Kishindo cha Rais Magufuli migodini chalipa

Wameandika:

Hiyo ni habari katika ukurasa wa mbele ila naamini itakuwa inahusu zaidi hizi sheria mpya za madini na sio yale makinikia.

Wahariri wetu siku hizi wamekuwa na tabia ya kutaka kuuza magazeti kwa njia ya kuandika headings za kumpaisha Mkulu.

--------------
KISHINDO cha Rais John Magufuli kuzuia kusafirishwa nje ya nchi mchanga wa madini maarufu kama ‘makinikia’ kisha kupeleka bungeni miswada mitatu kwa lengo la kubadili sheria ili kunufaisha taifa, kimeanza kuzaa matunda baada ya kuungwa mkono hadi ughaibuni.

Hali hiyo imetokana na mabilionea wa kampuni mbili za Australia na Canada zenye kujihusisha na shughuli za madini nchini kueleza namna zinavyomuunga mkono Magufuli (maarufu JPM), huku pia zikimpongeza na kuita hatua alizochukua kuwa ni za kizalendo.

Hivi karibuni, Magufuli aliunda kamati mbili zilizochunguza usafirishaji wa makinikia kwenda ughaibuni ambazo ripoti zake zilifichua upotevu mkubwa wa mapato kwa taifa.

Aidha, kutokana na matokeo ya ripoti hizo na mapendekezo yaliyotolewa, Serikali ilipeleka bungeni miswada mitatu iliyopitishwa kwa kishindo kuridhia mabadiliko kadhaa ya sheria, lengo likiwa ni kulinufaisha taifa na rasilimali tele ilizojaaliwa na siyo wawekezaji pekee.

Juni 29, mwaka huu, serikali iliwasilisha bungeni miswada mitatu inayohusu rasilimali za nchi ukiwamo muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2017, Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti hasi katika Mikataba ya Maliasili za nchi wa mwaka 2017, na Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa mwaka 2017.

Katika taarifa iliyochapishwa jana na gazeti dada la Nipashe la The Guardian, Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Royalty Exploration ya Canada inayofanya kazi zake nchini, James Sinclair, alisema uamuzi wa serikali wa kuwasilisha miswada kwa hati ya dharura bungeni ili kubadili sheria mbovu zilizopo ni hatua ya kupongezwa.

"Mapendekezo ya mabadiliko ya sheria yanalenga kuleta usawa katika rasilimali zinazopatikana nchini lakini tunaamini sheria hizo hizo pia zitaweka vitu vitakavyowavutia wawekezaji,” alisema.

Kampuni ya Tanzania Royalty Exploration Corporation, yenye makao makuu Toronto, Canada, inamiliki asilimia 55 ya hisa katika mradi wa Buckreef Gold Mine nchini na Shirika la Madini la Taifa (Stamico) linamiliki asilimia 45.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Sinclair akiwa nchini Canada, kampuni yake ya Buckreef Gold inaunga mkono mabadiliko hayo ya sheria yanayokusudiwa kufanyika nchini.

Aliwahakikishia wanahisa wake kuwa kupitishwa kwa miswada hiyo na hatimaye kuwa sheria baadaye hakutaathiri uendeshaji wa kampuni hiyo.

Alisema dhamira yake ni kushiriki kwenye maendeleo ya uchumi wa mataifa ya kigeni katika misingi ya usawa kwenye mikataba inayoingiwa.

Katika miswada iliyopitishwa bungeni wiki hii, serikali imeongeza tozo ya mrabaha kwenye dhahabu, fedha, shaba na platinum kufikia asilimia sita kutoka iliyokuwa asilimia nne na kupandisha hisa za serikali kwenye umiliki wa kampuni za madini kufikia asilimia 16.

Nayo Kampuni ya Australia ya Cradle Resources, ilisema kwenye taarifa yake kuwa mabadiliko ya sheria yatokanayo na miswada iliyopitishwa bungeni hayawezi kuwaathiri kwa kiasi kikubwa, ingawa mpango wake wa kutoa dola za Marekani milioni 55 zilizokuwa zimependekezwa zichukuliwe na wabia wake Kampuni ya Tremont Investments, umezimika kutokana na mabadiliko hayo.

