Kisanduku cha mayai.

tomjelly

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
560
Reaction score
198
BREAKING NEWS:
LEO Mama mmoja alikuwa anafanya
usafi chumbani
akakuta kisanduku chini ya uvungu.
Alipokifungua
akakuta mayai 5 na shilingi milioni 1. Aliporudi mumewe akamuuliza,
"Kisanduku hiki ni cha
nini pamoja na haya mayai?".
Mumewe akajibu kuwa amejiwekea
utaratibu kila akitoka nje ya ndoa,
ananunua yai na kuliweka kwenye kisanduku.
Mke wake (huku akifurahi) akasema,
"Kumbe mume wangu
umetoka nje ya ndoa mara 5 tu tangu
tuoane miaka 5 iliyopita?
Kumbe waliokuwa wanasema wewe muhuni ni wachonganishi tu.
Na vipi kuhusu
hizo milioni 1?".
Mume akajibu, "Huwa nayauza mayai
pindi yanapokuwa
mengi na pesa naziweka humo". Mke akadondoka chini na kuzimia.
★★★★ itaendelea akizinduka★★★★
 
Hahaaaaaa! Hii kali sana tuuu
 
Hajazinduka mpaka leo huyo wife au ndo kavuta

kazinduka mkuu, eti akawa anaziulizia zile milioni, huku anajichekeshachekesha. wanawake bhana. hata cjui niiendelezaje hii stori.
 
Kwa nini kwenye hizi story kila mara mwisho ni kuzimia?
 
Kwa nini kwenye hizi story kila mara mwisho ni kuzimia?

hata mi nashangaa!!!, ila ngoja ntawauliza wahusika / characters wa kwenye story hii, na wa story kama hizi. labda watakua na majibu kwanin wanazimiaga kila mwisho?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…