambako hawaishi watu,maana kila eneo ambalo utajiri mkubwa unagundulika watu wa eneo hilo wanakuwa maskini kupindukia,angalia mererani,mwadui,buzwagi n.k
labda kama gesi ni tofauti na madini mengine.
 
Inasemekana 1.2 tcf hizo gesi iliyoko kwenye kisima hicho cha Giligiliani 1 ni linganifu na thamani ya mapipa ya mafuta 216,000,000.
 
Mi nasikia wanachimba tu ila mpaka leo sijawah sikia hela Iliyokana na gesi imepelekwa wapi kwa utajili tulionao sidhan hata kama tunahitaj misaada ya nje na kuwa na madeni kiasi icho. Sio siri nchi inaliwa inatafunwa tukiwa tunaangalia yani kuna vitu vinakera mpaka havifikiliki sababu inauma
Mkuu ni sawa na wewe ukiwa na n'gombe lkn huna zana za kumchinja inabidi utafute mtu mwenye zana
akusaidie kuchinja unamwachia nyama yote wewe unachukua kwato,ngozi na kichwa
angalau watoto wafaidi supu.
 
kwenye gasi na mafuta yanakuwepo, sasa hayo mafuta yanakwenda wapi au yanaliwa na wanaojiita wajanja
Sio lazima kwenye gesi kuwepo mafuta, ila ni lazima kwenye mafuta kuwepo gesi, ila uwepo wa gesi ni dalili mojawapo ya uwezekano wa kuwepo mafuta
 
Mi nasikia wanachimba tu ila mpaka leo sijawah sikia hela Iliyokana na gesi imepelekwa wapi kwa utajili tulionao sidhan hata kama tunahitaj misaada ya nje na kuwa na madeni kiasi icho. Sio siri nchi inaliwa inatafunwa tukiwa tunaangalia yani kuna vitu vinakera mpaka havifikiliki sababu inauma
Mpaka sasa gesi inachimbwa sehemu moja tu, yaani mnazibay wanapochimba panafrican energy(songas), na ni kiasi kidogo sana, huko kwengine ndo yanafanyika matayarisho ya uchimbaji, bado sana
 
Back
Top Bottom