Kampuni mbili zilizoko kwenye Soko la Hisa la Australia (ASX), zilisema kwenye taarifa yao kuwa zina imani kuwa uwekezaji wanaoufanya nchini Tanzania utakuwa wa manufaa licha ya mabadiliko hayo ya sheria za madini.

Walkabout Resources Limited ya Australia, ilisema mabadiliko hayo hayawezi kusababisha athari mbaya kwenye uendeshaji wa shughuli zao.

Ilisema kwa kushirikiana na wanasheria wa ndani na wa nje walifanyia upembuzi wa miswada iliyopitishwa na Bunge na kubaini kuwa itakuwa na manufaa hata kwenye mradi wake wa Lindi Jumbo.

“Tumepitia kwa makini mabadiliko hayo, tumeangalia athari zake kwenye miradi yetu na baada ya kusikiliza maoni ya wanasheria wa ndani na wa nje ya kampuni hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika ambayo yatasababisha kampuni kupunguza au kusitisha uwekezaji wake nchini Tanzania,” ilisema taarifa hiyo.

Chanzo: Nipashe

My take:
Wawekezaji waliokuwepo kabla ya hizi sheria mpya wanajua wana fursa ya kufanya majadiliano na si kulazimishwa na hata wakati wa JK tozo iliwahi kuongezwa kutoka asilimia 3 ya Mkapa mpaka 4 hivyo hili si jambo geni sana kama waandishi wanavyotaka kulikuza.

Siku hizi,kwa mujibu wa magazeti yetu, kila analofanya JPM ni kishindo!!
PR STUNT
 
Those Tanzanians with defeatist mentality need to reform and embrace positivity in approaching national matters. There is no single law than is full proof in handling numerous challenges facing this country. However, there must be starting point in this long journey. I really commend the current leadership for taking the initiative to start this journey of hope. Instead of sitting on the fence waiting for the leaders to bring home the scoop, we must participate in the walk while pointing out the right path where demeanor occurs.
What an inspiring comment!
 
Hii ni aibu sana kwa gazeti husika , unaweza kujiuliza hivi baada ya andiko la kishamba kama hili , watoto wa vyuo watapata mikopo ?
 
Pamoja na juhudi za serikali ya JPM, wananchi wanatakiwa kuendeleza mapambano haya, kila mmoja kwenye nafasi yake.
Kujenga uchumi imara ni muhimu kuwapa upendeleo maalum wazawa na kuwadhibiti wageni wanaotorosha rasilimali.
Msingi wa kuwa tajiri ni kuzuia ulichonacho kisitoke kwa kiwango kikubwa kuliko unavyokusanya kutoka nje.
Kamwe nchi haiwezi kuwa tajiri kama raia wake ni masikini. Ni lazima wananchi wawezeshwe kuwa na uwezo wa kiuchumi ili nchi iwe tajiri.
 
Jaman jaman waTz aliyeturoga kafa....hv unajua ni exploration companies ngapii zmesitisha kazi zake kutokana na huu muswada...ni vizuri hata ningeweka public announcements zao hapa huyo mleta mada azionee....na huyo sinclair hajakubaliana kabisa na legislation iliyotolewa...na ningekupa statements aliyoonyeshaa..kifupi ni kuwa hiz sheria zikipitishwa hamna mining company itakayokuja kufanya kazi hapa Tz ....trust me
Babu Nyerere aliyegundua uranium songwe na kuamua lijegwe gereza hakuwa mpumbav alifikiria mbali so acha waondoke cz hata walipo kuwepo hawakuwa na manufaa katika nchi kizaz chetu tumeshindwa so watachimba kizaz kingine au ww ulitaka waendelee kuchimba wakati tunapata hasara eti bro
 
.....
My take:
Wawekezaji waliokuwepo kabla ya hizi sheria mpya wanajua wana fursa ya kufanya majadiliano na si kulazimishwa na hata wakati wa JK tozo iliwahi kuongezwa kutoka asilimia 3 ya Mkapa mpaka 4 hivyo hili si jambo geni sana kama waandishi wanavyotaka kulikuza.

