Kisa cha Silvio Berlusconi kilichopelekea kushindikana kumleta Diego Maradona klabuni Milan

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
IMG_6389.jpeg

Alipo ulizwa kuhusu Diego Armando Maradona maarufu kama El Pibe di Oro yaani Golden Boy, Mzee Berlusconi alisema:

Nilitaka saana kumleta Maradona ili aje AC Milan akamilike na hata abebe mataji makubwa na yenye hadhi kwa mchezaji kama yeye.

Nilitaka pia aje na acheze kwenye Timu yenye wachezaji wa hadhi yake huku akilindwa na Nyota kama Costacurta, Baresi, Maldini, na kiungo mkabaji Demetrio Albertini.

Pia nilitaka aje apikiwe magoli na viungo kama Roberto Donadoni, Carlo Ancelotti, na Frank Riijkard. Kule mbele nilitaka ajumuike na Ruud Gullit, Marco Van Basten na Daniele Massaro.

Pia nilitaka kipaji chake kije kinolewe na Mwalimu wa Walimu, nilitaka saana Maradona afundishwe na Arigo Sacchi.

Nilikwenda kupiga hodi Klabuni Napoli na kueleza kuwa ninahitaji huduma ya Nyota wao. Lakini kabla sijajibiwa nilipokea taarifa toka Hospitali nyingi za Mji huo zikieleza kupokea wagonjwa wengi wa mshtuko wa Moyo.

Rafiki yangu na msaidizi wangu Adriano Galiani alinifuata na kunikataza mara moja kuendelea na mpango huo. Nilipomuuliza Galiani kwanini amekuja na hoja hio wakati mwanzo alinipa sapoti kubwa ili kufanikisha mpango huo?!

Galiani aliniambia kuwa Maradona ameshikilia mioyo ya washabiki weengi wa Napoli, na kama tukifanikisha kumng’oa Klabuni hapo basi wapo Watu ambao watakufa na hilo litakuwa laana kubwa maishani mwetu.

Endeleeni kupumzika kwa amani Hayati Silvio Berlusconi na Hayati Diego El 10 Peruso El Diaz Armando Maradona.

Watu wa Soka tutazidi kuwakumbuka kwa mchango wenu.
 
Aisee, Kwaio Unataka kusema nini?

Kwamba Watu Wa Napoli waliokolewa Kufa na Silvio .... bahati yao huyo Silvio Berlusconi hakumsajili Maradona tu. Au unataka kusema ndo kiumbe bora sana kuliko wote Duniani kwenye Soka .

Mimi nitakataa. Kuna Pele huyu ni balaa..
 
Kuna kitabu Darasa la Kwanza kinaitwa Soma kwa hatua…nahisi hukukisoma…
 
@Gang Chomba tuletee na stori za party za Berlusconi maarufu kama "bunga bunga".
 
Aisee, Kwaio Unataka kusema nini?

Kwamba Watu Wa Napoli waliokolewa Kufa na Silvio .... bahati yao huyo Silvio Berlusconi hakumsajili Maradona tu. Au unataka kusema ndo kiumbe bora sana kuliko wote Duniani kwenye Soka .

Mimi nitakataa. Kuna Pele huyu ni balaa..
Pele na maradona walicheza kwa miaka tofauti tofauti,pele kitambo kiasi kipindi hicho Ac millan haina ushawishi
 
Their is nothing like Serie A ya 80's - 90's. Vijana wa leo Wengi hawawezi elewa hicho kitu, Hata hii Super League hii inayopaganiwa sasa haitaweza kuifikia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom