Unanswered cries
Member
- Dec 2, 2015
- 13
- 1
Mbunge wa kahama mjini ndugu Jumanne Kibela Kishimba,ameoneshwa kukerwa na ufujaji mkubwa wa mali za umma mjini hapa.akizungumzia suala la miradi hewa iliyoidhinishwa na nadiwani waliopita pamoja na mkurugenzi aliyehamishwa ndugu Kimario kwenye kikao cha madiwani,mbunge huyo alisema," nimekerwa sana na tabia iliyojengeka miongoni mwa madiwani na watumishi wa umma kufuja mali za umma."wizi wa mabilioni yamepotea mjini hapa zikiwemo milioni mia nane zilizotolewa na mgodi wa ACASIA zamani Buzwagi kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa miradi mbalimbali.Baadhi ya madiwani walionekana kukerwa na msimamo huo wa mbunge akiwemo diwani mmoja wa viti maarumu aneyeitwa mama OUKO.lakini chama kiliingilia swala hili na kumuunga mkono Mbunge pia na kumpa baraka zote mh.mbunge atumbue majipu mjini hapa.