Kishimba, Msukuma, Tabasamu mnapotosha umma

Kishimba, Msukuma, Tabasamu mnapotosha umma

Congo

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2008
Posts
2,079
Reaction score
2,334
Nimewataja hao waheshimiwa wabunge wetu. Naheshimu ubunge wao. Lakini baadhi ya maneno yatokayo midomoni mwao yanaleta ukakasi.

1. Mtu atakuwaje mwalimu wa biashara wakati hana hata kiosk. Huu ni upotoshaji. Elimu ilianza bila kuandika mahali pppote. Maandishi yalippanza elimu ile ikaanza kuwekwa kwenye maandishi. Maandishi na elimu hiyo imekuwa ikiboreshwa siku hata siku mpaka tuliyonayo sasa hivi.

Hivyo iko kwenye maandishi. Yale maandishi ndio yanayofundishwa mashuleni na vyuoni. Faida inakuwa kabisa kama una elimu ile na ukafanya kile ulichosomea. Na mfano elimu ya biashara imetokana na matukio ya kawaida kabisa ya kibiashara yanayotokea kila siku.

Ola sasa matukio hayo yako kwenye maandishi. Mfano mfanya biashara yeyote awe amesoma au hajasoma anajua neno MTAJI WA BIASHARA.

Na heshima inatotakiwa kuwekwa ukishasema huu ni mtaji wa biashara. Elimu ikauweka kwenye vitabu ikauita CAPITAL na OWNER'S EQUITY.

Hivyo kusema mtu atafundishaje biashara hana kiosk ni upotoshaji mkubwa sana. Kuna elimu ya ujenzi wa barabara, je anayefundisha elimu hiyo unataka awe amejenga barabaraba yake?

2. Kulaumu wasomi kila kukicha. Nashangaa sana. Hivi barabara zetu, mahospitali yetu, mabenki yetu, maji, n.k. yataendeshwaje bila kutumia wasomo wetu? Wasichanganye taaluma na siasa. Hakuna taaluma ya wizi. Wizi ni uhalifu unashughulikiwa kama uhalifu mwingine. Kama watu wameiba wakajenga muundombinu mbovu sio kwamba walifundishwa hivyo. Hao ni wahalifu, na uhalifu wao ni jambo lao binafsi.

3. Sasa likaja kubwa zaidi. Hoja ya.kuvalisha ng'ombe hereni (ear tags) ikapongwa kwa nguvu zote, mtu akafikia kusema kumvalisha ng'ombe hereni ni ushoga. Hapo ndio tunajiuliza tunaelekea wapi. Mimi naelewa kuwa sio ng'ombe anatakiwa kivalishwa hereni, anatakiwa pia.kuwa na LOGBOOK yake.

Itakayoandikwa kila taarifa kuanzia siku anazaliwa, matibabu anayopata, lini ameoshwa, amebadilisha wamiliki wangapi n.k. Huwezi kuuza nyama nje kwenye nchi zilizoendelea bila kuwa na taarifa sahihi ya ng'ombe na hatimaye nyama.

Wenzetu wamefikia wanawamezesha vifaa maalumu vya kielektroniki. Taarifa zao zinasomwa kila hatua. KUPIGA CHAPA NG'OMBE ni mtindo umeshapitwa na wakati.

Mwisho, niwaulize hao Waheshimiwa. Hivi biashara zao hawana wahasibu? Je, nyumba zao wanajengewa na wasio mainjinia? Wanakiumwa wanaenda kwa waganga wa kienyeji?

Katiba yetu inasema ili kuwa mbunge LAZIMA ujue kusoma na kuandika.
 
At least ungeweka hata aya basi kwenye andiko lako ili kuweka mantiki katika ushauri wako.

Kwa uandishi huu kina Kishimba na darasa la 7 lao wanaonekana ma proffesor.
 
Kishimba anauelewa mpana wa mambo Elimu ya Tz inafuta ujinga na sio kuongeza maarifa

Jana alikuwa wasafi nimemsikiliza Sana they guy is very smarter upstair
 
usipo jirekebisha,

ulowataja watakushinda na kukuacha kwa mbali sana jinsi ya kuandika lakini pia jinsi ya kujenga, kutetea na kusimamia hoja 🐒

hata hivyo chuki binafsi haifai 🐒
 
Kuna baadhi ya wabunge wana tabia katika michango yao wanadharau taaluma za watu kwa maneno yao ya kejeli!

Kinara wao ni huyo “ msukuma” anayeamini kuwa elimu yake ya darasa la saba ni sawa na wenzie wenye makapu ya shahada!

Kwa kutukuza elimu yake ya darasa la. Saba na kwamba yeye ametoboa ( kwa magendo ya dhahabu) kunawafanya watoto wengi watoroke shule waende kwenye machimbo ya dhahabu kwani hawaoni faida ya elimu! Hii ni hasara kwa Taifa na hii tabia lazima ikemewe na chama cha ccm!

Msukuma kuwapiga madongo Wasomi ni kutokana na inferiority complex, na ndio maana amefanya chini juu akanunua cheti feki ili nae aitwe Dr.!!
 
Umeumia kwani wanakusema wewe? Hao wanaongelea wasomi wa Tz sasa wewe ni msomi?

Hata hivyo mbona waliyoyaongea ni kweli, unajaribu kutetea nini kwani. We unaona sawa mtu yuko busy kufundisha biashara ukimuuliza anakwambia anafundisha biashara chuo kikuu mwaka wa 25 lakini kweli hana hata biashara moja? We unaona ni sawa?

Anyways, huwezi kuelewa wewe.
 
