Jamani huyu kakutana kimwili na mpenziwe bila kutumia kinga, sasa huyo mpenzi wake anajistukia tu, hata hiyo mimba huenda hajapata, ni hofu tu inamsumbua, hivo amemwambia huyu mleta mada (mpenzi wa huyo dada) waachane na anaondoka mbali kama ni mtoto wake atamtafuta (hapa anajihami kama itakua amepata mimba) ndio atamtafuta. - nimewaelewesha huku nikitoa na majibu kimtindo.
Ushauri.
Kaka huyo mpenzi wako anasumbuliwa na woga na hofu, hapo anahisi tayari umempa mimba na pengine magonjwa hivyo hajiamini, na kama alikwambia hataki kushiriki bila kinga wewe hukumsikiliza hilo ni tatizo.
Cha kufanya hapo ni yeye kupima kujua kama amebeba mimba au la? ikiwezekana mpime na magonjwa pia. Mkiwa vizuri jaribu kwenda nae kwa akili, na umsikilize, mtadumu tu.
Nb:
Kama tayari mlishapima akakuta ana mimba useme, maana kwenye post hujaweka wazi, ulikua unawaya waya tu. Kama sijakuelewa na mimi njo u cancel hii kitu ili nisipoteze lengo lako.