Siku hizi,kwa mujibu wa magazeti yetu, kila analofanya JPM ni kishindo!!
Utaratibu wenu wa kuishtaki serikali kwa sababu ya kuzuia kusafirisha makinikia umefikia wapi? Ebu nieleze asilimia tatu ya mrabaha ilikaa kwa muda gani kabla ya ile ya asilimia nne, na 4% imekaa muda gani kabla ya kuanza mazungumzo kupandisha tena na serikali ya awamu ya tano.
 
Kama kuna media ya hovyo kwa sasa kwa kujikomba kwa JPM ni IPP media

Nimejiuliza sana na kuhisi hawa jamaa (ITV) lazima watakuwa wametembelewa na "washauri nasaha" na kushauriwa kuhusu maafa makubwa yanayoweza kumfika mmiliki endapo hawatajiunga na "chorus" ya mapambio kumtukuza mkulu.

Naona kipaumbele namba moja cha Mheshimiwa ni kuhakikisha nchi nzima inasujudu kwenye madhabahu yake. Imagine, mzee Mwinyi, of all people, anaomba mheshimiwa atawale milele!
 
Hiyo ni habari katika ukurasa wa mbele ila naamini itakuwa inahusu zaidi hizi sheria mpya za madini na sio yale makinikia.

Wahariri wetu siku hizi wamekuwa na tabia ya kutaka kuuza magazeti kwa njia ya kuandika headings za kumpaisha Mkulu.

--------------
KISHINDO cha Rais John Magufuli kuzuia kusafirishwa nje ya nchi mchanga wa madini maarufu kama ‘makinikia’ kisha kupeleka bungeni miswada mitatu kwa lengo la kubadili sheria ili kunufaisha taifa, kimeanza kuzaa matunda baada ya kuungwa mkono hadi ughaibuni.

Hali hiyo imetokana na mabilionea wa kampuni mbili za Australia na Canada zenye kujihusisha na shughuli za madini nchini kueleza namna zinavyomuunga mkono Magufuli (maarufu JPM), huku pia zikimpongeza na kuita hatua alizochukua kuwa ni za kizalendo.

Hivi karibuni, Magufuli aliunda kamati mbili zilizochunguza usafirishaji wa makinikia kwenda ughaibuni ambazo ripoti zake zilifichua upotevu mkubwa wa mapato kwa taifa.

Aidha, kutokana na matokeo ya ripoti hizo na mapendekezo yaliyotolewa, Serikali ilipeleka bungeni miswada mitatu iliyopitishwa kwa kishindo kuridhia mabadiliko kadhaa ya sheria, lengo likiwa ni kulinufaisha taifa na rasilimali tele ilizojaaliwa na siyo wawekezaji pekee.

Juni 29, mwaka huu, serikali iliwasilisha bungeni miswada mitatu inayohusu rasilimali za nchi ukiwamo muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2017, Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti hasi katika Mikataba ya Maliasili za nchi wa mwaka 2017, na Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa mwaka 2017.

Katika taarifa iliyochapishwa jana na gazeti dada la Nipashe la The Guardian, Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Royalty Exploration ya Canada inayofanya kazi zake nchini, James Sinclair, alisema uamuzi wa serikali wa kuwasilisha miswada kwa hati ya dharura bungeni ili kubadili sheria mbovu zilizopo ni hatua ya kupongezwa.

"Mapendekezo ya mabadiliko ya sheria yanalenga kuleta usawa katika rasilimali zinazopatikana nchini lakini tunaamini sheria hizo hizo pia zitaweka vitu vitakavyowavutia wawekezaji,” alisema.

Kampuni ya Tanzania Royalty Exploration Corporation, yenye makao makuu Toronto, Canada, inamiliki asilimia 55 ya hisa katika mradi wa Buckreef Gold Mine nchini na Shirika la Madini la Taifa (Stamico) linamiliki asilimia 45.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Sinclair akiwa nchini Canada, kampuni yake ya Buckreef Gold inaunga mkono mabadiliko hayo ya sheria yanayokusudiwa kufanyika nchini.

Aliwahakikishia wanahisa wake kuwa kupitishwa kwa miswada hiyo na hatimaye kuwa sheria baadaye hakutaathiri uendeshaji wa kampuni hiyo.

Alisema dhamira yake ni kushiriki kwenye maendeleo ya uchumi wa mataifa ya kigeni katika misingi ya usawa kwenye mikataba inayoingiwa.