Unakaa unamsikiliza msukumah aliyekimbia umande,kisa ana utajiri wa wizi wa madini🤣🤣🤣please
 
Msukuma na Kishimba ni wafanyabiashara za magendo, alikiri kwenye mikutano kanda ya ziwa mwaka jana.

Magendo hayahitaji elimu ya darasani ni wezi tu hao
Acha chuki

Kufanya magendo ni jinai.
Nchi imeweka vyombo kadhaa kudhibiti magendo.
TRA, TAKUKURU, Polisi, Mamlaka ya Chakula na Dawa nk .
Ina maana vyombo hivyo havifanyi kazi yake?
Mkuu hata wewe una nafasi ya kutafuta pesa kwenye nchi hii iliyojaa fursa za kila aina.
Pambana, acha chuki.
 
Nimewataja hao waheshimiwa wabunge wetu. Naheshimu ubunge wao. Lakini baadhi ya maneno yatokayo midomoni mwao yanaleta ukakasi.
1. Mtu atakuwaje mwalimu wa biashara wakati hana hata kiosk. Huu ni upotoshaji. Elimu ilianza bila kuandika mahali pppote. Maandishi yalippanza elimu ile ikaanza kuwekwa kwenye maandishi. Maandishi na elimu hiyo imekuwa ikiboreshwa siku hata siku mpaka tuliyonayo sasa hivi. Hivyo iko kwenye maandishi. Yale maandishi ndio yanayofundishwa mashuleni na vyuoni. Faida inakuwa kabisa kama una elimu ile na ukafanya kile ulichosomea. Na mfano elimu ya biashara imetokana na matukio ya kawaida kabisa ya kibiashara yanayotokea kila siku. Ola sasa matukio hayo yako kwenye maandishi. Mfano mfanya biashara yeyote awe amesoma au hajasoma anajua neno MTAJI WA BIASHARA. Na heshima inatotakiwa kuwekwa ukishasema huu ni mtaji wa biashara. Elimu ikauweka kwenye vitabu ikauita CAPITAL na OWNER'S EQUITY. Hivyo kusema mtu atafundishaje biashara hana kiosk ni upotoshaji mkubwa sana. Kuna elimu ya ujenzi wa barabara, je anayefundisha elimu hiyo unataka awe amejenga barabaraba yake?
2. Kulaumu wasomi kila kukicha. Nashangaa sana. Hivi barabara zetu, mahospitali yetu, mabenki yetu, maji, n.k. yataendeshwaje bila kutumia wasomo wetu? Wasichanganye taaluma na siasa. Hakuna taaluma ya wizi. Wizi ni uhalifu unashughulikiwa kama uhalifu mwingine. Kama watu wameiba wakajenga muundombinu mbovu sio kwamba walifundishwa hivyo. Hao ni wahalifu, na uhalifu wao ni jambo lao binafsi.
3. Sasa likaja kubwa zaidi. Hoja ya.kuvalisha ng'ombe hereni (ear tags) ikapongwa kwa nguvu zote, mtu akafikia kusema kumvalisha ng'ombe hereni ni ushoga. Hapo ndio tunajiuliza tunaelekea wapi. Mimi naelewa kuwa sio ng'ombe anatakiwa kivalishwa hereni, anatakiwa pia.kuwa na LOGBOOK yake. Itakayoandikwa kila taarifa kuanzia siku anazaliwa, matibabu anayopata, lini ameoshwa, amebadilisha wamiliki wangapi n.k. Huwezi kuuza nyama nje kwenye nchi zilizoendelea bila kuwa na taarifa sahihi ya ng'ombe na hatimaye nyama. Wenzetu wamefikia wanawamezesha vifaa maalumu vya kielektroniki. Taarifa zao zinasomwa kila hatua. KUPIGA CHAPA NG'OMBE ni mtindo umeshapitwa na wakati.
Mwisho, niwaulize hao Waheshimiwa. Hivi biashara zao hawana wahasibu? Je, nyumba zao wanajengewa na wasio mainjinia? Wanakiumwa wanaenda kwa waganga wa kienyeji?
Katiba yetu inasema ili kuwa mbunge LAZIMA ujue kusoma na kuandika.
kajifunze kuandika kwanza
 
Acha chuki

Kufanya magendo ni jinai.
Nchi imeweka vyombo kadhaa kudhibiti magendo.
TRA, TAKUKURU, Polisi, Mamlaka ya Chakula na Dawa nk .
Ina maana vyombo hivyo havifanyi kazi yake?
Mkuu hata wewe una nafasi ya kutafuta pesa kwenye nchi hii iliyojaa fursa za kila aina.
Pambana, acha chuki.
Muwe mnaacha ujinga basi?

Msukuma aliongea hadharani, tafuta video wakati Biteko anafanya mikutano alipopewa unaibu Majaliwa
 
Muwe mnaacha ujinga basi?

Msukuma aliongea hadharani, tafuta video wakati Biteko anafanya mikutano alipopewa unaibu Majaliwa
We hutaki pesa?
Umeenda shule huku una mawazo kuajiliwa upate mshahara.
Wenzako wamepambana mpaka wametoboa unakuja kuleta umbea wa kike.

Kama magendo ni kitu chepesi Nenda nawe ukafanye utoboe.
 
Unakaa unamsikiliza msukumah aliyekimbia umande,kisa ana utajiri wa wizi wa madini[emoji1787][emoji1787][emoji1787]please
Tunawasikiliza wasomi wasio na suluhu za umeme, Sukari na mfumuko wa bei.

Hawana prediction na solutions za kuzuia mpaka vitokee
 
Back
Top Bottom