Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Meneja wa Huduma za Utangazaji katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka, amesisitiza kuwa midahalo ya kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025 lazima izingatie usawa na weledi ili isiwe na kasoro zinazoweza kupotosha taswira ya uchaguzi.
Akizungumza Agosti 16, 2025 jijini Arusha katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji Kanda ya Kaskazini, Kisaka ameeleza kuwa midahalo yenye washiriki wachache au usiokuwa na uwiano wa vyeo vya chama inapoteza maana na heshima yake.
“Kama mdahalo ni wa vyama vitatu na kimoja kikaahirisha, viwili vinaweza kuendelea. Lakini kama ni mdahalo wa vyama viwili na chama kimoja kikijitoa, huo si mdahalo tena. Vilevile, kama umeita Makatibu Wakuu, hakikisha wote ni Makatibu Wakuu na siyo chama kimoja Katibu Mkuu, kingine mweka hazina – huo si mdahalo,” amesema Kisaka.
Aidha, Kisaka ameonya juu ya upendeleo katika idadi ya wafuasi wanaoruhusiwa kuingia ukumbini, akibainisha kwamba kila chama kinachoshiriki mdahalo lazima kipewe nafasi sawa ya wawakilishi.
“Kama CCM imeruhusiwa watu 20, basi na CHADEMA wapate 20. Na hao watu wasiwe kundi la upande mmoja tu – changanya walimu, wafanyabiashara, manesi, vijana na wasomi ili ukumbi uakisi taswira halisi ya jamii,” ameongeza.