KISIMA CHA WACHAWI

FM facts

Member
Mar 16, 2019
45
88
Hiki Kinaitwa Kisima cha Wachawi (Witch's Well), na Maji yanayotoka Hapa Muda Mwingine Huwa ni ya Moto, Kuna Historia Mbili Tofauti juu ya Kisima Hiki.

Kisima hiki Kipo Katika Nchi ya Jamhuri ya Estonia Kaskazini mwa Ulaya Katika Kijiji Kidogo cha Tuhala Kilichopo Kaskazini mwa Estonia. Hadi Kufika Mwaka 2011 Idadi ya Watu Katika Kijiji hiki ilikua ni Watu 105 tuu.

Historia ya Kwanza inasema Kwaamba Kisima Hiki Kinahusisha na Imani za Kichawi Ambapo Inasemwa Kuwa Hapo Kale Wachawi wa Eneo Hilo Walikua Wanafanyia Vita Vyao (Kupigana) Huko Chini ya Ardhi na Kusababisha Nguvu nyingi Kuja Juu ya Ardhi Hvyo Kusababisha Kutoboka kwa Sehemu hiyo ya Ardhi na Kutengeneza Kisima Hicho... na Wanasema Kuna Muda Wachawi hao Huwa Wanafufuka na Kuja Juu kama Mizimu Kupitia Kisima hiki.

Kuna Historia Nyingine inasema Kisima Hiki Kimetokea Kwasababu Chini ya Ardhi kuna Mito Mitano imepita na Wakati Mito hiyo Chini ya Ardhi ilivyojaa Maji, Maji yakawa yanatafuta Wapi Pakutokea Kuja Juu ya Ardhi na Ndio Kivyotokea Kisima Hicho.

Kisima hiki kina Urefu wa Mita 2.5 tuu na Maji Yanayotoka Hapo sio Maji ya Kawaida, Ni Maji yenye Rangi ya Brown na Kinatajwa kama Moja ya Maajabu ya Ulaya, Kinaogopesha!.

Inaelezwa Kuwa Msimu wa Wakawaida Kinatoa Maji hadi Lita 100 Kwa Sekunde Moja Lakini Wakati wa Masika Kisima hiki Kinatoa Maji mengi Hadi Lita 5000 kwa Sekunde Moja! na Kuna Muda Husababisha Mafuriko Kabisa na Hiyo ni Kutokana na Maji kuwa Mengi sna Chini ya Ardhi Yanayotoka Hapo.

Kijiji hiki Kina Historia Kubwa sana, Kina Umri wa Zaidi ya Miaka 3000.

Tufollow Instagram @fm_facts
maxresdefault.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom