Kisa kilichonifanya nikatafakari sana!

Muuza simu used

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
4,393
7,043
Nakumbuka ilikuwa mwaka 2012 nilikuwa nimerudi kutoka nchi X nikafikia Dar es Salaam walipo ndugu na Jamaa kwa vile asimilia kubwa ya ndugu wengi wapo Dar es Salaam!
Sema ukweli ilikuwa ni muda mrefu sijarudi nyumbani na mimi kawaida yangu huwa siagi naposafiri wala sitoi taarifa ninapowasili!
Ilikuwa ni takribani miaka kadhaa bila mawasiliano yeyote mara jioni familia wanapata chakula cha usiku mjuba nikatokea gafta watu wahakuamini waliona kama maajabu!
Kisa kilichonifanya niandike uzi huu ni kwamba nilionana na mjomba yangu japo nimemzidi miaka kadhaa na tulikuwa hatujaonana muda sana,sasa baada ya kupata msosi pale tukaondoka mimi na yeye kwenda kulala siku hiyo hatukulala ilikuwa ni story mwanzo mwisho huku yeye akiniuliza kuhusu maisha nje ya Tanzania yapoje na mimi nikimuuliza story za zamani kipindi nilimkuta bush etc!
Alitamani sana nisafiri nae nikirudi nikamuahidi kwanza ajipange kwanza mambo yakishakuwa poa nitampa ramani anifuate basi tukamalizana hivyo!
Ukweli sikukaa sana Tanzania kipindi hicho yaani ndani ya wiki moja nikawa na mpango wa kurudi nilipotoka lkn safari hii moyo ukawa mzito sana yaani kila nikitafakari safari naona giza!
Ilipofika siku ya kusafiri usiku wake nilikaa kwenye kochi nikawa naomba sana lkn moyo ukawa mzito hadi machozi yakawa yanalenga lenga lakini nikajikaza kiume!
Sasa kabla ya kulala nikawa napanga baadhi ya vitu kwenye begi nikatoa álbum ya picha huwa simpagi mtu hata iweje zaidi ya kuona picha na kuirudisha!
Nikaitoa nikampa huyo mjomba wangu nikamwambia uncle chukua hii albamu yangu sijawahi kumpa mtu hata mama alikuwa anaitaka ila sikumuachia sasa nakukabidhi wewe uitunze nikirudi nitaikuta kwako!
Lakini moyoni nilikuwa naona kama vile hatutaonana tena!ndio maana nilimpa ile albamu ya picha!
Yaani nilikuwa naona kama vile ile safari ndio itakuwa mwisho wangu maana moyo ulikuwa mzito sana!nilimpa ile albamu ya picha ili lolote likitokea iwe kumbukumbu!
Alichukua ile albamu ya picha akashukuru sana anasema asante sana uncle ukirudi utaikuta nitaitunza vizuri!
Basi tukaagana mimi nikatembea!
Sasa kumbe mimi nilipoondoka na yeye akapanga safari ya kwenda mkoani lkn kabla ya kuondoka alienda kumuaga bi mkubwa ambaye ni dada yake kwamba anasafiri anaenda mkoani mara moja ila akamuachia ile albamu ya picha akamwambia mimi nilimuachia kwa vile anaenda mkoani anaogopa anaweza kuipoteza kwa hiyo anamuachia ila akirudi ni lazima ataipitia maana yeye ndio mmiliki!
Basi wakaagana akasafiri kwenda mkoani,alivyofika mkoani sijui nini kilimkuta gafla alijinyoga akafariki!
Nilisikitika sana kusikia habari zake japo sikuweza kuhudhuria mazishi yake kwa sababu ya umbali ila huwa nakumbuka sana wakati namkabidhi ile albamu kumbe tulikuwa tunaagana mara ya mwisho moyo wangu ulikuwa ni mzito sana!
Lala salama uncle!
 
Dah pole sana, moyo unapokuwa mzito mara nyingi kuna sababu.
 
Uliposema moyo wako ulikuw mzito na ukaondoka ivo ivo.Nikahis labda utatuambia baadae ulikuja kufa
 
Back
Top Bottom