Mimi kama mkulima namkaribisha kwa furaha Mkuu wa Wilaya aliyechaguliwa hivi karibuni. Wenzake wote hilo tatizo limewashinda ama walizembea. We fikiria umelima mahindi na mihogo unataka kuvuna ndio ng'ombe 100 wanaingia shamba na hata ukishitaki kwa mwenyekiti unaambiwa hana mamlaka ya kukamata mhalifu, ila wewe mkulima unatakiwa ugharimie usafiri wa askari haipungui elfu 40 (wa pikipiki). Ili mwenye mifugo akamatwe.
Cha kushangaza mapori ni mengi. Ila ni kama kwa hapa DSM mtu badala ya kuchunga jangwani apeleke punda, ng'ombe na kondoo fire halafu wakate waingie msimbazi watokee shule ya uhuru. Ndicho kinachofanyika kila siku mpaka tunachangia visima na mifugo.
Akiiweza changamoto hii Wakulima wengi watapona. Hili ni tatizo la muda mrefu na chanzo ni viongozi vijiji Matamko kibao yametolewa na wakuu wa Wilaya bila mafanikio.