Katika miswada iliyopitishwa bungeni wiki hii, serikali imeongeza tozo ya mrabaha kwenye dhahabu, fedha, shaba na platinum kufikia asilimia sita kutoka iliyokuwa asilimia nne na kupandisha hisa za serikali kwenye umiliki wa kampuni za madini kufikia asilimia 16.

Nayo Kampuni ya Australia ya Cradle Resources, ilisema kwenye taarifa yake kuwa mabadiliko ya sheria yatokanayo na miswada iliyopitishwa bungeni hayawezi kuwaathiri kwa kiasi kikubwa, ingawa mpango wake wa kutoa dola za Marekani milioni 55 zilizokuwa zimependekezwa zichukuliwe na wabia wake Kampuni ya Tremont Investments, umezimika kutokana na mabadiliko hayo.

Kampuni mbili zilizoko kwenye Soko la Hisa la Australia (ASX), zilisema kwenye taarifa yao kuwa zina imani kuwa uwekezaji wanaoufanya nchini Tanzania utakuwa wa manufaa licha ya mabadiliko hayo ya sheria za madini.

Walkabout Resources Limited ya Australia, ilisema mabadiliko hayo hayawezi kusababisha athari mbaya kwenye uendeshaji wa shughuli zao.

Ilisema kwa kushirikiana na wanasheria wa ndani na wa nje walifanyia upembuzi wa miswada iliyopitishwa na Bunge na kubaini kuwa itakuwa na manufaa hata kwenye mradi wake wa Lindi Jumbo.

“Tumepitia kwa makini mabadiliko hayo, tumeangalia athari zake kwenye miradi yetu na baada ya kusikiliza maoni ya wanasheria wa ndani na wa nje ya kampuni hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika ambayo yatasababisha kampuni kupunguza au kusitisha uwekezaji wake nchini Tanzania,” ilisema taarifa hiyo.

Chanzo: Nipashe

My take:
Wawekezaji waliokuwepo kabla ya hizi sheria mpya wanajua wana fursa ya kufanya majadiliano na si kulazimishwa na hata wakati wa JK tozo iliwahi kuongezwa kutoka asilimia 3 ya Mkapa mpaka 4 hivyo hili si jambo geni sana kama waandishi wanavyotaka kulikuza.

Siku hizi,kwa mujibu wa magazeti yetu, kila analofanya JPM ni kishindo!!
Mkuu, wala usilaumu magazeti maana yapo magazeti yanayofanya vizuri. Ukweli ni kwamba gazeti la Nipashe, kama unafuatilia, uwezo wao wa kuchakata habari ni mdogo sana. Kwa IPP gazeti linalojitahidi ni The Guardian. Sasa ukisoma hiyo habari ya Nipashe inakuwia ugumu kuona namna 'kishindo kilivyolipa'!
 
Ndio maana nasema siku hizi Wahariri wameamua kuja na heading za kumsifia Mkulu.We chunguza tu magazeti utaona hiyo hali na huenda pia ni mbinu ya kutaka kuuza magazeti tu.
Ka-upepo ndivyo kalivyo. Na jua pia kuwa wanafamilia zinawategemea, ujue,
 
Acheni kushabikia vitu msivyovijua ndugu Watanzania
Huyo Bwana Sinclair toka amiliki hizo 50% hajawahi kuendeleza mgodi wa Buckreef.
Anaipaka Serikali mafuta kwa mgongo wa chupa.
....
Ndugu hii Buckreef ndo ile iliyopo kati kati ya Katoro na Rwamgasa ambao na mtoto wa mzee wa Msata ni mmiliki ?
 
Comrade Nsanzu
Hili la kuhusisha na mtoto wa mzee wa Msaga ni geni
More info please kama ikiwezekana hata kwa PM ili tujenge nchi yetu
 
hahahaaaa, hawa wazungu wanatudharau sana yaan wameshajua njia sahihi ya kukukubalika kwa hii serikali ni kumpongeza mkulu kwa nguvu ata kwa kla anachokifanya, sasa hapo matunda yaliyozaliwa ndo yap jaman mbona mnatukejeli hivo?
Wamefurahi kwa mapendekezo kuwa wazi.Hata wao sasa watakuwa na Nafasi ya kupata japo kidogo.ukanjanja kumiliki soko lote utapungua.
 
Back
Top Bottom