Kisiasa, mwaka 2017 CCM imeimarika sana!

swali moja tu, hivi hawa wanaotuhumiwa kwa rushwa ni Chama gani vile,?akina bashite huku anatumia magari ya Wauza unga na mnyeti yupo ccm kweli?
 
Wezi haooooooo! Piga! Piga!

Mabina kabakia mbavu tu na fuvu kaburini! Chezea mawe weye!
 
Wewe na wanaokutuma.mna shida kubwa sana ya kufikiria ! Ccm hii ambayo uchaguzi wa ndani ulighubikwa na vitimbwi hata vya kumfanya mtu achaguliwe kwa 100% wakati inajulikana hata kikwete tu hajamchagua? Ccm iliyowazuia wenzake kukimbia/mikutano ya vyama hata ya ndani hamna wakati hata mwenyekit wake akienda kuzika anahutubia? Hahahaha ! U must think beyond mkuu..ni sawa na kwenda.mpirani kushangilia timu moja
 
Acha unafiki basi ndugu dah!!
Wameimarika kwa kuwazuia wengine kufanya shughuli za kisiasa kama walivyoruhusiwa na sheria!!

Ruhusuni na vyama vingine vifanye siasa,wawe huru kukutana na wananchi alafu ndo mje na hilo la nyie kukubalika ndo ntawaelewa
 
JPM NI CHAGUO LA MUNGU KWA WATANZANIA, MUNGU MBARIKI RAIS HUYU MPENDWA WA WATANZANIA.
Hauwezi kuachwa kwenye uteuzi wa watendaji wa tarafa mwezi Januari 2018. Umejitahidi sana, njozi za namna hii ndio zinatakiwa, ongezea na namba ya simu.
 
Imeimarika wapi? Kwa kutumia vyombo vya dola? Hii ndio ccm dhaifu kuliko zilizo wahi kuwepo tangu 1977. Hii iebebwa na polisi na jeshi. Hana lolote.
 
Watumishi wa umma heri awamu ya Kikwete
 
karibuni wanaccm tumpongeze na kumshangilia mwenyekiti wetu

Naona na wewe ni kati ya wale 'Senene' kikaangoni.Any way endelea kumsifu na kumubudu mungu wenu.
 
imeimarika kwa sababu inafanya biashara ya binadamu
 
Hapana haijaimarika,bali imeimarishwapolisisiem
 
Upinzani utaongelea lipi haswa zaidi ya kuzusha?
Kwani hayo uliyoyaandika si ni hisia zako tu lakini kiuhalisia hakuna kitu ni hewa! Umeona bei ya korosho tu lakini hujiulizi bei ya mahindi na mbaazi?
Kwenye rushwa tengua kauli. Sidanganyiki binafsi kwani sijaona lolote zaidi ya maigizo.
Kwenye ngada ndio kabisaaa usiseme lolote kwani hata bei imeshuka na wanaoiingiza ni ccm!
Mikopo ya wanafunzi imekaa kibaguzi na ili upewe ni sharti uonyeshe card ya ccm! Shame! Mlilofanikiwa kwa asilimia kubwa ni lile la kuiba kura za madiwani na kujitangazia ushindi na hili la kuwanunua wabunhe na madiwani kwa cash kama vitumbua! Shame again! Katubuni.
 
muadilifu lazima apambaniwe na waadilifu dhidi ya mafisadi waliotaka kuingia ikulu na kuitafuna nchi.
 
Kwahiyo katiba inaelekezaje mkuu au mnaikanyaga tu mjuavyo ninyi,

Je chama ca siasa kikifanya mikutano kwa ajili ya kujiimarisha ni kosa kubwa kwenu sio

Yaani mnapenda kusikia mnachokitaka tu sio
ACT Kila uchao wanafanya mikutano na kutoa maramko.
Chadema wanakutana kila mwezi na kutoa matamko...je ulisikiawamekamatwa?
 
ACT Kila uchao wanafanya mikutano na kutoa maramko.
Chadema wanakutana kila mwezi na kutoa matamko...je ulisikiawamekamatwa?
TUnataka ile mikutano ya hadhara watu wakaongee na wananchi kama hapo zamani
 
TUnataka ile mikutano ya hadhara watu wakaongee na wananchi kama hapo zamani
Wananchi wako makazini na shambani wakijenga Taifa nyie mnataka waandamane na kupigwa mabomu.
Naamini mwaka huu wananchi wengi wamepata ahueni ya kutokupigwa mabomu na kupata vilema vya maisha.

Kwenye mikutano ya kampeni mna fursa iliyo nzuri ya kuwahutubia wananchi.

Kama mna miradi mnayoitekeleza mna fursa nzuri ya kuongea na wananchi.

Kama ni kuhamasisha wananchi kujenga shule ,vyoo n.k fursa ipo.

Huu sio muda wa kuwafanya watanzania misukule wa siasa zenu za kimbea na kiharakati ili mpate clips za kuombea fedha ulaya.
 
CCM imefauru sana kwenye mwaka huu kwa kuwatumia wateule wa Ikulu kuwafanyia mazingaombwe ya siasa ya kuwanunua viongozi na wawakilishi wa wananchi kutoka upinzani ili kujifanya wanakubalika, niheri akuambiaye ulipo jikwaa kuliko kumziba mdomo na akaamua kukusenkenya kwa pembeni ilimradi tu uonekane fakini
 
Usiseme ccm imeimarika, sema uvunjwaji demokrasia na haki za binadamu vimeimarika na kushamiri 2017.
 
Sawa mlizuia bunge live kwa kauli kama zako hizo

Halafu kila siku mfalme yupo live
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…