Nadhani issue ni upendo. Mmekua pamoja kwa miaka mitano. Je, imekua ni miaka ya furaha na amani? Upendo, kujituma, kujitoa sadaka? Je, mmefunga ndoa? Dhehebu gani? Ushauri wangu mchukue mke wako. Vijana wengi sana wa kike wanalaghaiwa na wanaume. Wanabaki wameumizwa sana. Hivyo wengi sana walikosea kabla hawajawapata hao walio nao. Ila lazima ujiridhishe katika nafsi yako. Watoto waweza kuwa sababu ya kumrudisha but that should not be the essence. The essence of every marriage is love. Hivyo hakikisha na wewe unapona hilo jeraha ili ukimrudisha umpe pia upendo wote kama mwanzo. Swali la kujiuliza ni kwamba, usingegundua, ungemfukuza? Kumbe kuna mambo mengi tuu hatuyajui. Najua inaumiza na maumivu haya huongezwa na kiburi cha uanaume. Kwamba mimi ni dume, inakuwaje anifanyie hivi? Kumbe pamoja na udume wetu, tuu wadhaifu sana. Watu makini tuu ndio wanaweza kutambua udhaifu wao. Kama ni Mkristi, samehe saba mara sabini, yaani infinitely. Kama wewe nk Mkristo na umefunga ndoa, bado utafungwa na kifungo cha ndoa. Kama hujafunga ndoa, huoni pia kwamba humpendi? Basi, jaribu kutafakari kwa ndani na ujihakikishie kua kweli umemsamehe. Huyo mtoto ambaye sii wako nadhani huhusiki sana. Ila asikutie uchungu sana. Tuko hapa duniani na kila mtu hupitia njia yake. Sii kila mtu ataoa bikira na sii kila mwanamwali anauwezo wa kuwa mke mzuri. Pia sii kila aliyekosea kabla ya kuolewa kwamba hawezi kuwa mke mzuri. Wanasaikolojia wanasema kuwa, wale wanaojikuta wameingia ktka mahusiano ya kimapenzi mapema are very loving pple. They are full of love and they wish to have a commitment as early as possible. Bahati mbaya huangukia mikono isiyo salama na matokeo yake ndio hayo. Hivyo njia yako ndio hiyo uliyoianza. Usilazimishe na wewe kuwa kama fulani aliyeoa mwanamwali. Huyu wako hujui atakuokoa wapi. Mchukue na umpende zaidi. Nikupe tahadhari. Hakikisha umeweza kusamehe na kukubaliana na hali halisi. Thats it is. Historia haitajiandika kivingine. Usijidharau. Hakuweza kukuambia na wachache sana huweza kusema wenyewe bila kuulizwa. Na huenda na wewe hukuuliza pia. Hivyo sii kwamba ulidanganywa, bali ujasiri ulikosekana. Hivyo sasa umejua, pokea. Tahadhari ni kwmba, epuka kulipiza kisasi. Wanaume wengi walipogundua hali za wake zao zinazofananafanana na yako, au waliwatesa wake zao au walipata kisingizio cha wao kuanza kutoka nje ya ndoa na matokeo yake wamekufa kwa ukimwi. Hivyo, umrudishapo, samehe na achilia yote. Hata kama utamwacha huyu wa sasa, una uhakika gani na huyo utakayemtafuta? Afadhali ni ipi: Aliyetoa mimba sita halafu anakuambia hana mtoto au aliyekubali majukumu ya malezi? Je, afadhali ni ipi?: Anayetumia vidhibiti mimba lakini ametembea na wanaume kumi au aliyeumizwa na labda na mwanaume mmoja? Hamna formula hapo. Ni busara na upole utakuokoa. Ila Mungu yupo kama unamwamini. Msikilize piaMwanaume alimzalisha akiwa form two akaishi nae kiunyumba miezi 6 bila Mimi kujua (alinificha) Mimi nikabeba mzigo nikauzalisha nikaishi nao miaka mitano nimeambiwa na wengine kwamba aliishi na mwanaume miezi sita kabla ya Mimi kuishi nae miaka mitano nikamfukuza sasa ameomba msamaha anataka kurudi nimkubali au nimwache maana ana watoto wawili kwangu na kwa mtangulizi wangu nimuache au nioe nijibuni haraka nataka kufanya maamuzi
Hahahah hapa ndipo ninapoamini kumbe akili inatofautiana au watu wanakaa na wanawake wakiwa na umri mdogoKwa hiyo jf ndio inakuamulia????
Kama miaka 5 uloishi nae hujui ufanye maamuzi yapi????
Anataka akalelewe watoto wakeKwani kabla ya kukutana nae wewe ulikuwa msafi kama malaika? Alishindwa kukuambia hilo kwasababu hakujua reaction yako, ukimwacha unatagemea watoto wawili uliozaa nae atawalea nani?
......... nimuache au nioe ........
Kakamua utamu sasa anataka kutupa makapi ya mua, huyo ni wako mkuu.kwahiyo miaka mitano yote ulikuwa hujamuoa bado !!?